1661703250839.jpg

Bi Amina Mohammed kwa TICAD8:Afrika ni bara tajiri na sio tegemezi!

Leo,takriban watu milioni 600 barani Afrika wanakabiliwa na uhaba wa umeme.Hii ina maana bara litahitaji taratibu za maendeleo ya vyanzo vya nishati rafiki kwa mazingira.Kupanda kwa sasa kwa bei ya nishati kunaweza pia kuhimiza nchi za Afrika kutumia vyema uwezo mkubwa wa nishati mbadala wa bara hilo.Lakini hii inahitaji uwekezaji mkubwa na wa wakati.Alisema hayo Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Mkutano wa VIII wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo Afrika.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Mkutano wa VIII wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika  (TICAD) uliofanyika siku mbili ya  27-28 Agosti huko jijini  Tunisi, nchini Tunisia uliwaona washiriki zaidi ya elfu tano ambapo miongoni  mwao, wakuu wa Nchi 30 na wa serikali kutoka Afrika Nzima. Mada zilizokuwa kiini cha majadiliano ni kuhusu usalama wa vyakula, afya, mpito wa nishati na mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo uchumi wa kijani. Kwa maana hiyo Bara la Afrika ni tajiri na sio tu kwa maliasili yake,  lakini pia kwa idadi yake ya vijana wenye nguvu. Hivyo Jumuiya ya Kimataifa haina budi kubadili sura ya Afrika na mtazamo kwamba  bara hilo ni tegemezi na kuzisaidia nchi za eneo hilo katika maendeleo ya mifumo ya kisasa ya nishati na chakula.  Hayo yalisemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed, wakati akizungumza nchini Tunisia kwenye Mkutano huo.

Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika (TCAD) 27-28 Agosti 2022
Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika (TCAD) 27-28 Agosti 2022

Bi Amina Mohamed amesisitiza kuwa, nchi za Afrika zina viashiria vyote vinavyohitajika kwa ajili ya maendeleo endelevu, na ushirikiano wao katika uchumi wa dunia ambao utafanya uwezekano wa kuondokana na vikwazo vingi vya sasa.   Mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa kwa upande wake anaamini kuwa jumuiya ya kimataifa inadharau uwezo wa bara hilo. Ikumbukwe kwamba zaidi ya watu bilioni 1.2 wanaishi barani Afrika. Takriban asilimia 60 ya wakazi wa Afrika wana umri wa chini ya miaka 35. Ukuaji wa haraka wa miji katika nchi za Afrika unaahidi fursa mpya, ikiwa ni pamoja na katika uwanja wa maendeleo ya viwanda kwenye bara hilo.  Bi Amina Mohammed kwa maana hiyo ametaja hati mbili kama ramani ya njia  kwa ajili ya maendeleo endelevu ya bara hilo ambazo ni malengo ya maendeleo endelevu na ajenda ya 2063 ya Afrika.  Bi. Mohammed amesisitiza kuwa ili kufanikiwa kufikia malengo ya ajenda hizo mbili jumuiya ya kimataifa lazima ishirikiane kuondoa athari za migogoro mingi.

Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika (TCAD) 27-28 Agosti 2022
Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika (TCAD) 27-28 Agosti 2022

"Kujikwamua kutoka katika janga la UVIKO-19, matokeo ya vita nchini Ukraine, dharura ya hali ya mabadiliko ya tabianchi na shida ya kifedha inaweka idadi ya watu walio hatarini zaidi kwenye mtihani”, alisema Bi Amina. Kwa kusisitiza zaidi aliongeza kusema kuwa  mchanganyiko huo unaolipuka hutengeneza mazingira yenye rutuba ya kuzidisha migogoro iliyopo na ya siku zijazo na huzaa machafuko, ambayo yanadhoofisha juhudi za pamoja za kufikia malengo ya maendeleo endelevu (SDGs). Amina Mohammed amekumbusha kuwa eneo la biashara huria la Afrika, linachangia ukuaji wa viwanda, mchanganyiko na uchumi wa kidijitali wa nchi za kanda hiyo, na pia husaidia kuimarisha ushirikiano wa kikanda.  Na kuongeza kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa ili kufanyia kazi mambo matatu ambayo yatanufaisha uchumi wa Afrika na kusaidia kufikia malengo ya maendeleo endelevu. Kwanza,  kabisa alivyosema, ni muhimu kuhakikisha upatikanaji wa vyanzo vya nishati kwa wote na mabadiliko ya haki na ya usawa kwa vyanzo vya nishati mbadala.   Katika muktadha huo, Bi. Amina Mohammed alitoa wito wa kuwepo kwa mbinu jumuishi ili kuongoza maendeleo ya nishati barani Afrika, kwa kuzingatia uwekezaji endelevu na ushirikiano imara.

Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika (TCAD) 27-28 Agosti 2022
Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika (TCAD) 27-28 Agosti 2022

Bi Amina alisema: “Leo, takriban watu milioni 600 barani Afrika wanakabiliwa na uhaba wa umeme. Na hii ina maana kwamba bara litahitaji taratibu za maendeleo ya vyanzo vya nishati rafiki kwa mazingira. Kupanda kwa sasa kwa bei ya nishati kunaweza pia kuhimiza nchi za Afrika kutumia vyema uwezo mkubwa wa nishati mbadala wa bara hilo. Lakini hii inahitaji uwekezaji mkubwa na wa wakati.”  Pili,  alisema “Afrika inahitaji mabadiliko ya haraka ya mifumo yake ya chakula” na hivyo aksisitiza mwakilisho huyo wa umoja wa Mataifa kwamba “ili Afrika iwe kikapu halisi cha mkate, ni muhimu kufikia ongezeko la uzalishaji katika kilimo na mifumo ya chakula, kutumia teknolojia mpya na mifumo ya kisasa ya umwagiliaji, kufikia kilimo cha ufundi na kupunguza hasara baada ya mavuno”. Tatu, hatimaye matatizo ya Afrika, yanayosababishwa na migogoro inayoingiliana, hayatatatuliwa bila kushughulikia ukosefu wa usawa. Kwa kuhitimisha aliongeza kusema kuwa "Ni muhimu kubadili mtazamo wa Afrika kama bara tegemezi, na kuifanya kuwa mhusika mkuu katika hatua ya dunia, yenye haki na nafasi sawa, iwe ya kiuchumi au kisiasa, kama ukanda mwingine wowote”.

Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika (TCAD) 27-28 Agosti 2022
Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika (TCAD) 27-28 Agosti 2022

Mkutano huo  VII wa Kimataifa wa Tokyo  kwa ajili ya Afrika ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa, Banki Kuu na Umoja wa Afrika(UA), ulikuwa na lengo maalum ya kujadili jinsi ya kuunda pamoja ulimwengu endelevu katika muktadha mgumu wa janga la UVIKO-19 na hali halisi ya Ukraine. Nchi ya Tunisia iliyokuwa imekaribisha Mkutano huo, ilitazamia kuvutia uwekezaji hasa katika afya, kiwanda, anga katika katika ubunifu wa nishati kwa zaidi ya mipango 80 iliyowekwa mezani kwa thamani ya dola bilioni 2.7, kulingana na rais wa Chama cha Wafanyabiashara cha Tunisia-Japani. Kwa uwezo wake wa kiviwanda, alisema Tunisia inalenga kuwa mdau mkuu katika uzalishaji wa dawa na chanjo.

Na katika Hotuba ya Rais wa Kundi la Benki ya Dunia katika ufunguzi wa Mkutano huo wa VIII wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD 8), alisema kwamba Kundi la Benki ya Dunia linasalia kuwa mshirika aliyejitolea kwa muda mrefu kwa ajili ya Afrika. “Takriban nusu ya fedha zetu za IBRD na IDA zinakwenda bala la Afrika. Biashara ni njia yenye nguvu ya kujenga uchumi thabiti, kupunguza umaskini na kukuza ustawi. Ndani ya Kundi la Benki ya Dunia, tunashauri serikali kuhusu sera muhimu za kibiashara. Tunasaidia nchi za Kiafrika kutoa ulinzi wa kijamii unaolengwa na muhimu kwa walio hatarini zaidi” alisema Rais huyo. "Mpango wa Kukabiliana na Dharura wa Ulinzi wa Jamii wa UVIKO-19 kwa nchi ya Tunisia alieleza kuwa “unasaidia kulinda wanajamii walio hatarini zaidi". Aidha alisitiza kuwa "Nchini Malawi, tunafanya kazi na serikali kuboresha ulengaji wa mpango wao wa ruzuku ya mbolea. Sehemu kubwa ya kazi zetu barani Afrika inasaidiwa na IDA, mfuko wetu wa watu maskini zaidi duniani. IDA inasaidia sekta ya umma na binafsi. IFC na MIGA zinasaidia umati katika uwekezaji wa kibinafsi”.

MKUTANO KUHUSU AFRIKA:HOTUBA YA BI AMINIA NAIBU KATIBU MKUU WA UN
29 August 2022, 13:15