Wakimbizi ni wengi na watoto na familia zao  kutoka Ukraine kwenda nchi za jirani Wakimbizi ni wengi na watoto na familia zao kutoka Ukraine kwenda nchi za jirani 

Umoja wa Mataifa:wakimbizi milioni 1 kutoka Ukraine

Leo ni siku ya nane tangu kuanza kwa uvamizi wa jeshi la Urusi,nchini Ukraine kuendelea kuongezea dharura ya kibinadamu.Tume kuu ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi Filippo Grandi aliripoti juu ya bahari ya watu ambao wameondoka nchini kufikia nchi jirani.Wakati wa usiku,milipuko mipya huko Kiev.Na leo duru mpya ya mazungumzo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mabomu ya nguvu yamesikika hata usiku huko Kiev na sehemu nyingine za mji huko Ukraine, mahali ambalo wanaendelea kutoa habari za dharura ili watu wajifiche chini ya ardhi Vyombo vya habari mahalia vinabainisha kuwa hata mapigano nje ya mji wa Kiev. Adui anatafuta kuingia,  kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Meya wa mji,  Vitali Klitschko. Huko Kharkiv Mapigano yalishambulia zaidi majengo ya shule na Kanisa la Maria Mpalizwa. Vikosi vya kijeshi vya Urusi vipo hata upande wa Kusini, kutokea Crimea. Jana walichukua uthibiti wa Kherson na kubaki wamezunguka eneo la Mariupol, mji ambao umebaki bila kuwa na maji na mamia ya watu waliojeruhiwa na katika maji ya Odessa, zimefika meli za kivita za Urusi. Takwimu za waathirika bado haijajulikana, Waziri wa Ulinzi huko Urusi amesema wanajeshi wake 500 wameuawa, lakini Kiev ni zaidi ya waathirika 5.800 na zaidi ya raia elfu mbili wameuawa. Vyanzo vya habari kutoka Marekani linakadiri kuwa waru 1500 wameshakuwa na zaidi wa Ukraine.

Wakazi wakiwa kwenye foleni wakipokea chakula huko Kharkiv, Ukraine
Wakazi wakiwa kwenye foleni wakipokea chakula huko Kharkiv, Ukraine

Katika ujumbe wake mpya  uliotolewa na  Rais wa Ukraine Zelensky, alisema kwamba: “Hapa hautakuwa na amani, hautakuwa na wakati wa utulivu”. Hata hivyo siku ya Alhamisi tarehe 3 Machi 2022, kuna duru mpya  mazungumzo ya pili kati ya Belarus huko Brest, kati ya wawakilishi wa Moscow na Kiev. Ni matumaini kwambaduru ya siku inawezekana kusitisha moto, wakati Waziri wa nchi za Nje wa Urusi Lavrov amebainisha kuwa moja ya lengo la uperesheni ni uondoaji kamili wa kijeshi wa Ukraine. Wakati huo huo, chanzo cha habari kutoka serikali mjini Berlin kinaripoti kuwa Ujerumani inajiandaa kutuma makombora mengine 2,700 ya kutangulia ndege nchini Ukraine. Na katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Kamishena wa Uhusiano na Nje wa Umoja wa Ulaya Bwana Chris Patten amesema Mgogoro huu wa Urusi na Ukraine tayari unaathiri sehemu kubwa ya ulinzi na usalama wa raia, hasa wanawake na wasichana, ambao wako katika hatari kubwa ya unyanyasaji. Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya Bwana Patten ametoa wito kwa pande zote kuzingatia haki za binadamu na utu wa watu wote, kujizuia, na kuhakikisha wanafuata sheria za kimataifa za kibinadamu na haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na upigaji marufuku wa aina zote za unyanyasaji wa kijinsia.

Wakimbizi kutoka Ukraine wakiwa katika mpaka wa Poland wanapewa msaada na Caritas
Wakimbizi kutoka Ukraine wakiwa katika mpaka wa Poland wanapewa msaada na Caritas

Mapigano hayo yamesababisha watu wengi kulazimika kuyahama makazi yao, hali iliyowalazimu raia wengi kukimbilia nchi jirani. Iwapo mzozo huo hautakoma, maelfu ya familia za ziada zitahamishwa kwa nguvu, na hivyo kuongeza kwa kasi kiwango cha hali mbaya ya kibinadamu ambayo tayari ipo na kuongeza hatari ya unyanyasaji wa kijinsia na unyonyaji. “Ninaunga mkono wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kukomesha mara moja uhasama na kutoa wito kwa upatikanaji usiozuiliwa wa misaada ya kibinadamu kwa wale wanaohitaji, hasa wanawake na wasichana. Pia nitoe wito kwa wahusika wote kujiepusha na kushambulia huduma muhimu za afya na miundombinu mingine ya kiraia, ambayo ni muhimu katika kuhakikisha upatikanaji endelevu wa huduma, ikiwa ni pamoja na huduma ya afya ya ngono na uzazi na usaidizi wa kisaikolojia kwa waathirika wa unyanyasaji wa kingono na kijinsia”. Mwakilishi Maalum Patten pia ametoa wito wa kupewa kipaumbele kwa msaada wa kuokoa maisha kwa waathirika wa unyanyasaji wa kingono na kijinsia wakati wa kutoa misaada ya kibinadamu.

Wakimbizi wakiwa wamjifunika kwenye kituo kikuu cha Treni huko Kiev
Wakimbizi wakiwa wamjifunika kwenye kituo kikuu cha Treni huko Kiev

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hata hivyo limezungumza na kama Katibu Mkuu ni wajibu wangu kusimamia azimio hili na niongozwe na wito wake,” amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati akizungumza na waandishi wa habari punde tu baada ya Baraza hilo kupitisha azimio kuhusu  uvamizi wa Ukraine uliofanywa na Urusi. Azimio hilo limepigiwa kura ambapo nchi wanachama 141 wa Umoja wa Mataifa wameliunga mkono huku 5 zikipinga na 35 hazikuonesha msimamo wowote. Katibu Mkuu amesema “ujumbe wa Baraza Kuu ni thabiti na dhahiri. Maliza chuki nchini Ukraine sasa! Sitisha mashambulizi sasa! Fungua milango ya mazungumzo na diplomasia sasa! Mamlaka ya kieneo na uhuru wa Ukraine lazima viheshimiwe kwa mujibu wa Chata ya Umoja wa  Mataifa.” Bwana Guterres amesema kwa sasa hakuna muda wa kupoteza.

 

03 March 2022, 11:55