Tafuta

COP26 huko Glasgow. Rais Samia Suluhu wa Tanzania akiwa kati kati ya Waziri Mkuu Boris wa Uingereza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Guterres. COP26 huko Glasgow. Rais Samia Suluhu wa Tanzania akiwa kati kati ya Waziri Mkuu Boris wa Uingereza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Guterres. 

COP26:Rais Samia Suluhu asisitizia utekelezwaji wa kukabili mabadiliko ya tabianchi

Katika mjadala wa wazi wa viongozi wamkutano wa COP26 huko Glasgow,Rais Samia Suluhu wa Tanzania amesema“Mipango yetu ni mtambuka katika sekta zote muhimu lakini hatuwezi kufanikisha bila usaidizi wa kutosha na teknolojia inayotakiwa ili kujenga uwezo wetu.Waheshimiwa kama hatutachukua hatua sasa tena kwa mshikamano,lengo la kuwa na kiwango cha joto kwa nyuzi joto 1.5 litatoweka punde na hatutalifikia.

Kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa.

Katika Mkutano ulifunguliwa mnamo tarehe 31 Oktoba 2021 kuhusiana na mabadili ya tabia nchi ambao unawajumuisha zaidi ya viongozi wakuu wa nchi 200 , mashirika yasiyo ya kiserikali na wanaharakati, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezungumza katika mjadala wa wazi wa viongozi kwenye mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP26 huko Glasgow, nchini Scotland na kubainisha juu ya mshikamano na juhudi zao kama viongozi katika kukabili mabadiliko ya tabianchi kwamba vitapimwa si kwa ahadi kubwa wanazotoa kwenye mkutano huo bali kwa jinsi watakavyo tekeleza vipengele vyote vya mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi. Rais Samia ametaja vipengele hivyo kuwa ni pamoja na kupunguza makali ya mabadiliko ya tabianchi, kuhimili mabadiliko hayo sambamba na uchangiaji wa fedha kulingana na kiwango cha changamoto zilizoko hivi sasa.

Rais Samia akiwa anatoa hoja katika COP26
Rais Samia akiwa anatoa hoja katika COP26

Rais Samia amesema, “mabadiliko ya tabianchi ni suala la dunia nzima na hivyo majawabu yake ni lazima yawe ya kimataifa na hivyo tunatoa wito kwa nchi zilizoendelea ambazo ndio zinaongoza kwa uchafuzi zitekeleze kwa vitendo ahadi zao za kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabianchi kwa kutoa fedha za kutosha kutuwezesha sisi nchi za kipato cha chini kufanikisha malengo yetu kwenye michango ya kitaifa ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwa uendelevu.”Rai Samia amesisitiza kuwa fedha za kutosha hususan kupitia misaada ya fedha itakuwa ni msingi katika mikakati yetu ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi. Akitoa mfano amesema nchi yake ya Tanzania na nyingine za kipato cha chini zimeandaa mipango ya kina ya NDCs ikiwa na mikakati dhahiri ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi.

Rais Samia wa Tanzania akiwa katika mkutano wa COP26, Glasgow, Scotland
Rais Samia wa Tanzania akiwa katika mkutano wa COP26, Glasgow, Scotland

Katika kuelezea Rais Samia amesema kwamba: “Mipango yetu ni mtambuka katika sekta zote muhimu lakini hatuwezi kufanikisha bila usaidizi wa kutosha na teknolojia inayotakiwa ili kujenga uwezo wetu. Waheshimiwa kama hatutachukua hatua sasa tena kwa mshikamano, lengo la kuwa na kiwango cha joto katika nyuzi joto 1.5 katika kipimo cha selsiyasi litatoweka punde na hatutalifikia".

02 November 2021, 17:12