Dharura nchini Pakistan:mafuriko yasababisha zaidi ya vifo elfu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ni mafuriko ya uharibifu ambayo haijawahi kutokea katika miaka 30 iliyopita na ndiyo hali halisi iliyoelezwa na Waziri Mkuu Shehbaz Sharif, kwamba iliyoachwa nchini Pakistan na mvua za masika, ambazo hazikuwahi kuonekana zinanyesha muda mrefu kwa mwezi Julai. Kwa mujibu Padre Piero Ramello, Msalesia kutoka Lahore, aliyepushwa hatari hiyo wakati wa maporomoko ya maji amebainisha jinsi hali ilivykuwa ya hatari. Nyumba, bidhaa, riziki zimepotea kwa wengi, zimezama kama vile baharini. Takriban majimbo yote ya Baluchistan na Sindh, ambayo ni majimbo mawili yaliyoathiriwa zaidi, KPK na Punjab kusini, yanakabiliwa na mgogoro ambao haujawahi kushuhudiwa, na ambao serikali imeomba msaada wa haraka kutoka kwa jumuiya ya kimataifa. Familia nyingi zinahitaji chakula, malazi na huduma za afya na baada ya kupoteza wanyama na mifugo mingi, ambayo ni sehemu ya maisha yao ya kila siku, ugumu ni mkubwa, amefafanua Padre Ramello.
Hata hivyo naye Papa Francisko alikumbusha mshikamano wa ukarimu kwa jumuiya ya kimataifa, sawa na Waziri Mkuu Sharif wa nchi hiyo alivyokuwa ameomba. Majanga ya asili na vita vinavyo sababisha maelfu ya waathiriwa na mamilioni ya watu waliokimbia makazi yao lilikuwa wazo la Papa Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika 28 Agosti 2022 iliyomkuta katika ziara huko Aquila katika tukio la msamaha wa Selestina. Kwa maana hiyo alitoa wito wa nguvu kwa viongozi wa mataifa ili wawe na huruma na ukarimu wa mioyoni mwao. Baada ya kuwashukuru waliosimamia ziara yake hiyo ya kina, Kanisa, mashirika ya kiraia, Mawazo ya Papaalisema: "kwa hakika matokeo mabaya ya miezi mitatu ya mvua za monsuni nchini Pakistan, ambapo kuna dharura ya kitaifa na karibu vifo elfu, watu milioni 33, waliohamishwa na hatari ya mlipuko wa kipindupindu. Papa Francisko kwa maana hiyo alionesha ukaribu wake na kuinua sala yake na kusema: “Katika eneo hili ambalo limekumbwa na janga kubwa, ninataka kuwahakikishia ukaribu wangu watu wa Pakistan walioathiriwa na mafuriko ya viwango vya maafa. Ninawaombea wahanga wengi, waliojeruhiwa na waliokimbia makazi yao, na mshikamano wa kimataifa uwe tayari na ukarimu”.
Wakati huo huo, fedha zinazotolewa na serikali zinaonekana kutotosha kabisa. Tatizo kuu amesema Padre Ramello zaidi ya hali ya hali ya tabianchi ambayo kutokana na ongezeko la joto duniani inaonekana kuelemea sana Pakistan hasa ni kutokuwepo kwa mfumo wa utupaji taka au ukusanyaji, ambao watu nchini kote hutupa takataka hovyo kwenye mito. Wakati maji yanapokuwa mengi na yasiyozuilika, taka hutengeneza vizuizi vya kweli, kuzuia mtiririko wa kawaida na kuchochea mafuriko na mafuriko ya idadi kubwa. Mipango duni ya miji pia imesababisha ujenzi wa maelfu ya majengo katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko. Zidi ya hayo, kuna ongezeko la joto duniani: Maafisa wa Pakistani wanalaumu mabadiliko ya tabianchi wakisema Pakistan inakabiliwa na matokeo ya mazoea ya kutowajibika ya mazingira katika maeneo mengine ya dunia. Itakuwa nchi ya nane kutishiwa zaidi na hali mbaya ya hewa, kulingana na utafiti wa Shirila lisilo la Kiselikalo la Germanwatch.
Dalili za maafa hayo ni katika Mto Indus, unaopita katika jimbo la kusini la Sindh, ukiwa umejazwa na makumi ya mito na vijito vya milimani ambavyo vimevunja kingo zake kwa sababu ya mvua kubwa na barafu kuyeyuka. Malango hayo yamefunguliwa ili kukabiliana na mtiririko wa zaidi ya mita za ujazo 600,000 kwa sekunde, alisema mkuu wa bwawa kuu linalodhibiti mtiririko wa mto huo karibu na mji wa Sukkur, mkoani Sindh, ambako takriban watu 500,000 wanaishi. Mamlaka imeonya kwamba mito ya maji inatarajiwa kufika jimbo la Sindh katika siku zijazo, na kuongeza ugumu wa mamilioni ya watu ambao tayari wameathiriwa na mafuriko. Kwa hivyo, maafa makubwa ambayo nchi iko katika hali ya hatari katika wakati mgumu tayari kutokana na kuporomoka kwa uchumi na mzozo mkubwa wa kisiasa baada ya kuondolewa kwa Waziri Mkuu Imran Khan, ambayo ilifanyika mnamo Aprili mwaka huu kufuatia kura ya kutokuwa na imani na Bunge.