Mexico:Maaskofu wapyaisha jitihada ya upendeleo wa wadhaifu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika mpango wa kichungaji wa kimataifa, Maaskofu wa Mexico wamerudia lengo la huduma yao ya kuhinjisha kuhusu upendeleo kwa watu walio hatarini zaidi katika jamii, ambayo leo wanatambua nyuso za wahamiaji, wanawake, watoto, vijana na wazee wanaoteseka, na vile vile katika ile ya jamaa za watu waliopotea (maelfu ya waathiria waliotoweka wa vikundi vya uhalifu. Wakikabiliwa na ukweli huu ambao unawaumiza sana, wamejitolea kuwa Kanisa la sinodi na tegemeo zaidi, ambalo linatangaza na kutetea utu na kushirikiana katika ujenzi wa mfumo wa kijamii kutokana na kukutana na Kristo Msulubiwa na Mfufuka.
Kugundua upya tumaini
Hilo ni lengo la Baraza la Maaskofu wa Mexico (Cem), ambalo limetokwa katika ujumbe wao kwa watu wa Mungu uliotolewa tarehe 27 Aprili wakati wa mkutano mkuu wa Baraza la Mawaziri uliomalizika tarehe 28 Aprili sambamba na mkutano wa kitaifa wa Kanisa hilo. Hati hiyo iliwasilishwa katika mkutano na waandishi wa habari, na Rais Askofu Mkuu Rogelio Cabrera wa Baraza la Maaskofu Mexico (Cem) na katibu mkuu, Askofu Ramon Castro. Kwa imani hiyo ujumbe unasomeka kwamba wao wangependa kugundua tumaini, zaidi ya sifa za kawaida za nyakati zao za mabadiliko, ambayo, licha ya ukuu wa mwanadamu na hadhi yake, inaibuka kwa nguvu kubwa kukadiria kupita kiasi kwa mtu aliye juu ya jamii, ambaye anasahau ujenzi wa wema wa wote na kugawanya jamii. Katika muktadha huo, wamethubutu kuthibitisha, kwa kumtazama Yeye Aliyefufuka, kwamba wala utamaduni wa kifo, wala vurugu, wala uongo, wala uovu, hautakuwa na neno la mwisho”.
Tumaini la kuibua mzizi ya kiutamadui na kidini
Kulingana na maaskofu wa Mexico, tumaini hilo linaibuka kutoka katika mizizi ya kiutamaduni na kidini ambalo linawapatia utambulisho kama watu wa Mexico. Tumaini linawasukuma kuendelea kupigania amani, haki, uvumilivu, mshikamano na mazungumzo, katika kukabiliana na kile kinachotishia utu wa binadamu na tunu za familia, maisha, uhuru wa kujieleza, demokrasia, elimu na ukaribisho wa huruma, katika katikati ya vurugu, dhuluma na kutokujali ambayo imeenea na ambayo inaathiri zaidi masikini wote, wahamiaji, wanawake na watu wengi dhaifu. Kwa ajili hiyo maaskofu wa Mexico wamekusanyika katika mkutano huo wa kusikilizana. Walitaka kupyaisha jitihada zao za kujenga kwa ajili ya Pentekoste mpya ya kimisionari, iliyoainishwa katika Mkutano wa Aparecida mnamo (2007), ambao waliuanzisha tena katika kutaniko la Kikanisa la Amerika ya Kusini, lililofanyika Novemba mwaka jana 2021, na ambalo sasa wanajaribu kutambua kwa Kanisa lao katika Mexico, kupitia Mkutano wa Kikanisa. Kwa upendo huu kwa Kanisa, wanaunga mkono mchakato wa Sinodi kuelekea Roma mnamo 2023 iliyoitishwa na Papa Francisko. Akizungumza na waandishi wa habari, Askofu Mkuu Cabrera na Askofu Castro kwa upande mmoja ameonesha umuhimu wa kuweka mbele majadiliano na dhamana ya Kanisa katika jamii na kwa upande mwingine umuhimu wa kimkakati wa mpango wa kichungaji wa kimataifa unaoanza kupamba moto katika mkutano wa kwanza wa Kanisa.