Unabii wa amani wa Papa Wojtyla,baada ya miaka 20!
Andrea Tornielli
Imepita miaka 20 tangu usiku ule wa Jumamosi tarehe 2 Aprili 2005, wakati milioni ya watu wa ulimwengu mzima walilia kwa sababu ya kifo cha Mtakatifu Yohane Paulo II. Miongo miwili baadaye anakumbukwa kwa kufaa kama mtetezi mkuu wa maisha, utu wa binadamu, na uhuru wa kidini. Na hasa ilisisitizwa saai kwa kupinga hasa ukomunisti. Walio wachache wanakumbuka kinyume chake Mafundisho ya kinabii, kwa namna ya wakati huu wa giza la kihistoria.
Ilikuwa ni mwaka 2000, sehemu moja muhimu sana katika dunia yetu iliyokuwa inaishi bado kwenye kulewa kwa “mwisho wa historia” baada ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlin. Wakati Nchi za zamani za Pazia la Chuma, zaidi ya kuzaliwa upya kwa imani, walikuwa wakianza kueneza tabia za kutumia kuzidi kiasi, na kutokuwa na dini, Baba Mtakatifu aliyekuja kutoka Poland alitaka kuleta katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Sanamu ya Mama wa Fatima, kwa kutangaza maneno ambayo hadi wakati huo hayakuwa yanaeleweka: Ubinadamu huko njia panda. Leo una vyombo vya nguvu visivyo na kifani: anaweza kufanya dunia hii kuwa bustani au kuipunguzia kuwa rundo la vifusi.” Mwaka mmoja baada ya mkasa wa tarehe 11 Septemba ilizirudisha nchi za Magharibi kwenye hofu.
Yohane Paulo wa II tayari kunako 1991 alikuwa anapinga vita vya Ghuba na kuachwa peke yake na viongozi hao wa Magharibi ambao hadi miaka miwili iliyokuwa imepita walikuwa wameinua nafasi yake kuelekea nchi za Ulaya Mashariki. Papa alirudia kwa uwazi kabisa ile ya “Hapana” vita kunako 2003 wakati, kwa msingi wa ushahidi wa uongo, baadhi ya nchi za Magharibi zilipigana vita na Iraq kwa mara ya pili. Papa Wojtyla, akiwa tayari mgonjwa, na kujaribiwa katika mwili na ugonjwa wa Parkinson, alihisi uwajibikaji wa kuonya wale “vijana” wakuu wa serikali wahamasishaji wa kampeni mpya ya wanajeshi katika Ghuba akiwakumbusha wao, vita vya mwisho vya kutisha vya ulimwengu, ambavyo kwake, mzee, mfuasi wa Petro na mtoto wa taifa la mashahidi alikuwa ameishi uzoefu wake binafsi. Aliongeza bila kusema bila maandishi katika tafakari ya sala ya Malaika wa Bwana wito huu: “Mimi ni wa kizazi kile ambacho kiliishi Vita vya Kidunia vya pili na kunusurika. Nina wajibu wa kuwaambia vijana wote, wale walio na umri mdogo kuliko mimi, ambao hawajapata uzoefu huu: “Kusiwe na vita tena!”, kama Paulo VI alivyosema katika ziara yake ya kwanza katika Umoja wa Mataifa. Tunapaswa kufanya kila tuwezalo.”
Leo hii kuliko hapo awali, ulimwengu ambao moto unawaka, na Mataifa ambayo yanakimbizana na kujaza silaha, kwa chochezi ambazo zinaunda hali ya kujihami, na hofu ya kuhalalisha uwekezaji mkubwa katika silaha, tunapaswa kukumbusha maneno yale ya kinabii ya Askofu wa Roma aliyekuja kutoka “Nchi ya Mbali”, leo yamejikita kutoka kwa mfuasi wakeX, ambaye ameachwa peke yake kupaza sauti dhidi ya wehu wa vita.