Papa afanya Teuzi za Mabalozi wa kitume wa Vatican kwa ajili ya nchi mbali mbali
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko,Jumamosi tarehe 12 Aprili 2025 amefanya teuzi mbali mbali katika matukio na ambapo ni pamoja na mabalozi wa Vatican kwa ajili ya nchi kadhaa: amemteua Balozi wa kitume wa Vatican kwa ajili ya visiwa vya Cook, Kiribati, na visiwa vya Marshall,huko Samoa na huko Nauru Askofu Mkuu Gábor Pintér, Mwenye makao yake Velebusdo, ambaye ni Balozi wa Kitume wa Vatican huko New Zeland, Fiji, Palau, na Nchi za Shirikisho la Micronesia na Vanuatu.
Baba Mtakatifu aidha amemteua Balozi wa kitume wa Vatican kwa ajili ya Nchi za Chini , Askofu Mkuu Jean-Marie Speich, mwenye makao yake Sulci, hadi uteuzi huo alikuwa ni Balozi wa Vatican huko nchini Slovenia na Mwakilishi wa Kitume wa Vatican huko Kosovo. Baba Mtakatifu hatimaye amemteua, Balozi wa Kitume wa Vatican nchini Ethiopia, Askofu Mkuu Brian Udaigwe, mwenye makao yake Suelli, hadi uteuzi huo alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Sri Lanka.