Watu wengi wanajiua na hasa kwa upande wa bara la Afrika Watu wengi wanajiua na hasa kwa upande wa bara la Afrika 

Kampeni ya taarifa za WHO barani Afrika ili kuongeza uelewa mwa watu

Kutibu afya ya akili ili kuzuia ongezeko la watu wanaojiua,ndiyo Kampeni ya tarifa za Shirila la Afya Ulimwenguni (WHO) kwa bara la Afrika lote ili kuongezea uelewa kwa watu.Sababu yake ni kwamba Bara hilo lina idadi kubwa zaidi ulimwenguni pote:kwa kila wakaaji 100,000 kuna wastani wa watu 11 wanaojiua,huku ulimwenguni wastani ni watu 9 wanaojiua kwa kila wakaaji 100,000.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeanza kampeni ya kutoa taarifa barani Afrika ili kuongeza uelewa miongoni mwa nchi na idadi ya watu kuhusu afya ya akili, ambayo ni moja ya sababu zenye matatizo ambayo serikali mahalia  hazikabiliani nazo sana kuhusu kiwango cha kujiua. Bara hilo lina idadi kubwa zaidi ulimwenguni pote: kwa kila wakaaji 100,000 kuna wastani wa watu 11 wanaojiua, huku ulimwenguni wastani ni watu 9 wanaojiua kwa kila wakaaji 100,000. Jambo lililofichwa katika jamii za Kiafrika ambalo hata hivyo linaonekana wazi katika takwimu, kwani  kulingana na takwimu za hivi karibuni kutoka Benki ya Dunia iliyosasishwa hadi 2019 ya nchi kumi ulimwenguni kwa kiwango cha vifo zaidi  kutokana na kujiua, nchi tatu zilikuwa za Kiafrika  ambazo ni  Lesotho, Eswatini na Afrika Kusini na  wakati kulingana na takwimu za WHO zingekuwa hata nchi sita za Afrika kati ya kumi za kwanza.

Kulingana na takwimu za  Benki ya Dunia, Lesotho ina kiwango cha vifo karibu mara mbili (72.4 kwa kila wakazi 100,000) ikilinganishwa na Guyana, nchi ya pili katika orodha hii ya kutisha (watu 40 wanaojiua kwa kila wakazi 100,000). Nchi nyingine za Kiafrika hazina takwimu kama nchi  tatu zilizotajwa, lakini idadi inaongezeka. Hii ni kesi ya nchi ya Cameroon ambayo kati ya mwaka 2012 na 2019 ilishuhudia kiwango cha kujiua kikiongezeka kutoka asilimia 4.9 hadi 12.2, lakini pia kesi ya Zimbabwe, Namibia na Afrika Kusini. Na wanaofanya kitendo hicho ni wanaume. Kwa ujumla, inakadiriwa kuwa katika Afrika kwa kila  tendo la kujiua kuna majaribio ishirini yasiyofanikiwa.

Miongoni mwa sababu kuu za janga hili  ni afya ya kiakili, tatizo ambalo takwimu zake barani Afrika zinaongezeka, pia kutokana na janga Uviko-19,  lakini ambalo linanyanyapaliwa na tamaduni mahalia.   Kutokana na Siku ya Afya ya Kimataifa ya Afya ya Akili , iliyofanyika tarehe 10 Oktoba  na iliyoongozwa na kauli mbiu: “Fanya afya ya akili na ustawi kwa wote kipaumbele cha kimataifa”,  Shirika la Afya Ulimwenguni WHO ilijikita katika kuchambua hatua za kuzuia hali hiyo. Nchi za Afrika ndizo ambazo duniani kote zinajishughulisha kidogo na huduma za wagonjwa wanaougua ugonjwa wa akili, ambao kulingana na WHO huathiri kiwango cha kujiua katika ngazi ya bara kwa asilimia 11. Kulingana na maagizo ya kimataifa, gharama za afya ya akili zinatakiwa kuwa dola mbili kwa kila mtu katika nchi zenye kipato cha chini. Wastani wa matumizi ya serikali za Afrika, kwa upande mwingine, ni dola 0.50, ambayo licha ya kila kitu inawakilisha uboreshaji ikilinganishwa na dola 0.10 zilizotengwa mwaka 2017.

Bara pia halina wataalamu wa kutibu matatizo haya. Madaktari wachache wa magonjwa ya akili wote wamejikita katika maeneo ya mijini, na hivyo kufanya watu wanaoishi vijijini wasiweze kupata huduma. Lakini hata upatikanaji usio sawa na kutatua tatizo, kwa kuwa imehesabiwa kuwa kwa kila wakazi nusu milioni barani Afrika kuna mtaalamu mmoja tu. Takwimu mara mia  chini ya mapendekezo ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO). Kwa kuzingatia mahitaji yanayoongezeka, nchi za Afrika ziliamua katika kikao cha mwisho cha baraza la kikanda la WHO mwezi  Agosti uliyopita kuzindua mkakati ambao una muda  hadi  2030. Nchi zote zitalazimika kuidhinisha sheria za dharura kufikia tarehe hiyo, kuhusu afya ya akili (kwa sasa ni asilimia 49 tu ya nchi ambazo zimepitisha sheria kuhusu suala hilo), ambayo zitalazimika kutekelezwa na angalau asilimia 60 ya nchi hadi mwisho mwa mpango huo. Aidha, ifikapo mwaka 2030 nchi nyingi zitalazimika kuanza kufuatilia hali ya idadi ya watu kulingana na vigezo vilivyotolewa na WHO, ambapo katika miaka ya hivi karibuni tayari imezindua mipango ya udhibiti ili kusaidia baadhi ya nchi. Maendeleo ya mkakati huu yatakuwa na hatua mbili za kati mwaka 2025 na 2028 ili kuthibitisha maendeleo yake.

Hii ni hatua ya kwanza katika kukabiliana na tatizo la watu kujiua katika bara hilo, lakini si lazima liwe pekee. Miongoni mwa sababu nyingine zinazomsukuma mtu kujitoa uhai pia kuna hali ya umaskini uliokithiri unaoathiri nchi moja moja. Katika hali hiyo, hatua za serikali lazima ziwe kamili zaidi na sio tu kuhusiana na nyanja ya afya, kwa kuzingatia kwamba sababu za migogoro ya kiuchumi sio za Kiafrika tu  bali zinatoka nchi nyingine. Hili si tatizo dogo katika bara ambalo linaonekana kuzidi kukabiliwa na machafuko ya mara kwa mara ya siasa za kimataifa.

19 October 2022, 16:13