Tafuta

Malkia wa Uingereza ameaga dunia tarehe 8 Septemba 2022 akiwa na umri wa miaka 96 Malkia wa Uingereza ameaga dunia tarehe 8 Septemba 2022 akiwa na umri wa miaka 96 

Malkia Elizabeth II ameaga dunia na Mfalme mpya Charles anamkumbuka mama yake mpendwa!

Tangazo la kifo lilitokea muda mfupi baada ya saa 7.30 kwa saa za Italia saa 6.30 jioni huko jijini London,baada ya kuwa na wasiwasi uliooneshwa na madaktari tangu saa za alasiri.Sauti ya papo hapo ya wimbo wa taifa ilitangazwa kwa mitandao iliyounganishwa.Umati wa watu ilikusanyika katika Jumba la Buckingham na huko Balmoral.Katika ujumbe wa mrithi Charles amezingatia mapendo ya watu wengi kwa Malkia Elizabeth.

Elizabeth II amekufa kwa amani kama ilivyotangazwa na BBC. “London Bridge is down” yaani daraja la London liko chini limeanguka”ni kwa maneno haya ya kificho ambapo katibu wa Malkia alitangaza kifo chake kwa Waziri Mkuu Liz Truss na maafisa wengine wachache wa Uingereza. Katika habari rasmi, iliyobandikwa katika bango leusi lililo tundikwa na mtumishi kwa kuomboleza kwenye lango la Jumba Kuu la  Buckingham na watangazaji waliovalia mavazi meusi ya mitandao ya umoja ya BBC, Uingereza ilikuwa na hakika kwamba ilikuwa imempoteza mfalme aliyeishi kwa muda mrefu zaidi katika historia yake, na umati wa watu waliokusanyika mbele ya Jumba la Buckingham  na kwenye Jumba la Balmoral, ambapo Elizabeth alikuwa amekaa wiki chache zilizopita, wamekaa wakisali.

Taarifa kza awali uhusu afya yake Malkia Elizabeth

Taarifa kuhusi  afya ya Malkia Elizabeth ilianza kuvuja mapema alasiri, na wasiwasi uliooneshwa na madaktari na kuwasili Balmoral, watoto wake wanne na wengine wa familia. Habari za uchungu huo zilikuwa za ghafla, siku mbili tu zilizopita, picha rasmi ya Jumba la Buckingham ilionesha akitabasamu, ingawa amechoka, alipokutana na Liz Truss siku ya kuteuliwa kwake kama Waziri mkuu. Malkia Elizabeth, mwenye wa  umri wa 96, ndiye mfalme aliyeishi kwa muda mrefu zaidi wa Uingereza na mfalme mzee zaidi duniani, alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya matukio ya kukosa kusimama kwa miezi kadhaa.

Ujumbe wa Mfalme Charles III

Tarehe 9 Septemba Baraza la Urithi litakutana kutangaza jina la mfalme mpya, Mfalme Charles. Na katika ujumbe wake anaandika mfalme mpya kuwa: “Kifo cha mama yangu mpendwa ni wakati wa huzuni kubwa kwangu na kwa wajumbe  wote wa familia yangu. Ninajua kwamba kifo chake kitasikika sana nchini kote, ufalme, Jumuiya ya Madola na watu wengi ulimwenguni. Kwa kuongeza ameandika “Inafariji ufahamu wa mapenzi na heshima iliyohisisiwa kwa malkia”.

Askofu Mkuu Welby:Asante sana kwa kujitolea kwa ufalme wako

Ujumbe mwingi wa ukaribu na sala katika masaa ya mwisho huko Balmoral, kabla na baada ya habari za kifo chake umefika. Naye Askofu Mkuu wa Jimbo la Canterbury, Justin Welby, alijumuika mara moja katika maombolezo ya taifa, Jumuiya ya Madola na dunia nzima huku akimwombea Mfalme na Familia ya Kifalme ili Mwenyezi Mungu awape faraja. Askofu Mkuu Welby ameandika: “Tumempoteza mtu ambaye uaminifu wake usioyumba, utumishi na unyenyekevu vimetusaidia kujitambua sisi ni nani katika miongo kadhaa ya mabadiliko ya ajabu”. Amesisitiza hayo akichanganya huzuni na shukrani nyingi kwa kujitolea kwa ajabu kwa Malkia kwake. Askofu mkuu amekumbuka nyakati za janga ambalo alitia tumaini, wakati wa kuomboleza kwa kufiwa na mwenzi wake ambapo alionesha ujasiri na kila wakati akiwaweka wengine kwanza, kama ishara ya mani kubwa ya Kikristo. Siku kwa imani na upendo kwa Mungu. Urithi anaouacha mwenye enzi ni wa ajabu,” anasisitiza askofu mkuu, ambaye kwa kumbukumbu ya kibinafsi inayohusishwa na matukio mengi ya kukutana anataja uwazi wake wa mawazo, uwezo wa kusikiliza kwa makini, akili inayouliza, ucheshi, na wema usio wa kawaida ambao amesema “siku zote umeniacha na ufahamu wa baraka ambayo imekuwa kwa ajili yetu sote”.

08 September 2022, 21:59