Hunga Tonga-Hunga  Ha'apai :Volkano katikati ya bahari kisiwani  Tonga. Hunga Tonga-Hunga Ha'apai :Volkano katikati ya bahari kisiwani Tonga. 

Volkano,Tonga:UNICEF iko tayari kusaidia familia na watoto katika dharura

Shirika la kusaidia watoto UNICEF kwa upande wa Bahari ya Pasifiki,liko tayari kufanya kazi pamoja na serikali ya Tonga na washirika wake ili kuhakikisha msaada wa kuokoa maisha ya familia na watoto baada ya mlipuko wa Volkano chini ya Bahari na kusababisha dhoruba iliyowakumba visiwa na fukwe nyingi.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Mwakilishi wa UNICEF kwa ajili ya visiwa vya  Pasifiki, Jonathan Veitch amethibisha kuwa wako tayari kutoa msaada wa kibinadamu kwa serikali ya Tonga na watu waliopata pigo Tsunami na vumbi kubwa baada ya mlipuko wa Volkano chini ya bahari. Kwa maana hiyo UNICEF itafanya kazi na mamlaka, mashirika ya kijamii ya kiraia na washirika wengine kwa ajili ya maendeleo ili kuhakikisha jibu la haraka katika nyanja hiyo ambayo inajumuisha hutoaji wa maji safi na vifaa vya kiafya vya dharura kwa watoto na familia zilizokumbwa na mkasa huo. 

Hatari pia ipo kwenye visiwa vya Fiji, Samoa, Vanuta, Australia na New Zealand

Baaada ya majuma ya kazi ya volkano kwa utoaji wa majivu, kwenye maji ya Hunga Tonga Hunga Ha'apai  huko Tonga mlipuko wa  nguvu sana ulitokea mnamo tarehe 15 Januari , ambapo kwa mujibu wa vyombo vya kisatelite vinaonesha moshi mkubwa, majivu na gasi kuanzia kilometa 5 hadi 20,  juu ya Volkano na kuchafua kisiwa chote. Kwa dakika chache za mlipuko wa Volkano ulisababasha dhoruba au tsunami na kwa kukumba fukwe za Mji mkuu wa Tonga, Nuku'alofa. Na tahadhari hizo zielezwa pia kwa visiwa vya Fiji, Samoa, Vanuatu, Australia New Zealand.

Hakuna maji safi, chakula na uchafuzi wa hewa

Sehemu kubwa ya nchi iliangukiwa na majivu ya Volkano na kusababisha hukosefu wa maji  safi na chakula na zaidi uchafuzi wa hewa. Siku zijazo maji safi ya kunywa ndiyo itakuwa  shughuli kubwa yenye kipaumbele. Mawasiliano yalikatika tangu tarehe 15 Januari na kusababisha ugumu wa kupata habari kuhusu uharibifu. Hata hivyo mara baada ya kuthibitisha kutoka kwa Serikali, UNICEF  iko tayari kupeleka msaada wa kwanza wa dharura katika bohari za Fiji na za Brisbane. Msaada huo unajumuisha maji, vifaa vya usafi wa kiafya, mahema na vifaa vingine vinavyowezekana kusambaza kwa watu. Na kutokana na kufungwa kwa mipaka ya Tonga kwa sababu ya janga la UVIKO-19 linaloendelea, UNICEF itafanya kazi na Serikali na washirika wake katika nyanja ya kuweza kufikia watoto na familia ambazo wanahitaji msaada.

18 January 2022, 14:13