Vitendo vya kigaidi nchini Msumbiji visesababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Vitendo vya kigaidi nchini Msumbiji visesababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. 

Madhara ya Vitendo Vya Kigaidi Nchini Msumbiji: Utu, Heshima na Umoja wa Kitaifa

Takwimu zinaonesha kwamba, kuanzia tarehe 1 Juni hadi 21 Julai 2022 kuna mashambulizi 90 ya kigaidi yametokea. Idadi ya watu wanaokimbia vita ili kusalimisha maisha yao imeongezeka maradufu hadi kufikia watu 946, 508, ikiwa ni ongnezeko la watu 161, 944 hadi kufikia Mwezi Februari 2022. IOM linabainisha kwamba, wahamiaji 138, 231 waliweza kurejea tena nyumbani kwao.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Vitendo vya kigaidi ni ukweli ambao unaendelea kusababisha madhara makubwa kwa watu na mali zao, kiasi hata cha watu kukosa amani na utulivu mambo msingi katika mchakato wa maendeleo fungamani ya binadamu. Vitendo hivi vimeharibu urithi mkubwa wa utamaduni, utambulisho wa watu pamoja na historia yao. Hadi sasa Jumuiya ya Kimataifa imeshindwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti vitendo vya kigaidi vinavyoendelea kujitokeza sehemu mbalimbali za dunia, hususan huko Mashariki ya Kati na katika baadhi ya nchi za Kiafrika. Masuala ya wapiganaji mamluki, ushawishi wa vijana kutumbukia kwenye vitendo vya kigaidi na kitendo cha vijana hao kuona wameenguliwa kwenye masuala yanayowahusu ni kati ya mambo yanayowasukuma vijana kujitumbukiza katika vitendo vya kigaidi, hasa pale wanapohisi kwamba, wamepuuzwa. Umoja wa Mataifa unasema, ni jambo la kusikitisha kuwa wasajiliwa wapya kwenye vikundi vya kigaidi wana umri wa kati ya miaka 17 hadi 27. Vikundi vya kigaidi vinatumia ile dhana inayofanya vijana wa kike na wa kiume wajione wa kipekee, tofauti na maadili ya kijamii. 

Wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji kutoka Msumbiji ni kosa las kigaidi
Wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji kutoka Msumbiji ni kosa las kigaidi

Magaidi wanaangalia shida za vijana na ndio maana ni lazima jamii ijitahidi kushughulikia masuala ya vijana. Kuna haja kwa Jumuiya ya Kimataifa kujielekeza zaidi katika mchakato wa kuzuia vitendo vya kigaidi, kwa kutafuta ufumbuzi wa visababishi vya watu kuvutiwa na vitendo hivi viovu vinavyo nyanyasa utu, heshima na haki msingi za binadamu. Ni katika muktadha wa mapambano dhidi ya vitendo vya kigaidi, vyombo vya ulinzi na usalama nchini Msumbuji kwa kushirikiana na Vikosi vya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC vimefanikiwa kuwaokoa mateka wa vitendo vya kigaidi 600 kutoka Jimbo la Cabo Delgado, Kaskazini mwa Msumbiji. Takwimu zinaonesha kwamba, kuanzia tarehe 1 Juni hadi kufikia tarehe 21 Julai 2022 kuna mashambulizi 90 ya kigaidi yametokea na hivyo kusababisha watu wengi kuyakimbia makazi yao. Idadi ya watu wanaokimbia vita ili kusalimisha maisha yao imeongezeka maradufu hadi kufikia watu 946, 508, ikiwa ni ongnezeko la watu 161, 944 hadi kufikia Mwezi Februari 2022. Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) linabainisha kwamba, wahamiaji 138, 231 waliweza kurejea tena nyumbani kwao. Wachunguzi wa mambo wanasema kwamba, vitendo vya kigaidi Kusini mwa Afrika vinaendeshwa kwa kiasi kikubwa na wapiganaji wa Dola ya Kiislam, Is.

Msumbiji

 

 

08 August 2022, 16:37