Tafuta

Taarifa ya Jeshi la Polisi Temeke Dar es Salaam. Kuna watu 45 wamefariki dunia kati yao kuna wanaume 11 na wanawake 34. Majeruhi wa kukanyagana na kukandamizana ni 36 na kati yao 6 wako Muhimbili. Taarifa ya Jeshi la Polisi Temeke Dar es Salaam. Kuna watu 45 wamefariki dunia kati yao kuna wanaume 11 na wanawake 34. Majeruhi wa kukanyagana na kukandamizana ni 36 na kati yao 6 wako Muhimbili. 

Maombolezo ya Kifo Cha Dr. Magufuli: 45 Wafariki Dunia Dar!

Liicha ya Vikosi vya ulinzi na usalama nchini Tanzania kuimarisha ulinzi na usalama, kumejitokeza vifo vilivyosababishwa na msongamano pamoja na watu kukanyagana Dar. Watu 45 wamefariki dunia, kati yao kuna wanaume 11, wanawake 34. Majeruhi wa kukanyagana na kukandamizana ni 36 na kati yao 6 wamepelekwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Watanzania wanaendelea kuomboleza kifo cha Dr. John Pombe Magufuli, Rais wa awamu ya tano, aliyefariki dunia tarehe 17 Machi 2021 na anatarajiwa kuzikwa tarehe 26 Machi 2021 huko kijijini kwao Chato. Watanzania wanamlilia “Mtetezi wa wanyonge” kwa maana hawa ndio aliowapatia kipaumbele cha kwanza katika uongozi wake. Alikuwa mpiganaji mahiri aliyetaka kuona rasilimali na utajiri wa Tanzania unawanufaisha watanzania wengi. Alikuwa ni Jemedari hodari aliyeongoza mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi bila kupepesa pepesa macho! Dr. Magufuli alikuwa kweli ni “Jiwe”. Amevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo ameumaliza na imani ameilinda. Ni katika muktadha huu, watu wa Mungu Jijini Dar es Salaam, Jumapili tarehe 21 Machi 2021 walifurika kwenye Uwanja wa Uhuru kutoa heshima zao za mwisho kwa Hayati Dr. John Pombe Magufuli.

Taarifa ya Jeshi la Polisi nchini Tanzania (CHA/RB/2267/2021) inaonesha kwamba katika mchakato wa maombolezo na shughuli za kuaga mwili wa Hayati Dr. John Pombe Magufuli licha kuimarisha ulinzi na usalama, kumejitokeza vifo vilivyosababishwa na msongamano pamoja na watu kukanyagana. Watu 45 wamefariki dunia, kati yao kuna wanaume 11, wanawake 34. Majeruhi wa kukanyagana na kukandamizana ni 36 na kati yao 6 wamepelekwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi. Kutokana na maafa yaliyojitokeza Jijini Dar es Salaam, Serikali ya Tanzania imebadili mwelekeo wa tukio hili la kifaifa kwa kutoa nafasi kwa wananchi wengi kubaki barabarani, ili kutoa heshima zao, wakati mwili wa Hayati Dr. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kuagwa na wananchi wa Tanzania Visiwani. Watanzania wanahamasishwa kuendelea kusali na kumwomba Mwenyezi Mungu ili aweze kuwajalia amani, utulivu, upendo na mshikamano katika kipindi hiki kigumu cha historia ya Tanzania.

Maafa Tanzania

 

 

22 March 2021, 14:41