Tafuta

Rais Putin kwa upande wake, ametoa onyo kali kwa nchi zile ambazo zinatishia uhuru wa eneo la Urussi. Rais Putin kwa upande wake, ametoa onyo kali kwa nchi zile ambazo zinatishia uhuru wa eneo la Urussi. 

Rais Putin Atishia Ulimwengu Kutumia Silaha za Nyuklia! Hatari

Rais Putin, ameitishia Jumuiya ya Kimataifa kwamba, akilazimika atatumia hata silaha za kinyuklia, hatari kubwa kwa amani na usalama wa Jumuiya ya Kimataifa. Kwa upande wake Serikali ya China inawaalika wahasimu wa pande zote mbili, kukaa kwa pamoja na kuendeleza majadiliano katika ukweli na uwazi, ili kusitisha vita ambayo tayari imekwisha kusababisha maafa makubwa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Rais Vladimir Putin wa Urussi ametia mkwaju kwenye amri ya kuongeza idadi ya wanajeshi ambao wako tayari kwenda mstari wa mbele kupambana dhidi ya nchi za Umoja wa Ulaya zinataka kuiangamiza Urussi kwa kuwatumia wananchi wa Ukraine kuingia vitani kwa lazima. Rais Putin, Jumatano tarehe 21 Septemba 2022 ameitishia Jumuiya ya Kimataifa kwamba, akilazimika atatumia hata silaha za kinyuklia, hatari kubwa kwa amani na usalama wa Jumuiya ya Kimataifa. Kwa upande wake Serikali ya China inawaalika wahasimu wa pende zote mbili, kukaa kwa pamoja na kuendeleza majadiliano katika ukweli na uwazi, ili kusitisha vita ambayo tayari imekwisha kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao.

Russia sasa imekuwa ni tisho kwa amani na usalama wa Jumuiya ya Mataifa
Russia sasa imekuwa ni tisho kwa amani na usalama wa Jumuiya ya Mataifa

Rais Putin kwa upande wake, ametoa onyo kali kwa nchi zile ambazo zinatishia uhuru wa eneo la Urussi, kwamba, watakiona kile kilicho mnyoa Kanga manyoya na wala kauli hii si ya kuchukuliwa kiulaini kiasi hicho. Amesema, Urussi itatumia uwezo wake wote kulinda nchi na raia wake. Urussi kwa sasa hivi inaendelea kuwakusanya askari wa akiba tayari kuingia vitani. Urussi ina silaha za kutosha kujilinda. Askari 300, 000 wa akiba wataingizwa katika vikosi vya ulinzi na usalama tayari kwa mapambano, amesema Bwana Serghej Shoigu, Waziri wa Ulinzi na Usalama wa Urussi. Walau wanahitajika zaidi ya watu milioni 25 ili kuendesha vita, kwani kwa sasa Urussi inapambana vikali na Nchi za Ulaya ya Magharibi.

Rais Putin

 

22 September 2022, 15:24