Mji wa Mariupol nchini Ufaransa umeharibiwa sana. Mji wa Mariupol nchini Ufaransa umeharibiwa sana. 

Wito wa UN kusitisha vita ili kunusuru raia wa Marioupol

Dominika tarehe 24 Aprili 2022 UN umerudia kutoa wito wa kusitisha mapigano mara moja ili kuruhusu raia wa wanaoripotiwa kukwama na kuzingirwa na machafuko katika mji wa Mariupol uliopo Kusini mwa Ukraine waweze kuhamishwa kwa usalama.Wakati huo huo naye kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Bi Bachelet amezitaka pande husika kuheshimu sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Dominika tarehe 24 Aprili 2022 Umoja wa Mataifa umerdia kutoa wito wa kusitisha mapigano mara moja ili kuruhusu raia wanaoripotiwa kukwama na kuzingirwa na machafuko katika mji wa Kusini mwa Ukraine wa Mariupol kuhamishwa kwa usalama. Kwa mujibu wa Amin Awad mratibu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mgogoro wa Ukraine amesema “Maisha ya makumi ya maelfu ya raia wakiwemo wanawake, watoto na wazee, yako hatarini huko Mariupol. Tunahitaji utulivu na usitwashi wa mapigano hivi sasa ili kuokoa maisha yao. Kadri tunavyongoja ndivyo maisha zaidi yatakavyokuwa hatarini. Ni lazima waruhusiwe kuondoka kwa usalama sasa na leo hii. Kesho inaweza kuwa tumechelewa sana. Hata hivyo ikumbukwe mpema mwezi huu, naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres alitoa wito wa kusitishwa mapigano kwa ajili ya kuingiza misaada ya kibinadamu wakati Wakristo wa Kiorthodox wanasherehekea sikukuu ya Pasaka, na wito ambao uliungwa mkono na Baba Mtakatifu Francisko, pamoja na Mabaraza ya Kanisa Katoliki na Kiinjili.

Katika siku ya Pasaka watu wa Mariupol  baada ya misa walipewa mikate
Katika siku ya Pasaka watu wa Mariupol baada ya misa walipewa mikate

Katika siku hiyo ya Pasaka, Bwana Awad alikumbusha na kusisitiza wito wa  Bwana Guterres wa kusitisha mapigano ili kuruhusu misaada ya kuokoa maisha kuingia ndani ya Mariupol na maeneo mengine yanayoshambuliwa na kuwezesha kuondoka kwa wale wanaotaka kuondoka huku kukiwa na ripoti za hali ya Mariupol kuwa mbaya zaidi.  “Wakati wa mpangilio adimu wa kalenda ya likizo za kidini za Pasaka ya Kiorthodox, Pasaka ya kawaida na mfungo wa Ramadhani, ni wakati wa kuzingatia ubinadamu wetu wa pamoja, kuweka migawanyiko pembeni  na kukumbatia upendo, alisema Bwana Awad.

Waamini wa Kiorthodox waliingia Kanisa kuadhimisha Misa ya Pasaka kwa hofu
Waamini wa Kiorthodox waliingia Kanisa kuadhimisha Misa ya Pasaka kwa hofu

Hatia hivyo uvamizi wa Urussi kwa  miezi miwili iliyopita umeitumbukiza Ukraine katika mzozo wa haki za binadamu na janga la kibinadamu ambalo limeharibu maisha ya raia  nchini kote na kwingineko. Alithibitisha  hayo  hayo tarehe 22 Aprili kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Bi Michelle Bachelet huku akizitaka pande zote husika katika mzozo huo kuheshimu sheria za kimataifa za haki za binadamu na hasa kanuni zinazosimamia masuala ya uhasama.  Bi. Bachelet alisema kwamba  katika wiki hizi nane za machafuko sheria za kimataifa za kibinadamu haijapuuzwa tu bali inaonekana zimetupiliwa mbali. Vikosi vya jeshi la Urussi vimeshambulia kwa makombora na kushambulia kwa mabomu maeneo yenye watu wengi, kuua raia na kuharibu hospitali, shule na miundombinu mingine ya kiraia, vitendo ambavyo vinaweza kuwa uhalifu wa kivita”.

Mariupol imegeuzwa kuwa majabali
Mariupol imegeuzwa kuwa majabali

Kwa kuongezea alisema “Tulichokishuhudia mjini Kramatorsk mji unaodhibitiwa na serikali hapo  tarehe 8 Aprili  wakati mabomu yalipopiga kituo cha reli, na kuua raia 60 na kuwajeruhi wengine 111, ni ishara ya kushindwa kuzingatia kanuni za kimataifa zinazokataza mashambulizi ya kiholela na kuzingatia kanuni ya tahadhari iliyowekwa katika sheria za kimataifa za kibinadamu.” Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kufuatilia Haki za Kibinadamu nchini Ukraine (HRMMU) pia umeandika kile kinachoonekana kuwa ni matumizi ya silaha zenye athari kiholela, na kusababisha vifo vya raia na uharibifu wa miundombinu wa kiraia, kutoka kwa vikosi vya jeshi vya Ukraine mashariki mwa nchi.  Tangu tarehe 24 Februari hadi usiku wa manane wa tarehe 20 Aprili, HRMMU imeandika na kuthibitisha raia 5,264 - 2,345 waliuawa na wengine 2,919 kujeruhiwa.   Kati ya hao, asilimia 92.3 sawa na watu (2,266 waliuawa na watu 2,593 kujeruhiwa) na wamerekodiwa katika eneo linalodhibitiwa na Serikali. 

Mariupol imegeuzwa kuwa majabali.Watu wanakula chakula nje
Mariupol imegeuzwa kuwa majabali.Watu wanakula chakula nje

Takriban asilimia 7.7 ya watu walioathirika (79 waliuawa na 326 kujeruhiwa) katika majimbo ya  Donetsk na Luhansk yanayodhibitiwa na vikosi vya kijeshi vya Urusi na vikundi vilivyojihami, imesema ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mastaifa OHCHR. Kufuatia na hizo ripoti Bi Bachelet amesema “Tunajua idadi halisi itakuwa kubwa zaidi idadi kamili itakapodhihirika kwani hali ya kutisha tunaishuhudia katika maeneo yenye mapigano makali, kama vile Mariupol. Kiwango cha mauaji ya raia katika maeneo ambayo hapo awali yalichukuliwa na vikosi vya Urusi pia kinaibuka. Kuhifadhi ushahidi na kuheshimu mabaki ya watu waliokufa lazima vihakikishwe, pamoja na msaada wa kisaikolojia na mwingine kwa waathiriwa na jamaa za waliopoteza maisha vihakikishwe.”  HRMMU pia imepokea taarifa kuhusu madai ya kuzuiliwa kiholela na bila mawasiliano na vikosi vya Ukraine au watu wanaoshirikiana navyo.  Katika baadhi ya matukio, jamaa hawana habari kuhusu wapi wapendwa wao waliko, na kuibua wasiwasi mkubwa kuhusu kutoweka kwa kulazimishwa, kufuata taratibu zinazofaa na hatari ya kuteswa na kutendewa ukatili.

Kwa maana hiyo “Kazi yetu hadi sasa ina historia ya kutisha ya ukiukwaji unaofanywa dhidi ya raia. Kwanza kabisa, vita hivi visivyo na maana lazima vikome. Lakini kwa vile mapigano hayaoneshi dalili ya kupungua, ni muhimu kwamba pande zote katika mzozo huo zitoe maelekezo ya wazi kwa wapiganaji wao kuheshimu kikamilifu sheria za kimataifa za kibinadamu na sheria za kimataifa za haki za binadamu,” amesisitiza Bi Bachelet.  Kwa kuongezea amesema kuwa: Hii inamaanisha kutofautisha kati ya vitu vya kiraia na vya kijeshi. Inamaanisha kutolenga au kuua raia kwa makusudi. Inamaanisha kutofanya ukatili wa kijinsia. Watu, pamoja na wafungwa wa vita, hawapaswi kuteswa. Raia, wafungwa na watu wengine katika vita lazima watendewe utu.

Mkuu wa Shirika hili  haki za Kibinadamu aliongeza kusema kuwa kuna ripoti za utesaji, unyanyasaji na mauaji yaliyofanywa na pande zote zinazopigana.  Kuna video nyingi zinazotolewa na pande zote mbili zinazopatikana mtandaoni zinazoonesha vitisho, kuhojiwa, kuteswa na hata mauaji ya wafungwa wa vita. Wale wanaoongoza vikosi vya kijeshi lazima waeleze wazi kwa wapiganaji wao kwamba yeyote atakayepatikana kuhusika katika ukiukaji huo atachukuliwa hatua na kuwajibishwa,” Bachelet alisema.  Kwa kuhihitimisha alisema “Ninatoa wito kwa pande zinazohusika katika mzozo kuchunguza ukiukaji wote wa sheria za kimataifa za haki za binadamu na sheria za kimataifa za kibinadamu yanayodaiwa kufanywa na raia wao, vikosi vya jeshi na vikundi shirikishi vyenye silaha, kulingana na majukumu yao chini ya sheria za kimataifa.

25 April 2022, 14:46