Siku ya Familia Kimataifa, ilianzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo 1994 na kuadhimishwa kila tarehe 15 Mei Siku ya Familia Kimataifa, ilianzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo 1994 na kuadhimishwa kila tarehe 15 Mei 

Siku ya Familia Kimataifa:tuisaidie&tuilinde ibaki na uzuri wake!

Kila tarehe 15 Mei ni Siku ya Kimataifa ya Familia iliyoanzishwa mnamo 1994.“Jitihada za kulinda tunu za thamani na unyeti wa uhusiano,ambao unasaidia kuishi wema na ambao unasaidia ubinadamu wote”,ndiyo msisitizo wa Papa Francisko katika ujumbe wake mfupi kwa njia ya mtandao katika siku hii ya kimataifa ya Familia.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya familia tarehe 15 Mei  Umoja wa Mataifa bado hata leo hii bado unataka kuhamasisha muundo wa familia ambao unabadilika ulimwenguni kufuatia mienendo ya kimataifa na mabadiliko ya demografia lakini bado Umoja huo unatambua familia kama kundi msingi katika jamii. Katika ujumbe mfupi wa Papa Francisko katika fursa ya siku hii, amebainisha kuwa:

Tusaidie familia, tuitetee kwa kile ambacho kinatoa ahadi ya uzuri. Tukaribie huduma hiyo ya upendo nyeti na huruma. Na jitihada za kulinda tunu za thamani na unyeti wa uhusiano, ambao unasaidia kuishi wema na unasaidia ubinadamu wote.

Familia kama msingi wa maendeleo na ustawi ndani ya kiungo na watoto

Siku ya Kimataifa ya Familia ilianza mnamo 1994 na imekuwa ikifafanuliwa kama kikundi msingi sana na mazingira asili kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa wajumbe wake, kwa namna ya pekee watoto. Familia ni mahali pa kutunza, kulinda na kusaidiana. Kulea watoto katika misingi ya kawaida na asili katika jamii na kuhakikisha uwepo wa huduma bila ubaguzi. Lakini licha ya hayo Familia ya kisasa inakabiliana na matatizo makubwa mno. Athari kubwa inayopatikana kwa watoto baada ya familia kuvunjika ni wao kukosa mahusiano na mmoja au wazazi wote. Kwa mfano, wazazi wanapotengana, watoto mara nyingi hukulia ndani ya familia ya “mzazi mmoja” ambapo mara nyingi zimepelekea kupunguza au kupoteza mawasiliano na mmoja wa wazazi.

Ngazi za mahusiano kuanzia na wazazi na kati ya watoto

Kama jamii tunahitaji kufahamu kwamba katika mahusiano mengi tofauti tofauti ambayo watu huwa nayo kwa muda wa maisha yao, mahusiano kati ya mzazi na mtoto ni moja miongoni mwa ambayo ni muhimu. Namna wazazi wanavyotendeana na wanavyowatendea watoto wao, itakuwa ni kiashiria kikubwa cha namna watakavyokuwa ukubwani na  jinis watavyoweza kucheza katika jamii. Huku mahusiano kati ya mzazi na mtoto yanapozidi kudorora kutokana na hali ya familia, tunaona kwamba watoto kutoka katika familia zilizovunjika wanapoteza kwa ujumla hisia ya kustahiki kuwa sehemu fulani. Hisia hii inamaanisha kujihisi kukubalika na kuthaminiwa kama mwanachama au sehemu ya kitu. Ni fikra muhimu tunayohitaji kuihisi ili tuweze kuyaendea masuala yanayotuzunguka na kupambana na mazito maishani mwetu. Wajuzi wamependekeza kuwa fikra hii muhimu inakosekana ndani ya vijana wengi kutoka katika majumba yaliyovunjika na ndiyo kigezo kikubwa kinachopelekea vijana kuingia katika magenge ya kila aina. Inaweza kuwa sababu ya kwa nini tunaona ongezeko la uhalifu wa magenge. Vijana wengi wanaona kuwa uanachama katika magenge ni kama mbadala wa familia na yanayowapatia hisia hiyo ya kustahiki kuwepo sehemu fulani. Siku ya familia ni muhimu sana.

Maana ya majukumu ya familia katika maandiko matakatifu

Katika masuala ya familia tunaweza kupata maaana kamili kutoka katika maandiko matakatifu hasa kuhusu wajibu na majukumu ya mke na mme katika familia. Ingawa wanaume na wanawake wako sawa katika uhusiano na Kristo, maandiko yanatoa majukumu maalum kwa kila mmoja katika ndoa. Mume anapaswa kuchukua uongozi katika (1 Wakorintho 11:3, Waefeso 5:23). Uongozi huu usiwe wa kihimla, kukandamisa, au shupavu kwa mke, lakini lazima iwe kwa mujibu wa mfano wa Kristo kuongoza Kanisa. "Enyi wanaume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neon" (Waefeso 5:25-26). Kristo alivyolipenda Kanisa la watu wake na huruma,, msamaha, heshima, na kutokuwa na ubinafsi. Kwa njia hiyo waume wanapaswa kuwapenda wake zao.

Unyenyevu na mamlaka

Wanawake wanapaswa kunyenyekea kwa mamlaka ya waume zao. "Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa, naye ni mwokozi wa mwili wake. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo" (Waefeso 5:22-24). Ingawa wanawake wanapaswa kunyenyekea kwa waume zao, Biblia pia inawaambia wanaume mara kadhaa jinsi wanavyo takiwa kuwafanyia wake zao. Mume hapaswi kuchukua nafasi ya kiihimla, kama kumiliki mali, lakini wanapaswa kuoneesha heshima na upendo kwa mke wake na maoni yake, kwa namna nyingine kuhehimiana.

Upendo sawa kati ya mme na mke: kuheshimiana na kufuata kanuni

Kiukweli, Mtakatifu Paulo mtume wa Watu katika wataka wa Waefeso 5:28-29 anawahimiza watu kuwapenda wake zao katika njia sawa wanavyoipenda miili yao wenyewe, kuwalisha na kuwatunza. Upendo wa mume kwa mke wake unapaswa kuwa sawa na upendo wa Kristo kwa mwili wake, Kanisa. Cha kushangaza, upendo huo umegeuka kuwa miliki, wivu chuki uhasama, na zaidi katika nchi za magharibu, upendo kwa wana ndoa umeleta mkanayiko mkubwa, lakini kwa ujumla inabidi kurudi tena katika msingi wa nini maana ya familia na majukumu yake ndani ya kiungo cha familia na katika jamii yote.

 

15 May 2022, 10:10