Ukame unaikumba sehemu ya Oromi nchini Ethiopia na mikoa ya Somalia. Ukame unaikumba sehemu ya Oromi nchini Ethiopia na mikoa ya Somalia. 

Ethiopia:Unicef,watu milioni 6.8 watakuwa na hitaji la dharura ya kibinadamu

Matazamio ya mwaka 2022,ni karibia watoto 850,000 watateseka na utapiamlo wa kukithiri katika vipindi vinne kwa sababu tofauti,miongoni mwake migogoro,ukame na kushuka kwa uchumi.Zaidi ya watoto 155.000 katika mikoa ya Somalia na Oromia nchini Ethiopia hawaendi shule kutokana na kwenda kutafuta maji.Ni taarifa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Vipindi vitatu vya majira ya mvua vilivyofuatana bila kunyesha mvua, vimepelekea ukame wa kutisha katika uwanda wa Ethiopia kwenye mikoa ya Afar, Oromia, kwa Nchi na Mataifa ya Kusini (SNNPR), na mikoa ya Somalia na kukauka madimbwi na visima, wanyama kufa kwa ukosefu wa maji na kusababisha mamia elfu ya watoto na familia zao kusukumwa kuhama makao katika hali ngumu zaidi. Muktadha wa ukame mbaya umethibitishwa na Gianfranco Rotigliano, Mwakilishi wa Shirika la Umaja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Etiopia. Kwa mujibu wake amesema, watoto na familia zao wanapambana namna kuishi kwa sababu ya kupoteza zana za kuishi na wakati huo huo inatarajiwa kuwa zaidi ya watu milioni 6,8 watakuwa na dharura ya kibinadamu kufikia katikati ya mwezi Machi 2022. Kwa maana hiyo shirika la UNICEF liko linatafuta njia ya kusaidia hata mrundikano wa watu katika maeneo yaliyokumbwa na baa hilo la ukame.

Uwanda wa Oromia Kusini, Mashariki na Mikoa ya Somalia

Mikoa iliyo kumbwa zaidi ni katika maeneo ya uwanda wa Oromia Kusini na Mashariki pamoja mikoa ya Somalia.  Kuna ukosefu wa maji safi na salama ya kunywa na vyakula ambalo linaendelea kusababisha kesi za utapiamlo kwa watoto. Inatarajiwa kuwa kwa mwaka 2022 karibia watoto 850.000 watateseka kutokana na utapiamlao wa kukithiri katika vipindi vinne kwa sababu tofauti, ambazo miongoni mwake ni migogoro, ukame na kushuka kwa uchumi. Katika maeneo yenye ukame Oromia na Mikoa ya Somalia, karibia watoto 225.000  wana utapiamlo wa kutisha na zaidi ya wanawake 100.000 wana ujauzito au wananyonyesha na wanahitaji msaada wa kumwilishwa, kwa mujibu wa Rotigliano msemaji wa UNICEF.

Watoto wasio kwenda shule wana hatari kubwa ya kunyonywa

Ukosefu wa maji salama umesababisha hali kuwa mbaya kwa watoto na wanawake. Ikiwa watoto wanalazimika kunywa maji machafu, wana hatari ya magojwa mbali mbali ikiwemo kuhara ambayo ni moja ya sababu kubwa ya vifo vya watoto chini ya miaka 5. Hadi kufika leo hii, maeneo yaliyokumbwa na baa  hilo huko Oromia na mikoa ya Somalia, karibia watu milioni 4,4 wako wanakabiliana na ukosefu mkubwa wa maji. Watoto wenu kwa sasa wamepoteza hata mafunzo yao kwa sababu ya ukame. Zaidi ya watoto 155.000 katika uwanda huo wa Oroma na Mikoa ya Somalia hawendi shule ili kuweza kusaidia utafutaji wa maji, ambapo wanalazimia kutembea umbali mrefu au wanatakiwa watunze wadogo zao wakati wazazi wao wanakwenda mbali kutafuta maji kwa ajili ya familia zao na wanyama wao. Watoto ambao hawendi shule wana hatari kubwa ya kunyonywa au  kuingia katika mantiki zenye hatar zaidi, amesisitiza msemaji wa UNICEF.

Wito wa UNICEF ili kusaidia maeneo ya Ukame nchini Ethiopia

Ili kweza kujibu jambo hili UNICEF imelazimika kuratibu na Mamlaka mahalia, kufanya kazi bila kuchoka ili kuweza kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa wale ambao wanahangaika na wanahitaji msaada. Shughuli hiyo inajumuisha kurudisha mabwawa na na visima na mifumo ya maji, usafirishaji wa dharura ya maji, kusaidia watoto wenye hali ngumu ya utapiamlo na kutoa mafunzo ya dharura wakati huo huo kutoa ulinzi wa watoto. Kutokana na hilo ndipo kuna wito wa jibu la UNICEF ili kuweza kukabiliana na maeneo yaliyokumbwa na ukame nchini Ethiopia ambapo wanahitaji dola milioni 31 za kimarekani ambayo ziweze kuongezwa kwa msaada wa kibinadamu wa dola milioni 351. Fedha hizi maalum zinalenga msaada maalum ili kuweza kufikia watu zaidi ya milioni 2 walioko katika hali ngumu kwenye mikoa ya Afar, Oromia, SNNPR na ya  Somalia.

02 February 2022, 14:36