Mlima Kilimanjaro, Tanzania:Siku ya Utalii duniani kila  tarehe 27 Septemba Mlima Kilimanjaro, Tanzania:Siku ya Utalii duniani kila tarehe 27 Septemba 

Siku ya Utalii duniani:Kutafakari kwa upya Utalii kwa mafanikio na uthabiti kwa wote

Katika ujumbe kwa Katibu Mkuu wa UN kwa siku ya Utalii duniani Septemba 27 anasema ni azima kuwekeza katika utalii safi na endelevu,kupunguza matumizi ya sekta ya nishati,kuchukua hatua zinazolenga kufikia sifuri uzalishaji na kulinda viumbe hai.Hakuna wakati wa kupoteza.Hebu tufikirie upya na kuunda upya utalii na tutoe mustakabali endelevu wenye mafanikio na uthabiti kwa wote.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kila tarehe 27 Septemba ya kila mwaka Umoja wa mataifa (UN) unaadhimisha Siku ya Utalii duniani. Katika fursa hiyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana Antonio Gutterress ametoa ujumbe wake ambapo anasema kwamba Siku ya Utalii Duniani huadhimisha uwezo wa washiriki wa kukuza ushirikishwaji, kulinda asili na kukuza uelewa wa kitamaduni. Utalii ni kichocheo kikubwa cha maendeleo endelevu. Inachangia elimu na ukombozi wa wanawake na vijana na kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi na kitamaduni. Inachukua jukumu muhimu katika mifumo ya ulinzi wa kijamii ambayo huunda msingi wa uthabiti na ustawi. Ni lazima kuwekeza katika utalii safi na endelevu, kupunguza matumizi ya  sekta ya nishati, kuchukua hatua zinazolenga kufikia sifuri uzalishaji na kulinda viumbe hai. Tunahitaji kubuni nafasi za kazi zenye staha na kuhakikisha kwamba faida inanufaisha nchi na jumuiya za wenyeji.

27 Septemba ni Siku ya Utalii Duniani
27 Septemba ni Siku ya Utalii Duniani

Shughuli za utalii za serikali, biashara na watumiaji lazima zifuate Malengo ya Maendeleo Endelevu na Dhamira ya 1.5. Uhai wa sekta hii na maeneo mbalimbali ya utalii, kama vile mataifa madogo ya visiwa vinavyoendelea, inategemea hii. Mkutano wa mwaka huu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari, ambapo Jumuiya ya kimataifa na sekta ya utalii wameahidi kutayarisha makubaliano ya kisheria kuhusu uchafuzi wa plastiki ifikapo 2024, unawakilisha hatua muhimu ya kwanza. Hakuna wakati wa kupoteza. Hebu tufikirie upya na kuunda upya utalii na, kwa pamoja, tutoe mustakabali endelevu zaidi, wenye mafanikio na uthabiti kwa wote.

"Kutafakari upya utalii” ndiyo kauli mbiu ya Siku ya Utalii duniani

Watalii wa kimataifa waliowasili mwanzoni mwa 2022 walikuwa maradufu ya kiwango kilichorekodiwa mwaka wa 2021. Katika baadhi ya kanda waliowasili tayari wako katika, au hata juu zaidi, viwango vya kabla ya janga. Kuondolewa kwa vizuizi vilivyosalia vya usafiri, pamoja na kuongezeka kwa imani ya watumiaji, kutakuwa vichocheo muhimu kwa ajili ya kurejesha sekta hiyo, na kuleta matumaini na fursa kwa mamilioni ya watu duniani kote. Siku ya Utalii Duniani inaadhimishwa  huku mabadiliko ya kuelekea utalii yakitambuliwa kama nguzo muhimu kwa maendeleo na maendeleo yanapoendelea. Mnamo Mei 2022 ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kufanya mjadala maalum kuhusu utalii, kuonesha umuhimu wa kihistoria wa sekta hiyo. Utalii sasa ni ajenda ya serikali na mashirika ya kimataifa katika kila eneo la kimataifa.

Mlima Kilimanjaro Tanzania
Mlima Kilimanjaro Tanzania

Wakati huo huo, maeneo na biashara zinajirekebisha kikamilifu ili kukabiliana na changamoto na majukumu, kama inavyooneshwa na wimbi la watu waliotia saini Azimio la Glasgow kuhusu Hatua za Tabianchi  katika Utalii, lililoongozwa na UNWTO. Ikumbukwe azimio la Glasgow  ni maelewano ya kuharakisha hatua za tabianchi katika utalii na kupata ahadi dhabiti za kuunga mkono malengo ya kimataifa ya kupunguza kwa nusu ya uzalishaji wa hewa chafuzi katika muongo ujao na kufikia uzalishaji  Zero haraka iwezekanavyo kabla ya 2050. Kwa maana hiyo zaidi ya mashirika 450 yalitia saini tamko hilo.

Siku ya Utalii duniani 2022:Tufafakari kwa upya Utalii
Siku ya Utalii duniani 2022:Tufafakari kwa upya Utalii

Katika Siku ya Kimataifa ya Maadhimisho ya Utalii inaweka watu katikati ya mijadala muhimu. Je Utalii unakwenda wapi? Je tunataka kwenda wapi? Na je tunafikaje huko? Katika fursa ya tukio hili la siku ya Utalii ikwa mwaka 2022 inaongozwa na Kaulimbiu ya "Kufikiria Utalii upya" ambapo inalenga kuhamasisha mjadala kuhusu kufikiria kwa upya utalii kwa ajili ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na kupitia elimu na kazi, na matokeo ya  utalii kwenye sayari na fursa za kukua kwa njia endelevu zaidi.

Siku ya Utalii duniani 2022: Tutafakari kwa upya Utalii
27 September 2022, 11:19