Rais mpya wa  Kenya Bwana William Ruto akitoa kiapo Septemba 13. Rais mpya wa Kenya Bwana William Ruto akitoa kiapo Septemba 13. 

Kenya:Rais Ruto ameahidi kubadili maisha ya watu atakaowaongoza

Mnamo Septemba 13 nchini Kenya imekuwa ni siku muhimu kwa kuona anaapishwa kiongozi wa awamu ya tano Rais William Ruto ambaye ameahidi kutimiza ahadi za kampeni ya uchuguzi. Rais katika hotuba yake aliziomba serikali za maeneo ya Afrika mashariki,ya kati na magharibi kushirikiana na Kenya ili mbolea inapatikane kuongeza uzalishaji wa chakula.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Hatimaye kenya imefunguwa kwa mara nyingine tena ukurasa mpya na kumkaribisha rais wa tano William Ruto aliyeapishwa tarehe 13 Septemba 2022. Katika afla hiyo walifika Viongozi na marais 20 wa Afrika ili kumpongeza Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua wa[ Audio Embed Siku ya kiapo cha rais William Ruto wa Kenya na ahadi ya kuwainua wananchi]liokula kiapo mbele ya umati mkubwa katika uwanja wa Mpira.  Katika matamkoa yao, viongozi hao wapya wa taifa wameliahidi kuyabadili maisha ya watu wa Kenya licha ya hali ngumu ya kiuchumi.  Hata hivyo kwa upande wa watu wakenya a wananayo hamu kubwa ya kuona uteuzi atakaoufanya kwenye Baraza lake la Mawaziri na nyadhifa zingine kuu serikalini ili kufanikisha agenda zake na zaidi hata kwa ngazi ya wanawake.

Makamu Rais wa Kenya Bwana  Rigathi Gachagua akiapa
Makamu Rais wa Kenya Bwana Rigathi Gachagua akiapa

Rais mpya wa Kenya William Ruto katika hotuba yake alitangaza mikakati muhimu ambayo alisema italiwezesha taifa hilo kuimarika kiuchumi. Akizungumza baada ya kuapishwa kuwa rais, Bwana Ruto alitangaza  wali ya yote hata kushusha bei ya mbolea  kutoka shilingi elfu sita mia tano kwa mfuko mmoja wa kilo hamsini hadi shilini elfu tatu mia tano. Amesema kwamba bei hiyo mpya itaanza kutekelezwa kuanzia wiki ijayo huku serikali yake ikijaribu kuibadilisha sekta ya kilimo nchini. Bwana Ruto alisema kwamba wakati wa kampeni za uchaguzi, walikusanya maoni kutoka kwa wananchi ambao walilalamikia kupanda kwa bei za bidhaa muhimu. Kwa hiyo  licha ya serikali iliopita kujaribu kusuluhisha swala hilo, kupitia kutoa ruzuku hali ya kiuchumi ya Wakenya imezidi kudorora.

Viongozi wa Mataifa walifika katika afla ya kitaifa
Viongozi wa Mataifa walifika katika afla ya kitaifa

Kutokana na hilo serikali yake itaangazia suala hilo la ruzuku ili kuhakikisha kwamba bei za bidhaa muhimu zinapunguzwa. Kiongozi huyo mpya ameshtumu tabia ya kuficha bidhaa kwa lengo la kupandisha bei na kuzitaka serikali za kaunti kuhakikisha kwamba mbolea inapatikana miongoni mwa wakulima.  Rais William vile vile katika hotuba yake aliziomba serikali katika maeneo ya Afrika mashariki, ya kati na magharibi kushirikiana na Kenya katika kuhakikisha kwamba mbolea inapatikana ili kuanza safari ya kuongeza uzalishaji wa chakula. Hakuishia hapo katika hotuba yake Rais William Ruto kwani alisema juu ya ahadi yake ya kurejesha shughuli za utaratibu wa kutoa bidhaa katika bandari ya Mombasa na amefichua kwamba atatoa maagizo zaidi kuhusu utendakazi wa bandari ya Mombasa ili kuwezesha urahisi wa kufanya biashara na kuinua uchumi wa Mombasa.

Siku ya kiapo cha Rais Ruto nchini Kenya
Siku ya kiapo cha Rais Ruto nchini Kenya

Akiendelea Kiongozi huyo mpya wa Kenya alibainisha kuwa kulingana na ahadi yake ya kuunga mkono uhuru wa Idara ya Mahakama, atawapandisha cheo majaji ambao waliteuliwa na Tume ya Huduma za Mahakama (JSC) mwaka wa 2019. Ruto alisema kwamba yeye mwenyewe ataongoza hafla ya kuapishwa kwa majaji hao, Aggrey Muchelule, George Odunga, Weldon Korir na Joel Ngugi mnamo Jumatano, Septemba 14. “Ili kudhihirisha zaidi dhamira yangu ya uhuru wa mahakama, mchana wa leo, nitawateua majaji sita ambao tayari wamependekezwa kuteuliwa katika mahakama ya rufaa iliyofanyika miaka mitatu iliyopita. Kesho nitaongoza kuapishwa kwao ili waweze kuendelea na shughuli ya kuwahudumia watu wa Kenya”.

Rais William Ruto ameongezea kuwa mtangulizi wake Uhuru Kenyatta ataendelea kuwa mwenyekiti katika eneo la Afrika Mashariki. Akitoa tangazo hilo, Bwana Ruto alimpongeza rais huyo anayeondoka madarakani kwa kazi nzuri ya kuhakikisha amani katika eneo zima. Alimpongeza Bwana Uhuru kwa kuongoza mipango ya amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na Ethiopia. "Ninajitolea, kwa mipango ya amani katika eneo letu, ikiwa ni pamoja na Ethiopia na Ukanda wa Maziwa Makuu, nimemwomba kaka yangu, Rais Uhuru Kenyatta, ambaye amefanya mazungumzo ya kupongezwa na wakuu wa maeneo hayo na amekubali kuendelea kuwa mwenyekiti wa majadiliano kwa niaba ya watu wa Kenya.

Siku ya kiapo cha Rais Ruto nchini Kenya
Siku ya kiapo cha Rais Ruto nchini Kenya

Katika hotuba yake ya kwanza kama Mkuu wa nchi, ya Kenya Bwana Ruto alisema kuwa alikuwa ameelekeza afisi husika kumpa afisa mkuu wa polisi IG mamlaka ya kifedha. Mara tu itakapotekelezwa, afisi ya Polisi IG, ambayo inakaliwa na IG Hillary Mutyambai, atakuwa afisa wa uhasibu rasmi wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS). Tangazo hilo linahamisha mamlaka iliyokuwa chini ya Ofisi ya Rais, iliyoongozwa na mtangulizi wake Uhuru Kenyatta. “Ninapozungumza nanyi, nimeagiza vyombo vinavyotoa uhuru wa kifedha kwa Jeshi la Polisi kwa kuhamisha bajeti yao kutoka Ofisi ya Rais na kumteua Inspekta Jenerali kuwa afisa mhasibu na kuwekwa mezani kwangu ifikapo leo mchana.”  Wakati wa kampeni, Ruto alilalamika kuwa Huduma ya Kitaifa ya Polisi ilikuwa ikitumiwa kueneza maswala ya kisiasa. Rais William Ruto amewahakikishia wazazi  nchini Kenya kwamba ataanzisha jopo kazi la mageuzi ya elimu litakalosimamia ushirikishwaji wa umma unaolenga kurekebisha Mtaala wa elimu ya (CBC)

Alipokuwa akitoa hotuba yake ya kuapishwa Bwana Ruto alishiriki matatizo ya wazazi ambao wanapata shida na  mfumo wa elimu huku kundi la kwanza la wanafunzi likitarajiwa kujiunga na shule muhula wa pili.  "Ushiriki wa umma ni muhimu katika suala hili. Nitaanzisha jopokazi la kurekebisha elimu katika ofisi ya rais ambalo litazinduliwa wiki zijazo.  Kikosi kazi kitaendana na matakwa ya kikatiba ya ushirikishwaji wa umma”.

Siku ya kiapo cha rais William Ruto wa Kenya
14 September 2022, 14:49