Tafuta

 Waziri wa Indonesia amesema atapeleka barua ya mwaliko kwa Papa kumkaribisha atembelee nchi yao. Waziri wa Indonesia amesema atapeleka barua ya mwaliko kwa Papa kumkaribisha atembelee nchi yao. 

Indonesia,Waziri wa masuala ya kidini:Ninapeleka barua ya mwaliko kwa Papa

Waziri wa Mambo ya Kidini wa Indonesia Bwana Menag RI Yaqut Cholil Qoumas,aliyefika tarehe 23 Aprili 2022 katika Visiwa vya Molucche ili kushiriki maadhimisho ya kutoa daraja la wakfu wa kiaskofu kwa Askofu mpya Senno Ngutra wa Jimbo la Amboini aliwaeleza nia yake ya kwenda Roma kumpatia mwaliko Baba Mtakatifu ili atembelee nchi yao.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Nchi ya Indonesa, inataka kumwalika Baba Mtakatifu kutembelea nchi hiyo. Amesema hayo kwa Balozi wa Vatican Askofu Mkuu Pietro Pioppo na kwa Maaskofu Katoliki nchini Indonesia, Waziri wa Mambo ya Kidini Menag RI Yaqut Cholil Qoumas, aliyefika mnamo tarehe 23 Aprili katika Visiwa vya Molucche ili kushiriki maadhimisho ya kutoa daraja la wakfu wa kiaskofu kwa  Askofu mpya, Senno Ngutra wa Jimbo katoliki la Amboini nchini Indonesia.

Waziri huyo akikutana na  Balozi wa Vatican, Maaskofu na mapadre wa Indonesia katika Kituo Katoliki cha Amboini, kabla ya maadhimisho makuu ya Ekaristi kwa ajili ya Wakfu wa kiaskofu Bwana Menag RI alielezea juu ya ziara yake anayotarajia kufanya mjini Vatican, ili kuweza kukabidhi yeye binafsi ujumbe na mwaliko rasmi  kwa Baba Mtakatifu ili aweze kutembelea nchini Indonesia.

Awali, Vatican ilikuwa imekubaliwa na tangazo rasimi kuhusu shauku ya Baba Mtakatifu kuitembelea nchini Indonesia na Timor Est mnamo Septemba 2020, lakini ziara hiyo iliyokuwa katika hatua ya uchunguzi kwa ghafla ilifutwa kutokana na janga la Uviko -19. Waziri Menag RI Qoumas baadaye alielezea kuwa Serikali ya Indonesia lengo la kuhamasisha ujenzi mpya wa Kanisa Kuu huko IKN Nusantara, ambao utakuwa  mji mkuu wa Indonesia kwa upande wa  Kalimantan ya Mashariki. Kwa sababu hiyo wako wanaratibu na Askofu mahalia katika Jimbo Kuu la Samarinda, Askofu Mkuu Yustinus Harjosusanto,  alisema Waziri huyo.

Zaidi  ya hayo Waziri wa Mambo ya Kidini ana lengo la kutaka kufikiria siku kuu mbili kikristo kitaifa  ambazo zinahusu: “Siku ya Kupaa kwa Bwana na siku ya Pasaka kwa jina  “Isa Al Masih” zibadilishwe rasmi katika neno la Kristo, kwa sababu ya kupokea maombikutoka  jumuiya ya Kikristo nchini Indonesia. Na katika hotuba yake mara baada ya kuwekwa wakfu, Askofu mpya Senno Ngutra, wa Jimbo la Amboini, ambaye katika siku za nyuma alishirikiana kikamilifu na vijana katika kuongeza uelewa wa dini mbalimbali, alimwelekea Waziri huku akiialika serikali kuendeleza mshikamano wa kijamii na kuvumiliana baina ya dini na  si tu katika maneno ya hotuba bali kwa mipango na matendo madhubuti ili kuleta manufaa yenye matunda katika jamii ya nchi yao.

27 April 2022, 11:20