Jubilei ya wagonjwa Aprili 5-6:Shuhuda hai wakati wa ugonjwa!
Vatican News
Katika ofisi ya waandishi wa habari mjini Vatica Ijumaa tarehe 4 Aprili 2025 iliwasilishwa baadhi ya shuhuda za madaktari na wasio, ambao ni wahusika wakuu katika tukio la kuishi Jubilei ya Wagonjwa na Ulimwengu wa kiafya, (5-6 Aprili 2025),mojawapo ya tukio kuu la Saba kwa Mwaka Mtakatifu, kama ilivyopangwa katika ratiba ya matukio makuu ya Jubilei. Miongoni mwa washiriki katika hatua ya mkutano huo, alikuwa Monsinyo Graham Bell, Katibu Msaidizi anayesimamia wa Baraza la Kipapa Uinjilishaji, Sehemu ya Masuala Msingi ya Uinjilishaji Ulimwenguni, na Dk. Lucia Celesti, Daktari katika Hospitali ya Kipapa ya Watoto Bambino Gesù, anayehusika na Mapokezi, ambaye alizungumza juu ya dhamira ya hospitali hiyo katika Jubilei hii yam waka Mtakatifu 2025.
"Tumaini ni sehemu ya DNA yetu. Watoto kutoka maeneo ya vita daima wamefika hospitalini, lakini na tunakuwa karibu sana pia ni wengi kama katika miaka ya hivi karibuni. Kukaribisha familia ambayo nyumba yao ilipigwa kwa bomu na ambayo inaweza kuhifadhi chuki ya kizazi kwa wale ambao walipiga nyumba zao, na kuwakaribisha kwa upendo, kiukweli inasaidia kuvunja mzunguko ambao ungekuwa na matokeo ya upendo ambayo yangekuwa na uwezo wa kusambaza baadaye."
Ukiona vifo vingi lazima uogope ila imani ni muhimu
Dk. Rocìo Bellido Octavio ni muuguzi katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Jorge cha Zaragoza na amekuwa na shughuli nyingi wakati wa janga hili alisema: “Unapoona vifo vingi, unapoona hali mbaya, unaona kwamba hudhibiti ugonjwa huo na kwamba hujui, unaogopa, lakini katika muktadha huu imani ni muhimu ili kufanya kazi kwa uhakika kwamba Mungu alikuwa pamoja nami. Imani, haikunisaidia kuelewa hali hiyo, ilinisaidia kuisimamia, kupata nguvu nilipokuwa sina iliyobaki, kuvuta pumzi nilipohisi kwamba ninaikosa,”alisisitiza.
Ushuhuda wa mwenyeheri Benedetta Bianchi Porro
Kwa upnde wa Padre Andrea Vena, Afisa wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na msimamizi wa Mchakato wa Kutangazwa Mtakatifu, Benedetta Bianchi Porro, alisimulia historia ya Mwenyeheri Benedetta Bianchi Porro kuwa: "Benedetta alifariki akiwa mchanga, historia yake ni ya sasa, ya kisasa, historia iliyooneshwa na machafuko makubwa. Mwishowe atabaki kuwa kiziwi, kipofu, amepooza na bado anaimba maisha, furaha, kukubali hali yake na kuikumbatia kikamilifu."