Kazakhstan na msimamo wa kisiasa katika makutano ya makabila na dini nyingi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Nchi ya Kazakhistano iliyowekwa kati ya Urusi, na ambayo inapakana nayo kwa sehemu nzima ya kaskazini, China upande wa mashariki, jamhuri za zamani za Kisovieti katika sehemu ya kusini (Kyrgyzstan, Uzbekistan, Turkmenistan) na ziwa kubwa la Bahari ya Caspian kuelekea magharibi, na hivyo Kazakhstan ni kubwa, kama vile Ulaya Magharibi yote. Jina lake linamaanisha “Nchi ya Cossacks” na inaonesha wahamaji, ambao waliishi nyika za Asia ya Kati.
Milinganisho ya kijiografia na kisiasa
Kazakhstan ilikuwa sehemu ya Milki ya Urusi na baadaye ya USSR hadi mnamo 1991. Miaka ya 1990 ilishuhudia mkusanyiko unaoendelea wa madaraka mikononi mwa Rais Nursultan Nazarbayev, ofisa wa serikali ya zamani ya Kisovieti, ambaye alibaki kwenye usukani wa nchi hadi mnamo 2019 wakati aliweza kukabidhi mamlaka kwa Kassym-Jomart K. Tokayev. Ikiwa, katika ngazi ya ndani, Nazarbayev alikuwa ameendesha sera ya kimabavu, katika ngazi ya kimataifa alikuwa amefuata sera ya pande nyingi yenye lengo la kujenga na kudumisha uhusiano mzuri na nchi jirani, hasa mamlaka ya Kirusi na China, na Iran, Uturuki, lakini pia Umoja wa Ulaya na Marekani.
Ushirikiano huo umekuwa ukiunganishwa na nchi ya Uchina iliyo karibu, kiasi kwamba katika siku za Kongamano la viongozi wa dini za ulimwengu na za jadi (14-15 Septemba), Rais Ji-Xinping yuko katika ziara ya kiserikali katika mji mkuu. Matukio ambayo yamejitokeza katika miezi ya hivi karibuni kutokana na vita vya Ukraine yanaathiri muundo wa ndani na hivyo Tokayev anaonekana kuwa na nia mpya ya uhusiano na mshirika huyo mwenye wa nguvu wa Urusi kama ulivyooneshwa na msimamo wake katika Mkutano wa Kiuchumi wa Kimataifa wa wa Mtakatifu Pietroburgo 2022 mnamo Juni ambapo alisema kuwa nchi yake haitambui maeneo ya kujitenga ya Urusi yanayokaliwa na wanajeshi wa Moscow.
Mwamko wa Kazakhstan
Katika nchi hii iliyochanganyika kihistoria yenye makabila mengi kama 150, kwa upande wa kijamii na kisiasa, swali kubwa ni la watu wachache wa Urusi, amesema hayo mwandishi wa habari Chiara Zappa, Gazeti la ‘Mondo e Missione’ akizungumza na mwandishi wa habari wa Vatican alieyko katika ziara ya Kitume ya papa Francisko nchin Kazakhstan. Kwa mujibu wa Chiara Zappa anachunguza usawa fulani ambao umeonesha muundo wa idadi ya watu wa nchi tangu wakati wa uhuru wake kuwa kundi kubwa zaidi lilikuwa la Kazakh lakini hawakuwa wengi kabisa kutokana na kwamba walikuwa karibu 42% ya wakazi. Warusi walikuwa karibu 37%. Kkabila la Kazakh kiukweli lilijiona kama la watu wachache katika nyumba yao wenyewe kutokana na nafasi kubwa ambayo Warusi walikuwa nayo katika jamii na katika utawala.
Ili kubadilisha minganisho huo ilichukua miaka:, kwa maana hiyo kiongozi Nazarbayev alifanya kazi ya kukumbuka 'oralmandar', Kazakhs ambao waliishi nje ya jimbo jipya, na baadue kulikuwa na uhamiaji wa wakati mmoja wa kipande kikubwa cha watu wa Kirusi kuelekea taifa la Kazakhstan. Leo hii, thuluthi mbili ya wakazi milioni 19 ni wa kabila la Kazakhstan. Ni ule unaoitwa “Mwamko wa Kazakh”, ingawa wakati huo huo, katika muktadha wa sera za ujumuishaji wa vikundi mbali mbali vilivyopo nchini, haki za Warusi, kama vile utambuzi wa lugha, hazijapuuzwa.
Hofu kwa misimamo mikali ya Kiislamu
Badala yake, kwa kutazama upande wa kidini, huko Kazakhstan uhusiano kati ya watu na dini umesisitizwa kila wakati amebainisha Chiara Zappa, kiasi kwamba uhuru wa kuabudu ni moja ya alama kuu za siasa za Kazakh. Na umakini huu wa mazungumzo unaenda sambamba na udhibiti wa uwezekano wa kuongezeka kwa makundi yenye itikadi kali ya Kiislamu. Ikiwa ni kweli, kwamba katika miji mikubwa kuna mwelekeo wa dini rasmi zaidi, isiyo na mizizi sana katika maisha ya kila siku, maeneo ya vijijini ni ya kiutamaduni zaidi na, juu ya yote, hatua zinazolenga kupunguza hatari zozote zinaelekezwa kwa hayo. Ukuaji wa misimamo mikali inayotokana na Afghanistan, kama ilivyotokea pia nchini Pakistan, ni chanzo cha wasiwasi ameisitiza Zappa.
Ujenzi wa udugu
Msisitizo, kwa upande wa Bi Chiara Zappa, umewekwa juu ya ukweli kwamba mazungumzo na udugu hutoka chini na kutoka kwa maisha halisi ya watu. Huo ndiyo ufunguo wa kuunda vifungo katika kiini cha kijamii cha kushikamana. Wakati vitendo kutoka chini vinavuka kwa maelewano na wale wa viongozi, basi matunda bora zaidi yanahitajika. Kongamano la viongozi wa Dini za ulimwendi na dini za jadi hunafanyika katika muktadha huu, ambalo linaleta pamoja wajumbe zaidi ya mia moja kutoka nchi 50 huko Nur-Sultan na ambapo Papa Francisko ambaye anashiriki. Kwa maana hiyo Bi Chiara amehitimisha kuwa “ Siku zote huwa najiamini kunapokuwa na mipango ya mikutano ninawaombe neema. Ni kweli wakati mwingine viongozi wanapo shindwa kushirikisha msingi katika juhudi zao, lakini thamani kubwa ya kiishera inabakia. Kwa kuona kuwa viongozi wa Dini wanaendeleza mnyororo wa maombi ya kawaida kwangu inaonekana kama njia pekee ya kujenga ufahamu kwa ulimwengu mzima”.