Februari 28 ni Siku ya Kimataifa ya Magonjwa Adimu
Na Angella Rwezaula Vatican.
Miaka 15 ya Siku ya Ugonjwa Adimu: Kamwe asiwe peke yake mwenye ugonjwa adimu”, ndiyo kauli mbiu iliyochaguliwa kufanyika jijini Roma katika, Jumba la sanaa la Kitaifa la ‘Sanaa ya Kisasa na ya Kisasa’, kuanzia asubuhi saa 4.00 hadi saa 7.15 mchana. Ni katika fursa ya Siku ya XV ya Magonjwa Adimu Kimataifa ambayo hufanyika kila tarehe 28 Februari ya kila mwaka, ambapo katika tukio muhimu zaidi la mwaka inakadiriwa ni watu milioni 300 duniani wanaoishi na ugonjwa usio wa kawaida.Watafiti mbali mbali ulimwenguni wanaendelea kufanya hivyo na kuwepo kwa harakati nyingi zinazohamasisha uelewa wa hali halisi hiyo ndani ya kila jamii ulimwenguni.
Papa awatia moyo wenye ugonjwa adimu na watafiti
Baba Mtakatifu Francisko wakati wa salamu zake kwa waamini na mwahujaji waliofika kusali sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 27 Februari 2022, Papa pia alitoa salamu maalum kwa wote waliofika kwenye tukio la Siku ya Magonjwa Adimu ikiwa ni kesha lake. Kwa wao wote alisema: “Ninawatia moyo vyama mbalimbali vya wagonjwa na familia zao, pamoja na watafiti wanaofanya kazi katika uwanja huu. Niko karibu nanyi!
Shirikisho la Uniamoji-Italia la Magonjwa Adimu
Nchini Italia, kwa mfano katika Siku hii hupangwa na kuratibiwa na Shirikisho la “Uniamo-Italia la Magonjwa Adimu”, ambacho ni kituo cha kitaifa cha marejeo kwa zaidi ya watu milioni 2 walio na magonjwa adimu na familia zao. Kituo cha “Uniamo-Italia la Magonjwa Adimu”, kwa maana hiyo kimependa kuwashukuru wale wote ambao wameonesha usikivu fulani kwa masuala yanayowahusu kwa karibu na kuangazia changamoto za siku zijazo kupitia safari bora ya mgonjwa.
Azimio la Umoja wa Mataifa kwa changamoto za magonjwa adimu Desemba 2021
Siku ya Ugonjwa Adimu imefikia katika toleo lake la 15, tangu kuanzishwa kwake ambapo inamefika wakati muhimu ambao unakuja miezi michache tu mara baada ya kupitishwa kwa zana mpya ya kuhamasisha usawa ambapo ni Azimio la Umoja wa Mataifa la kushughulikia changamoto za watu wanaoishi na ugonjwa adimu na familia zao, lililopitishwa Desemba 2021 na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Azimio hili ni muhimu sana kwa watu wenye ugonjwa nadra au adimu, kwa sababu linalenga kukabiliana na changamoto za watu wanaoishi na hali hizi, wagonjwa na wanafamilia ili kuweza kuwapatia msaada.
Mipango nchini Italia ya kuhamasisha kujua magonjwa adimu
Mipango nchini Italia ya kuhamasisha sula la utambuzi huo wa magonjwa nadra au adimu, imepangwa kufanyika safari ya wagonjwa pia kwa mwaka huu watasafirishwa ndani ya tramu mbili ambazo zitavuka barabara kuu za Roma na Milano kwa lengo la kutangaza habari za magonjwa adimu na kuwaleta raia karibu sana na changamoto za wagonjwa na familia zao. Pia kutakuwa na tangazo la televisheni na Benedetta De Luca, mwanamitindo mwenye ushawishi na ulemavu aliyezaliwa na ulemavu wa nadra wa kuzaliwa, na tangazo la radio kwa ushirikiano wa "RadioAIdel22", maabara ya kwanza ya radio ya Italia ndani ya chama cha kukuza kijamii kinachojitolea kwa ugonjwa adimu.