Tafuta

2021.08.30 wadudu 2021.08.30 wadudu  

Congo DRC:Ugonjwa wa Bubonic waibuka tena na kuleta hatari ya maisha kwa watoto

Kwa mujibu wa Shirika la kusaidia watoto linabainisha kuwa umaskini,mizozo na watu kutawanywa vimechangia kurudi kwa ugonjwa wa Bubonic nchini Congo DRC uliodumu kwa karne kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya muongo mmoja na utafiti mpya ulioungwa mkono na shirika la UNICEF umebaini watoto wako hatarini zaidi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kwa kuibuka tena kwa ugonjwa wa Bubonic unaosambazwa na viroboto kutokana na  wanyama kama panya na nguchiro kwenda kwa binadamu baada ya kuwauma na kisha binadamu aliyeambukizwa kuweza kuambukiza binadamu mwingine, kunawaweka hatarini maisha ya watoto na vijana katika jimbo la Ituri Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa mujibu wa taaarifa hivi karibuni iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, (UNICEF).  Umaskini, mizozo na watu kutawanywa vinachangia kurudi kwa ugonjwa huo uliodumu kwa karne kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya muongo mmoja, na utafiti mpya ulioungwa mkono na shirika hilo umebaini watoto wako hatarini zaidi.

Hii ni hatari kubwa kwa watoto. Utafiti wa UNICEF kuhusu ugonjwa huo ulilenga maeneo matatu ya afya huko Ituri, ambapo zaidi ya wagonjwa 490 wamerekodiwa kati ya mwaka 2020 na 2021, na vifo 20. Wagonjwa wengine 578, na vifo 44 vinavyohusiana na ugonjwa wa tauni unaosambazwa na panya pia, vilitokea katika jimbo hilo wakati huo huo. Naye Izzy Scott Moncrieff, msimamizi na mchambuzi wa masuala ya sayansi ya jamii wa UNICEF mahalia (CASS) amesema “Jambo la kutia wasiwasi hapa ni kwamba tumepata ugonjwa huo katika maeneo ambayo hayajawahi kuona visa hivyo kwa zaidi ya miaka 15, na wagonjwa wengi wao katika maeneo ambayo kulikuwa na wagonjwa wachache sana au hakuna kabisa hapo awali. Kuna athari mbaya kwa watoto kwa sababu wako kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa.”

Na uchafu ni kichocheo kikubwa: Janga la Bubonic, linalojulikana pia kama Black death, ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na bakteria wajulikanao kama Yersinia pestisbacteria, viroboto ambavyo kwa kawaida hupatikana katika Wanyama wadogo kama panya buku, panya wa kawaida na vicheche na wanyama hao wakimuuma binadamu wanamuachia viroboto hivyo vinavyosababisha ugonjwa na dalili zake ni uchungu na kuvimba malengrelenge yaitwayo kitaalam kama buboes.  Mlipuko wa ugonjwa huo mara nyingi unaibuka katika hali ya uchafu au mazoea duni ya usafi wa mazingira ambayo huvutia panya wanaobeba viroboto, kutafuta chakula, ambao huambukiza watu katika nyumba zao.

Ingawa ugonjwa huo unaweza kuwa na athari mbaya lakini, unatibika kwa urahisi na dawa za kuua wadudu.  Nchini DRC, hasa Ituri, Madagascar na Peru, ndio sehemu pekee ulimwenguni ambapo wagonjwa wa bubonic wanaendelea kuripotiwa. Kwa mujibu wa UNICEF imesema mlipuko wa sasa unatofautiana na ule wa awali kwa sababu pigo la Bubonic na aina ya ugonjwa wa homa ya mapafu, ambayo husambazwa kutoka kwa mtu kwenda kwa mtu kupitia hewa, vyote vimeripotiwa katika maeneo ambayo hapo awali hayakuwa na ugonjwa huo. Maeneo haya yako mashariki mwa jimbo la Ituri, karibu na mpaka na Sudan Kusini na Uganda.

Familia masikini ndio zilizo hatarini zaidi: Bi Scott Moncrieff amesema ugonjwa huo huambukizwa zaidi katika maeneo ya vijijini na viroboto viliyobebwa na panya wa porini. Familia masikini zinaweza kuathiriwa haswa. Yako Adhiku, mwenye umri wa miaka 40, anaishi katika nyumba ya matope yenye umbo la mviringo na paa la nyasi katika mji wa Aru, moja ya maeneo matatu ya afya katika utafiti wa UNICEF.  Kwanza aligundua kuwa binti yake, Asizu, ambaye ana umri wa miaka miwili, alikuwa amepata ugonjwa huo wa bubonic wakati alipopata uvimbe kwenye shingo.  “Pia alipoteza hamu ya kula, alikuwa na homa, na ufizi wake ulikuwa mwekundu sana," ameasema Bi Adhiku.  Kwa kuhofia kwamba mtoto atakufa, alimkimbiza katika kituo cha afya cha huko ambako alipewa vidonge kwa ajili ya binti yake na kila mtu katika familia, ikiwa na wao wangeambukizwa. Bi Adhiku aliwaambia watafiti kuwa mara nyingi alikuwa akiona panya wakirandaranda kuzunguka nyumba yake. Alikopa hata paka kujaribu kuwafukuza panya hao.  “Uwepo wa ugonjwa wa bubonic hapa unatufanya tuwe masikini inanibidi nibaki nyumbani kumuuguza mwanangu na kwa hiyo sina wakati wa kwenda shambani kulima tena.”

Kusaidia jamii zilizoathirika. Ingawa ugonjwa huo unatibika kwa urahisi na dawa za kuua wadudu, ambazo zinapatikana katika maeneo mengi ya afya huko Ituri, UNICEF imesisitiza kuwa ni muhimu kutafuta matibabu haraka. Ripoti ya hivi karibuni iligundua kuwa ingawa jamii katika maeneo matatu ya walengwa wanajua mambo ambayo yanaongeza athari zao kwa tugonjwa wa Bubonic, umasikini, mizozo na makazi yao yamezuia watu kuchukua hatua kujilinda na watoto wao. Hali hiyo inazidishwa zaidi na sababu za ziada, kama ukosefu wa rasilimali, ambayo inalazimisha watu wengi kulala kwenye sakafu kwa sababu hawana vitanda,  mazoea yasiyo salama ya mazishi, utupaji taka hovyo, na kutafuta huduma ya matibabu kupitia njia za jadi badala ya vituo vya afya vinavyotambuliwa.

UNICEF inaomba msaada ili kusaidia jamii zilizoathiriwa huko Ituri, pamoja na kupitia kampeni ya kutokomeza panya na viroboto na ujenzi wa nyumba zinazostahimili panya na wadudu hatari.   Shirika hilo pia linafanyakazi ili kusaidia kutoa vitanda kwa watoto vilivyotengenezwa kwa vifaa vinavyopatikana hapa nchini. "Tunataka kuwapa wazazi njia kila inapowezekana kuwapatia watoto vitanda na kuwazuia vijana wasilale chini ambapo wanakabiliwa na hatari zaidi kutapa bubonic kupitia kuumwa kwa viroboto," Bi Scott Moncrieff alisema. “Wakati huo huo, tunataka kuhakikisha kuwa wamiliki wa kaya na wakulima wadogo wanaweza kuishi katika mazingira salama na rasilimali za kuweka chakula na mifugo salama katika majengo tofauti na wanakoishi na kulala.”

30 August 2021, 14:29