Vatican:Lazima Kutokomeza Utumwa wowote ule kwa njia ya Elimu!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Monsinyo Juan Antonio Cruz Serrano, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Baraza la Umoja wa Mataifa la Marekani (OAS), alizungumza tarehe 25 Machi 2025 mjini Washington katika kikao maalum cha Baraza la Kudumu la Shirika katika kukumbuka waathirika wa utumwa na biashara ya watumwa kupitia bahari ya Atlantiki (Transatlantic,) inayoadhimishwa na Umoja wa Mataifa kila mwaka Machi 25. Tukio hilo liliambatana na Juma la VIII ya Wamarekani Wenye Asili ya Kiafrika na elimu ya kijamii ya utumwa katika Bara ka Amerika.
Janga la utumwa mamboleo
Mwakilishi wa kudumu alibainisha kwa uchungu kwamba janga la utumwa halikutokea katika siku za nyuma tu: kwa bahati mbaya linaendelea kutokea hata leo na katika nchi kadhaa. Ikiwa tutafumba macho na masikio yetu kwa jambo hili, tutakuwa tukishirik" ndani yake, aliongeza, akinukuu maonyo ya Papa juu ya suala hilo. Utumwa unamlenga mwanadamu, ambaye thamani yake imepunguzwa kuwa ya manufaa kwa mtu au kitu, Papa Francisko alikuwa amesisitiza hayo mwaka 2023 na, hata mapema katika waraka wa Fratelli Tutti wa 2020, yaani Wote ni ndugu na alikuwa ametuhimiza kukumbuka daima bila kuchoka na bila kujiumiza sisi wenyewe, mateso, biashara ya utumwa na makabila mengi ya leo.
Juhudi za kuondoa utumwa kwa bidii ya elimu
Juhudi za kuondoa utumwa mambo leo , pamoja na majanga mengine mengi ya ulimwengu wa kisasa, zinapaswa kuwa kwa umoja, katika muktadha mpana wa wasiwasi wa kuanzisha michakato" inayoongoza amani yenye upatanisho muhimu kati ya watu, ambapo utambuzi wa hadhi ya mwanadamu unachukua nafasi kuu. Elimu na mafunzo, katika kuendeleza dhamira yake kupitia taasisi zake za kuhakikisha hali ya kutosha ya elimu na mafunzo kwa hiyo inalenga katika elimu ya maadili, kijamii na kiroho yenye uwezo wa kujumuisha uzoefu mpya na tofauti wa sekta hizo za jamii ambazo mara nyingi zimefanywa zisizoonekana na kunyamazishwa, kama ilivyo kwa waathiriwa wa biashara haramu ya binadamu. Kwa kumalizia, ujumbe wa Vatican uliwashukuru wale waliohudhuria kwa hisia za ukaribu zilizooneshwa kwa Papa, hata wakati wa kulazwa hospitalini.