IFAD:Dunia yetu inachangamotisha watu Asilia!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Bwana Mattia Prayer Galletti Mtaalam wa kiufundi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo IFAD ametoa hotuba yake kwenye Semina katika mantiki ya Sinodi inayoendelea mjini Vatican. Semina hiyo meandaliwa na Mfuko wa Vatican wa Joseph Ratzinger-Benedikto XVI ikiongozwa na mada:Changamoto za Kanisa la Amazonia:ushirikiano wa lazima kati ya Mashirika ya kimataifa na Kanisa Katoliki na uongozi wa maadili. Katika hotuba yake amesisitizia umuhimu wa kushirikishana kuwasaidia watu asilia na walioko vijijini. Bwana Galletti anasema, jitihada kwa ajili ya watu asilia, na ambapo Shirika la IFAD ndiyo jukumu la kupambana na umasikini vijijini, kutokana na kwamba asilimia 75 ya masikini duniani wanaishi kwa hakika katika maeneo hayo.
Jitihada za Ifad zilianza miaka 30 iliyopita
Katika hotuba yake inasema kuwa jitihada za IFAD zilianzishwa miaka 30 iliyopit ana ambapo leo hii IFAD imetoa fedha ya miradi 63 katika nchi 32 katika kanda zote duniani na kufikia milini 6 za watu na karibu aina 150 za watu tofauti wa asilia. Aidha anasema kwamba, kuna zana mbili zilizotumika ili kufikia malengo. Awali ya yote ni kutumia zana ya fedha kwa ajili ya kutimiza miradi ya dhati hasa ya kukutana moja kwa moja na watu mahalia, na zana ya pili ni ile ya kutmua sera za kisiasa kwa njia kuandaa Jukwa za Watu asilia ambao wanapata fursa ya kufanya majadiliano ya kuendelea kati ya watu asilia, Mashirika ya kimataifa na serikali. Pamoja na hayo yote lakini ameorodhesha pia changamoto wanazokumbana nazo katika utendaji wa kazi na watu asilia: changamoto ya kwanza ni ya kiuchumi, hasa mbali na mitindo ya kiuchumi ya sasa, mahali ambapo ni wachache sana wanapokea na walio wengi wanapokea lakini kidogo sana. Watu asilia mara nyingi amesema wanaonekana kama kizingiti cha kuzuia mtindo wa uchumi hasa ule wa kutaka kurarua leo hii, lakini ki ukweli ni kwamba watu hawa wanaishi katika maeneo ambayo rasilimali nyingi zinaweza kutolewa au kuibwa, na pia kwa sababu kanuni zao ambazo wanaweka kama msingi wao wa maisha, ni zile za kushirikishana, za kutoa zawadi, za umiliki wa pamoja, za kukataa kutumia hovyo, na uwajibikaji na hizo katika hali halisi ndizo zinafungua vita vya wazi wazi na mtindo wa kutaka kutaka kuwamiliki. Kwa maana hiyo swali linakuja , je! Tuna uhakika kuwa hatuna chochote cha kujifunza kutoka kwao?
Uwajibikaji wa pamoja wa mali
Changamoto ya pili ni ile ya mazingira na hivyoBwana Galeetti anauliza tena swali je ni nani aliye bora zaidi kati ya watu wa asili ambao wanaweza kusema ni bora zaidi wa ulinzi wa kazi ya uumbaji kuliko wao? Watu hao ambao wameweza kuhifadhi na kuendeleza uhusinao wa nguvu na mazingira ambayo wanaishi kwa namna ya haki na dhati, mazingira ambayo wamefungamanika nayo. Na zaidi anasema katika dunia ya asili, nguvu ya asili ni kiini cha zana ya kitasaufi. Changamoto ya tatu ni ile ya utamaduni. Tamaduni za watu asilia ndiyo ufunguo wa uendeshaji wa rasilimali za sayari. Kazi yetu anasisitiza ni kujikita katika uhusiano na wazo la kisayansi, katika majadiliano yenye kujenga. Na hatimaye changamoto la nne ni lile la kisiasa. Bwana Galletti amethibitisha kwamba iwapo hatutafikia kutambua umuhimu wa kulinda haki za asili na kama ilivyo za wale walio wadhaifu na za kizazi kijacho, utambuzi rahisi wa matatizo hautatosha kupata suluhisho mwafaka na la kudumu!
Lazima kuwa na utambuzi wa uwajibikaji mbele ya maliz zetu za pamoja
Na suala la msingi ni utambuzi wa uwajibikaji wa pamoja mbele ya mali za pamoja. Na kanda ya amazonia ni mali ya pamoja. Lakini kuna suala ambalo haliwezi kuachwa bila kujiuliza: je kwa namna gani ya kufanya? Inatakiwa kutambua kuwa mali ni ya pamoja na ili kujikita ndani ya nyumba hiyo ya pamojana iwapo hatutambui mali yote kama ya binadamu wote pamoja, katika udugu wa kushirikiana, kuwa na maana moja ya hatima yetu, mahali ambapo lolote lile litakalo tokea katika sayari, kama vile vita, janga la asili, yote yanatugusa kwa kwa karibu na kusutukuma kujikita katika matendo ya dhati. Akihitimisha hotuba yake Bwana Gilletti anasema tena, Jumuiya ya kimataifa inahitaji watu wa asili. Bado tunahitaji kujifunza kutoka katika utamaduni unaotoa thamani ya uhusiano wa kijumuiya, wa kushirikishana kutafakari kwa kina heshima kwa ajili ya asili, kuwasiliana na kila kitu cha maisha.
Kufanya kazi kwa ajili ya mafunzi ya uongozi wa maadili
Aliyezungumzia umuhimu wa mafunzo ya uongozi wa maadili ili kutimiza maono katika ulimwengu wa leo, kuhama kutoka nafasi ndogo kwenda katika nafasi kubwa ya jumla, yaani ni ya ulimwengu, ni mtaalam wa elimu jamii Francisco Torralba ambaye ameelezea namna gani fadhi za uongozi mpya zinapaswa kuwa. Kwani mtu asiye na kiburi, lakini ukarimu, mwenye uwezo wa kujua jinsi ya kufanya kazi pamoja na wengine. Kazi msingi ya kiongozi, anasema, ni uwezo wa kujitoa zawadi yeye mwenyewe, talanta na uwezo wake, ili wengine waweze kukua bila kuchanganya mtu mwenyewe na huduma ambayo mtu anaitwa kuitenda na kwa maana hiyo uwezo kuwa shuhuda na ili kuendelea mbele. Amemnukuu Baba Mtakatifu Francisko ambaye anathibitisha: tunaishi katika mabadiliko ya wakati mwingine siyo tu kipindi kinachobadilika”, na hivyo anahitimisha akisema kwamba inahitajika mabadiliko ya dhana ya uongozi wa kisiasa ili kuweza kukabiliana na changamoto za leo na kesho.