Tafuta

Cookie Policy
The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the services. Furthermore, technical and analysis cookies from third parties may be used. If you want to know more click here. By closing this banner you consent to the use of cookies.
I AGREE
Gigue
Ratiba Podcast
Kupashwa habari kwa Bikira maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Kupashwa habari kwa Bikira maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. 

Kupashwa habari Maria:Mimi ni mjakazi wa Bwana nitendewe ulivyonena!

Leo Mama Kanisa anaadhimisha siku kuu ya Maria kupashwa habari kuwa atakuwa ni Mama wa Mungu.Papa Francisko amekuwa na ibada kuu kwa Mama Maria na kati ya sifa alizompatia anasisitiza kuwa:"Kujitolea kwa Maria sio nidhamu ya kiroho,bali ni hitaji la maisha ya Kikristo.Mama Maria ni msaini wa uandishi wa Mungu kwa wanadamu.Maria ndiye safina salama katikati ya gharika.Mkristo bila Mama Yetu ni yatima.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kupashwa habari kwa Bikira Maria, ni tukio muhimu sana kwa wakaristo hasa Wakatoliki na Waorthodox ambapo tangazo la Malaika Mkuu Gabrieli alipomtangazia Bikira na akakubali kuwa Mama wa Mungu kwa kuitikia: ‘Tazama mimi hapa mjakazi wa Bwana, nitendewe kama ulivyo nena”(Lk 1:35).

Leo tarehe 25 Machi 2025  Mama Kanisa anaadhimisha siku kuu ya Maria kupashwa habari kuwa atakuwa ni Mama wa Mungu. Baba Mtatifu Francisko kama Mapapa wengine watangulizi wake amekuwa na  ibada kuu kwa Mama Maria (inajionesha wazi ile ya "Salus Populi Romani) lakini hata hivyo  kati ya sifa alizompatia anasisitiza kuwa: "Kujitolea kwa Maria sio nidhamu ya kiroho, bali kuwa ni hitaji la maisha ya Kikristo. Mama Maria ni msaini wa uandishi wa Mungu kwa wanadamu. Maria ndiye safina salama katikati ya gharika. Mkristo bila Mama Yetu Maria ni yatima," na sifa nyingi sana ambazo ni vigumu kuzieleza zote.

Mama Yetu wa Mateso Saba. Katika mahubiri yake tarehe 3 Aprili 2020, kutoka Mtakatifu  Marta, Papa Francisko alizungumza kuhusu Mama Yetu wa Huzuni na kusisitiza umuhimu wa kutafakari juu ya mateso  Saba. Kwa namna ya pekee, alionesha unyenyekevu wa Maria: "Hakuwahi kujitafutia vyeo mwenyewe. Cheo muhimu zaidi kwa Bikira Mwenyeheri ni 'Mama', ambayo alipokea kutoka kwa Yesu mwenyewe. Na kwa hiyo, kama Mama tunapaswa kumfikiria, lazima tumtafute, tunapaswa kumwomba. Yeye ni Mama, na katika Kanisa Mama. Tutaendeleza...

Tuombe:

Mama Maria ni Mama wa Mungu

 

 

25 Machi 2025, 16:40
Prev
April 2025
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930   
Next
May 2025
SuMoTuWeThFrSa
    123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031