Kard.Re:Kardinali Tucci aliandaa ziara za kitume za Yohane Paulo II kwa dhati!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mkurugenzi wa Gazeti la La Civiltà Cattolica, mtaalamu wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican, mkurugenzi mkuu wa Radio Vatican na mratibu wa safari za Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili ndiye Kardinali Roberto Tucci, Mjesuit aliyeshikilia majukumu haya yote wakati wa maisha yake na alijipambanua “kwa roho yake kuu ya huduma na hisia ya uwajibikaji, siku zote akisukumwa na upendo kwa Mungu na kwa Kanisa, kuruhusu kujitokeza ubinadamu mkubwa, uwezo usio wa kawaida wa mazungumzo na namna ya adabu na watu. Haya ndiyo yaliyosemwa na Kardinali Giovanni Battista Re, Dekano wa Makardinali, akimkumbuka Kardinali aliyefanya huduma yake, kati wa kipindi cha Mtakatifu Yohane Paulo II kwa miaka mingi na ambapo Jumatatu asubuhi tarehe 14 Aprili 2025, Kardinali Re alimwita kama “ mtumishi mwaminifu wa Kanisa na wa Papa”, wakati wa Ibada ya Misa Takatifu iliyoadhimishwa katika kumkukizi ya miaka kumi ya kifo chake katika kikanisa cha jumba la Leone XIII mjini Vatican.
Alitangaza kifo cha Papa Yohane Paulo I
Liturujia hiyo ilihudhuriwa na Makardinali Emil Paul Tscherrig, ambaye katika miaka yake ya kazi katika Sekretarieti ya Vatican alishirikiana katika maandalizi ya safari za Karol Wojtyla, James Michael Harvey, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Nyumba ya Kipapa na Yohane na George Jacob Koovakad, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini na mratibu wa sasa wa ziara za Kipapa na pia Askofu Mkuu Renato Boccardo, wa Jimbo Kuu la Spoleto-Norcia, na Bwana Alberto Gasbarri, ambaye alishughulikia ziara za kitume za mapapa kuanzia 2001 hadi 2005 na 2005 hadi 2016. Pia walikuwepo Askofu Mkuu Piero Marini, Mshehereheshaji wa liturujia za Kipapa kwa miaka ishirini, pamoja na Karol Wojtyla na Joseph Ratzinger, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk. Paolo Ruffini na Katibu wa Baraza hilo Monsinyo Lucio Ruiz, Padre Federico Lombardi, aliyekuwa mkurugenzi wa zamani wa Radio Vatican na Msemaji mkuu wa Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican, ambaye mwanzoni mwa maadhimisho hayo alisema kwamba kaka yake Tucci alipokuwa mkurugenzi wa Radio Vatican, aliishi katika kile kiitwacho nyumba ndogo ambayo baadaye ilikuja kuwa monasteri maarufu ya Mater Ecclesiae mita chache kutoka Jumba la Leone XIII na alikuja kila asubuhi kwenye kikanisa kuadhimisha Misa kwa lugha ya Kilatini iliyokuwa ikitangazwa na Radio Vatican, na katika kikanisa hicho, kabla ya kuadhimisha Misa, alitangaza kifo cha Papa Yohane Paulo wa Kwanza. Lilikuwa tangazo la kwanza la kifo cha Papa Luciani.”
Urafiki na Wojtyla
Katika mahubiri yake, Kardinali Re alikumbuka urafiki kati ya Tucci na Wojtyla ulioanza wakati wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, kwamba wote wawili, kiukweli, mnamo 1965 walikuwa sehemu ya Kamati iliyowekewa vikwazo, ambayo ilikutana hasa huko Ariccia kuandaa maandishi ambayo baadaye yalikuja kuwa Katiba ya Kichungaji ya Gaudium et Spes juu ya Kanisa katika ulimwengu wa kisasa. Kuanzia mwaka 1973 hadi 1985, akiwa mkurugenzi mkuu wa Radio Vatican, Mjesuit uyo aliunga mkono maendeleo ya mtangazaji, akitoa maudhui kwa vipindi vilivyosikilizwa sana katika miaka hiyo ya mgawanyiko wa dunia katika kambi mbili. Sifa zake za kitaalamu katika ulimwengu wa mawasiliano ya kijamii kuwa bora, pia akiwa na ustadi mashuhuri wa usimamizi, anayejali sana watu,” alisisitiza Kardinali Re.
Pamoja na Paulo Paul II katika safari za kimataifa
Kama mkuu wa Radio Vatican na kama mwandishi wa habari, Kardinali Tucci aliandamana na Mtakatifu Yohane Paulo II katika ziara zake za kwanza za kitume na ushirikiano naye ukawa dhabiti na mkali zaidi mnamo 1982, kwa ajili ya kazi aliyokabidhiwa ya kutunza maandalizi ya ziara za kitume nje ya nchi ya Papa, jambo ambalo alilifanya daima kwa hekima na uwezo mkuu hadi mwaka 2001. Kardinali Tucci alishughulikia masuala yote ya maandalizi, alibainisha Kardinali Re akiongeza kwamba: mara tu Papa alipoamua mahali pa kwenda, mratibu wa safari alikwenda angalau mara mbili kwa taifa ambalo lingetembelewa. Alikuwa na ujuzi sana katika kutafuta njia za kufikia kile ambacho Baba Mtakatifu alitaka. Alikuwa na uwezo wa kukabiliana na hali ngumu zaidi kwa utulivu na uwazi. Kardinali Re aidha alisisitiza, akitoa mfano, zaidi ya hayo, baadhi ya safari ngumu na hata hatari, kama ile ya Nikaragua wakati wa Sandinismo, Uholanzi na sehemu nyingine.
Ukurasa mrefuwa maisha ya Kardinali Tucci kama mtu anayehusika na kuandaa safari za kitume, ilikuwa ni mchango wa moja kwa moja kwa Papa ambaye aliamsha hisia za kidini katika jamii na kuwa na matokeo katika historia ya ulimwengu. Kwa usahihi kama ishara ya shukrani na shukrani kwa kazi iliyofanywa na pia kwa roho ambayo alikuwa amejitolea kwa manufaa ya Kanisa, Papa Yohane Paulo II alimuunda Padre Tucci kuwa Kardinali mwaka 2001. Baba Mtakatifu Francisko pia alitoa muhtasari wa ushuhuda wake wa maisha katika telegramu aliyomtumia Mkuu Mkuu wa Shirika la Yesu wakati wa kifo chake, akisisitiza kuwepo kwake kwa bidii na nguvu kutumika kwa kufuata thabiti na ukarimu kwa wito wa mtu mwenyewe, kama mwangalifu wa kidini kwa mahitaji ya wengine na mchungaji mwaminifu kwa Injili na Kanisa.
Chumba cha mikutano katika jumba la Pio kilichowekwa jina lake
Mwishoni mwa maadhimisho hayo, chumba cha mikutano kilichopewa jina la Kardinali Roberto Tucci kilizinduliwa kwenye ghorofa ya pili ya Jumba la Pio, Jengo ambalo ni nyumbani kwa Vatican News, Radio Vatican, Osservatore Romano na Vatican Media na kuekwa bamba kwenye mlango wa Chumba hicho.
[ Photo Embed: Bamba linaloonesha Jina la Kardinali Tucci S.J]
“Yeye ni kielelezo kwetu sote, ili abaki kama mtu aliyefungua mlango wa umisionari,” alisema hayo Monsinyo Ruiz, huku akikumbuka kazi ya Wajesuit. Hapa ni mahali pa sisi kukutana pamoja ili kufikiria jinsi tunavyoweza kumpeleka Bwana hadi miisho ya dunia.” Baada ya sala ya kubariki Ukumbi huo wa mikutano, kwa kunyuzia maji ya Baraka Dk. Paulo Ruffini alifunua utepe wa Bamba hilo na kufungua ukumbi.