Jamhuri ya Korea imekubali kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika ujenzi wa chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasilino (TEHAMA) nchini Tanzania. Jamhuri ya Korea imekubali kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika ujenzi wa chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasilino (TEHAMA) nchini Tanzania.  

Korea Kusini Kusaidia Ujenzi wa Chuo Cha TEHAMA: Sayansi na Teknolojia Kwa Watanzania

Serikali ya Jamhuri ya Korea imekubali kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika ujenzi wa Chuo Cha Teknolojia ya Habari na Mawasilino (TEHAMA) nchini Tanzania. Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa lengo la Chuo hicho ni kuwasaidia vijana kuendeleza ubunifu wao na kuonesha namna wanavyoweza kuunda vifaa mbalimbali kwa matumizi ya watu!

Na Ofisi ya Waziri Mkuu, - Seoul, Korea ya Kusini.

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Korea imekubali kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika ujenzi wa chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasilino (TEHAMA) nchini Tanzania. Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa lengo la chuo hicho ni kuwasaidia vijana kuendeleza ubunifu wao na kuonesha namna wanavyoweza kuunda vifaa mbalimbali “Mpango wa Rais wetu wa kuwapa vijana shughuli za kufanya katika eneo la Sayansi na Teknolojia ni mpango ambao unaungwa mkono na Serikali ya Korea.” Waziri Mkuu amesema hayo Oktoba 27, 2022 baada ya kumaliza mazungumzo ya kiserikali na Waziri Mkuu wa Korea Kusini, Han Duck-Soo katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu uliopo Seoul.

Korea ya Kusini imetia nia ya kusaidia ujenzi wa Chuo cha TEHAMA, Tanzania
Korea ya Kusini imetia nia ya kusaidia ujenzi wa Chuo cha TEHAMA, Tanzania

Tarehe 14 Oktoba 2021 Mheshimiwa Rais Samia akizungumza katika kilele cha Mbio za Mwenge kitaifa kwenye Viwanja vya Magufuli, Wilayani Chato, Mkoani Geita, alisema Serikali inatarajia kujenga chuo bora zaidi cha kisasa cha TEHAMA ili kuongeza kasi, ubunifu na ufanisi katika matumizi ya teknolojia hiyo. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekutana na Viongozi wa Kampuni ya Mirae Chemical ambao wanajenga kiwanda cha kuchakata maganda ya korosho baada ya kubanguliwa ambacho kwa mara ya kwanza teknolojia hiyo inaingia nchini Tanzania. “Hii ni fursa kubwa kwa wakulima wetu, hiki kilikuwa ni kilio kikubwa kwa wakulima, tumezungumza nao na kuwasisitiza waendelee na ujenzi katika eneo la Mkuranga. Kiwanda hiki kitakuwa kinakusanya maganda ya korosho kwa wakulima, hii ni fursa kwa wakulima kwani itaongeza tahamani ya zao hilo.” Amesema kuwa kwa sasa Serikali itahamaisha Halmashauri nchini kutafuta maghala kwa ajili ya kukusanya maganda ya korosho yaliyonunuliwa kutoka kwa wakulima. “Wakulima sasa wajipange kuuza maganda ya korosho, kwasasa ubanguaji utafanyika ndani ya nchi na wakulima wataanza kuuza maganda pamoja na mbegu inayopatikana kwenye zao la korosho.

29 October 2022, 17:53