Madhambulizi bado yanaendelea huko, mkoa wa Donetsk na watoto wanapata shida katika kusaka mkate wa kula. Madhambulizi bado yanaendelea huko, mkoa wa Donetsk na watoto wanapata shida katika kusaka mkate wa kula. 

UNICEF:Kufikia mwishoni mwa 2021 mizozo,ghasia na migogoro imesababisha watoto milioni 36.5 kuhama!

Watoto milioni 36.5 wamehama makwao kufikia mwisho wa 2021,kutokana na vurugu na migogoro na ni idadi kubwa zaidi iliyorekodiwa tangu Vita vya Kidunia vya pili.Idadi hii inajumuisha wakimbizi na watoto milioni 13.7 wanaotafuta hifadhi na karibu watoto milioni 22.8 waliokimbia makazi yao kutokana na migogoro na ghasia.Takwimu hizi hazijumuishi watoto waliokimbia makazi yao kutokana na athari za tabianchi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kulingana na makadirio ya UNICEF, mizozo, ghasia na migogoro zaidi ilisababisha watoto milioni 36.5 kuhama makwao kufikia mwisho wa 2021, idadi kubwa zaidi iliyorekodiwa tangu Vita vya Kidunia vya pili. Idadi hii inajumuisha wakimbizi na watoto milioni 13.7 wanaotafuta hifadhi na karibu watoto milioni 22.8 waliokimbia makazi yao kutokana na migogoro na ghasia. Takwimu hizi hazijumuishi watoto waliokimbia makazi yao kutokana na athari za hali ya hewa na mazingira au majanga, wala wale waliokimbia makazi yao hivi majuzi mwaka wa 2022, ikiwa ni pamoja na kutokana na vita nchini Ukraine. Kiasi kikubwa cha idadi ya watoto waliokimbia makazi yao ni matokeo ya moja kwa moja ya misururu ya migogoro, ikijumuisha migogoro mikali na ya muda mrefu kama ile ya Afghanistan, hali tete katika nchi kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC au Yemen, na majanga yanayohusiana na hayo yanayozidishwa na athari za mabadiliko ya hali tabianchi: kama vile udhaifu, uhamishaji wa watoto pia unaenea kwa kasi. Mwaka 2021, idadi ya watoto waliokimbia makazi duniani iliongezeka kwa milioni 2.2.

Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF Catherine Russell akizungumza kuhusia na hili alisema  “Hatuwezi kupuuza ushahidi: idadi ya watoto waliokimbia makazi yao kutokana na migogoro na migogoro inaongezeka kwa kasi, kama vile jukumu letu kuwafikia. Ninatumaini idadi hii ya kutisha itachochea serikali kwanza kuzuia watoto wasihamishwe  na wanapohamishwa, kuwapa fursa ya kupata elimu, ulinzi na huduma zingine muhimu zinazosaidia ustawi na maendeleo yao sasa na katika siku zijazo.”

Kinachoongeza  katika idaidi hiyo  ni migogoro kama vile vita vya Ukraine, ambavyo tangu Februari mwaka huu tayari vimesababisha zaidi ya watoto milioni 2 kukimbia nchi na wakimbizi wa ndani milioni 3. Zaidi ya hayo, watoto na familia pia wanafukuzwa kutoka kutoka nyumba zao kutokana na hali mbaya ya tabianchi, kama vile ukame katika Pembe ya Afrika na Sahel na mafuriko makubwa huko Bangladesh, India na Afrika Kusini. Mnamo 2021, kulikuwa na visa vipya milioni 7.3 vya kuhama kwa watoto kutokana na majanga ya asili. Idadi ya wakimbizi duniani imeongezeka zaidi ya mara mbili katika muongo mmoja uliopita na watoto ni karibu nusu ya jumla ya wakimbizi hao. Zaidi ya theluthi moja ya watoto waliokimbia makazi yao wanaishi Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara (milioni 3.9 au 36%), robo Ulaya na Asia ya Kati (milioni 2.6 au 25%) na 13% (milioni 1.4) Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.

Kadiri idadi ya watoto waliohamishwa na wakimbizi inavyofikia idadi ya juu, upatikanaji wa huduma muhimu kama vile huduma za afya, elimu na ulinzi unapungua. Takriban theluthi mbili ya watoto wote wakimbizi wameandikishwa katika shule ya msingi, huku takriban kijana mmoja kati ya watatu kati ya vijana mkimbizi wakihudhuria shule ya sekondari. Watoto wahamiaji, wawe wakimbizi, wanaotafuta hifadhi au watu waliokimbia makazi yao, kiukweli wanaweza kupata hatari kubwa kwa ustawi na usalama wao. Hii ni kweli hasa kwa mamia ya maelfu ya watoto ambao hawajasindikizwa au waliotenganishwa ambao wako katika hatari kubwa ya ulanguzi, unyonyaji, vurugu na unyanyasaji. Watoto wanawakilisha takriban 34% ya waathiriwa waliosajiliwa wa biashara mbaya ya binadamu duniani kote. UNICEF inazitaka nchi wanachama kuheshimu ahadi zao kwa haki za watoto wote wahamiaji, ikiwa ni pamoja na zile zilizowekwa chini ya Mkataba wa Kimataifa wa Wakimbizi (GCR) na Mkataba wa Kimataifa wa Uhamiaji (GCM), na kuwekeza zaidi katika data na utafiti unaoakisi ukubwa halisi wa matatizo yanayowakabili wakimbizi, wahamiaji na watoto waliokimbia makazi yao.

17 June 2022, 18:15