Nyumba zimeharibiwa vibaya sana. Nyumba zimeharibiwa vibaya sana. 

Unicef/Ukraine:kila siku ya vita ni mateso makali kwa watoto

Kufungwa kwa shule kunaleta muktadha mkubwa wa elimu katika wakati ujao wa watoto milioni milioni 5,7 wenye umri wa kuanza shule na milioni 1,5 ya wanafunzi wa shule za sekondari.Ukraine Mashariki ilikuwa tayari ni moja ya ardhi ambayo ilikuwa imechafuliwa na mabomu ya kulipuka ulimwenguni hata kabla ya vita vinavyopendelea na sasa katika hali hii,mstakabali wao utakuwaje.Unicef inaripoti.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Inakadiliwa kuwa milioni 3,2 ya watoto ambao wamebaki katika nyumba zao na nusu yao kuna uwezekano wa kukabiliwa na tishio la kutokuwa na chakula cha kutosha. Kwa wiki sita karibu robo tatu ya watoto wote wa Ukraine wameondoka. Milioni 1,4 ya watu wasio kuwa na maji safi ya kunywa nchini Ukraine. Na milioni 4,6 ya watu hawana maji na chakula. Kufungwa kwa shule kunaleta muktadha mkubwa wa elimu katika wakati ujao wa watoto milioni milioni 5,7 wenye umri wa kuanza shule na milioni 1,5 ya wanafunzi wa shule za sekondari. Ukraine Mashariki ilikuwa tayari ni moja ya ardhi ambayo ilikuwa imechafuliwa na mabomu ya kulipuka ulimwenguni hata kabla ya vita vinavyopendelea na sasa katika hali hii, mstakabali wao utakuwaje.

"Kwa miaka 31 ya huduma yangu kibinadamu sijawahi kuona madhara kama haya kwa majuma machache"

Kwa mujibu wa uthibitisho wa Manuel Fontaine, Mkurugenzi wa Mipango ya UNICEF amebainisha kwamba amerudi wiki iliyopita kutoka nchini Ukraine lakini kwa miaka yake 31 tangu aanze huduma ya kibinadamu, hajawahi kuona madhara makubwa namna hiyo  yalivyo sasa  hivi kwa muda mfupi tangu kuanza kwa vita  Nchini Ukraine. Watoto, familia na jumuiya nyingi ziko chini ya shambulio. Hali halisi ni mbaya sana katika miji kama Mariupol na Kherson, mahali ambao watoto na familia zao zimebaki kwa majumba  yao kwa kujificha chini ya Majengo hayo bila kuwa na maji salama na huduma za usafi, ukosefu wa chakula cha kawaida na hata tiba  na madaktari. Hawa wanaishi chini ya majengo huku wakisubiri mabomu na vurugu viishe. Mnamo tarehe 10 Aprili 2022 Shirika la Umoja wa Mataifa la  kusaidia wakimbizi UNHCR lilikuwa limetoa taarifa kwamba watoto 142 waliuawa na 229 kujeruhiwa. Lakini idadi hiyo ni makadirio tu kwa sababu inawezekana kuwa kubwa zaidi hasa kusabishwa na moto au matumizi ya silaha za kulipuka katika maeneo ya makazi ya watu.

"Robo tatu ya watoto nchini ukraine wamekimbia"

Hata mifumo yote ambayo inasaidia watoto waweze kuishi, nayo iko chini ya shambulio. Fujo na ghasia hizi zimeleta madhara makubwa au kuharibu mamia ya nyumba za kuishi. Mashambulizi ya Hospitali, miundo mingi ya kiafya na vifaa vya tiba, pamoja na mauaji na watu wa kiafya, ni suala ambalo linazidisha ugumu mkubwa wa kuweza kutoa tiba za dharura msingi za kiafya na matibabu. Katika mkoa wa Donbas, kizazi kizima cha watoto kimeona maisha yao na elimu yao kukanganyikiwa wakati wa miaka 8 ya migogoro ya kivita. Kwa hakika kwa majuma sita, robo tatu ya watoto wa ukraine wamekimbia. Wamelazimika kuacha kila kitu nyumba zao, shule na mara nyingi hata kuacha familia zao nyuma. Watoto wengi wasiosindikizwa na ambao wako hatari ya virugu, nyanyaso za kijinsia, unyonyaji na biashara haramu ya binadamu na wawanake ambao pia wanakabiliwa hizo hizo. Kwa upande wa shirika la UNICEF wasi wasi mkubwa ni kutokana na taarifa zinazofikia kila siku kuhusiana na nyanyaso za kijinsia na aina nyingi sana na vurugu.

"Maisha na mustakabali yanategemea mamilioni ya watoto"

Aidha amesema “Nina wasiwasi sana juu ya kuenea kwa mabaki ya vita ambayo huweka watoto katika hatari ya kifo na majeraha ya kutisha. Mashariki mwa Ukraine tayari ilikuwa mojawapo ya maeneo yaliyochafuliwa na mabomu ya kulipuka zaidi duniani hata kabla ya kuongezeka kwa hivi karibuni. Ukweli huu unaenea kwa kasi katika maeneo mengine ya nchi. Wanafuatilia kwa karibu afya, haki na hadhi ya wanawake na wasichana huku hatari ya unyonyaji na unyanyasaji ikiongezeka”. Hata hivyo kwa upande wao wambainisha kwamba wataendelea kusisitiza haja ya kuhakikisha watoto ambao wametengwa na familia zao au wanaoishi katika taasisi wanalindwa na kwamba kila juhudi inafanywa ili kupata ridhaa ya wale wanaowalea na idhini ya mamlaka kabla ya watoto hawa wanaondolewa au kuhamishwa. Unicef inaomba kila mwenye uwezo wa kumaliza vita hivi aitumie. Maisha na mustakabali yanategemea mamilioni ya watoto. Kila siku vita vinavyoendelea ni siku moja zaidi ya mateso kwa watoto. Watoto wa Ukraine hawawezi kusubiri.

12 April 2022, 16:16