Mkutano wa Papa Yohane Paulo II na Rais wa Kisovietiki Michail Gorbachev  mnamo tarehe Mosi Desemba 1989. Mkutano wa Papa Yohane Paulo II na Rais wa Kisovietiki Michail Gorbachev mnamo tarehe Mosi Desemba 1989.  

Rais Mickhail Gorbachev,aliyekuwa mtu wa mageuzi ameaga dunia

Aliyekuwa rais wa mwisho wa Umoja wa Kisovieti,mhusika mkuu wa perestroika na glasnost,mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 91 na alikuwa mgonjwa sana.Mnamo 1989 alifanya mkutano wa kihistoria na Papa Yohane Paulo II.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kiongozi wa mwisho wa Umoja wa Kisovieti ameaga dunia usiku wa kuamkia Jumatano tarehe 31 Agosti, akiwa na umri wa miaka 91, katika Hospitali Kuu ya Kliniki huko Moscow, Urusi ambapo alilazwa hospitalini kwa ugonjwa wa muda mrefu. Mikhail Gorbachev alizaliwa mnamo 1931, na alikuwa mmoja wa wahusika wakuu wa mwisho wa karne ya ishirini kwa kuanzisha tena uhusiano na nchi za Magharibi na kujitoa kupunguza silaha za nyuklia na kwa ajili ya mageuzi yaliyofanywa ndani ya USSR ambayo yalisababisha kuanguka kwa ukomunisiti wa kisovietiki na mwisho wa vita baridi.

 Rais  Michail Gorbachev na Rais wa Marekani
Rais Michail Gorbachev na Rais wa Marekani

‘Perestrojka’ na ‘Glasnost’ yalikuwa maneno ya mwongozo wa hatua yake ya mageuzi. Ya kwanza, ‘urekebishaji’, ilimaanisha mageuzi ya kiuchumi, ambayo yalikusudia ufunguzi wa awali wa uchumi wa soko baada ya miongo kadhaa ya takwimu. Ya pili, ‘uwazi’, ilikusudiwa kutoa mwanga juu ya siku za nyuma, mara nyingi kufichwa na propaganda, na kufungua mfumo kwa habari huru. Asili ya  kutoka Caucasus Kaskazini, Bwana Gorbachev alisomea sheria na aliteuliwa kuwa kiongozi wa chama cha mkoa wake akiwa na umri wa miaka 39. Mnamo 1978 alikuwa huko Moscow kama katibu wa Kamati Kuu ya chama, na mnamo 1985 alikuwa katibu mkuu baada ya Černenko, mnamo 1990 alichaguliwa kuwa rais wa USSR.

 Rais  Michail Gorbachev
Rais Michail Gorbachev

Mkutano ambao hautasaulika ulikuwa ule na Papa Yohane Paulo II jijini Vatican mnamo tarehe 1 Desemba 1989. Rais wa Kisovietiki na Papa wa Poland walipopeana mkono, picha ilienea ulimwenguni kote katika muktadha wa kihistoria usiofikirika kwa kusema kwamba  Gorbachev karibu na Yohane  Paulo II huku tawala za kikomunisti zikiporomoka katika Ulaya Mashariki. Mnamo 1990 alipokea Tuzo ya Amani ya Nobel  kwa ajili ya jukumu lake kuu katika mabadiliko makubwa katika uhusiano kati ya Mashariki na Magharibi. Baadaye  mnamo Agosti 1991, alinusurika kupinduliwa na kufungwa kwa siku tatu katika jumba la rais kwenye Bahari Nyeusi: mnamo Desemba mwaka huo huo, Muungano wa Sovieti ulianguka.

 Rais  Michail Gorbachev na Papa Yohane Paulo II mnamo 1989
Rais Michail Gorbachev na Papa Yohane Paulo II mnamo 1989
 Rais  Michail Gorbachev na Papa Yohane Paulo II mnamo 1989
Rais Michail Gorbachev na Papa Yohane Paulo II mnamo 1989

Gorbaciov, “alikuwa kiongozi adimu, mwenye mtazamo wa ajabu aliyeifanya dunia kuwa salama”, ndiyo  maoni yake Rais wa Marekani Bwana  Joe Biden, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Bwana Antonio Guterres akimkumbuka kuwa “mwanasiasa wa kipekee ambaye amebadilisha mkondo wa historia. Ulimwengu, umempoteza kiongozi wa kimataifa na mfuasi asiyechoka wa amani”, ameisitiza. Na kwa upande wa Rais wa Tume ya Ulaya Ursula Von der Leyen katika maneno yake amesema “Alifungua njia kwa Ulaya huru”.

Kifo cha Rais Gorbachev
31 August 2022, 14:03