Tafuta

Siku ya kutokomeza njaa duniani. Siku ya kutokomeza njaa duniani. 

Siku ya kutokomeza Umaskini duniani 2022:Haki kwa wote kwa vitendo!

Kauli mbiu ya mwaka 2022 katika siku ya kutokomeza Umaskini duniani ni 'Hadhi kwa Wote kwa Matendo.Ahadi tunazofanya pamoja kwa ajili ya haki ya kijamii,amani na sayari.'Umaskini na ukosefu wa usawa usio lazima ni matokeo ya maamuzi ya kimakusudi au kutochukua hatua ambayo inawanyima uwezo maskini na waliotengwa katika jamii zetu na kukiuka haki zao msingi.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Hadhi kwa wote kwa matendo. Ahadi tunazofanya pamoja kwa ajili ya haki ya kijamii,amani na sayari ndiyo kauli mbiu inayoongoza Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Umaskini 2022-2023. Katika kilele cha cha siku hiyo ifanyikayo kila mwaka tarehe 16 Oktoba, zimepyaishwa miito ya kuzingatia suala hili kwa makini katika ulimwengu wa umaskini. Hadhi kwa mwanadamu sio tu haki ya kimsingi yenyewe bali ni msingi wa haki zingine zote msingi. Kwa hiyo, heshima sio dhana ya kufikirika, ni ya kila mmoja. Leo, hii watu wengi wanaoishi katika umaskini unaoendelea, wananyimwa hadhi na utu wao na kudharauliwa. Kwa kujitoa kukomesha umaskini, kulinda sayari na kuhakikisha watu wote kila mahali wanafurahia amani na ustawi, ndiyo Ajenda ya mwaka  2030, ambapo inasisitiza tena ahadi ile ile iliyowekwa chini ya Azimio la Kimataifa la Haki za Kibinadamu. Hata hivyo, hali halisi ya sasa inaonesha wazi kuwa watu bilioni 1.3 bado wanaishi katika umaskini wa pande nyingi na karibu nusu yao ni watoto na vijana.

Inawezekana kutokomeza umaskini ikiwa ubinafsi utafutika duniani
Inawezekana kutokomeza umaskini ikiwa ubinafsi utafutika duniani

Ukosefu wa usawa wa fursa na mapato unaongezeka kwa kasi na, kila mwaka, pengo kati ya matajiri na maskini linaongezeka zaidi. Katika mwaka uliopita 2021 wakati mamilioni ya watu wakihangaika kupitia mmomonyoko wa haki za wafanyakazi na ubora wa kazi ili kufikia siku nyingine, nguvu za shirika na utajiri wa tabaka la mabilionea vimerekodi ongezeko lisilo na kifani. Umaskini na ukosefu wa usawa usio lazima ni matokeo ya maamuzi ya kimakusudi au kutochukua hatua ambayo yanawanyima uwezo maskini na waliotengwa katika jamii zetu na kukiuka haki zao kimsingi. Vurugu za kimya na endelevu za umaskini, kutengwa kwa jamii, ubaguzi wa kimuundo na kupunguzwa uwezo,  inafanya kuwa vigumu kwa watu walionaswa katika umaskini uliokithiri kutoroka na kukana ubinadamu wao.

Inawezekana kutokomeza umaskini ikiwa ubinafsi utafutika duniani
Inawezekana kutokomeza umaskini ikiwa ubinafsi utafutika duniani

Janga la COVID-19 lilimulika hali hii inayobadilika, na kufichua mapungufu mengi ya  mfumo wa ulinzi wa kijamii na vile vile ukosefu wa usawa wa kimuundo na aina mbalimbali za ubaguzi ambazo zinazidisha na kuendeleza umaskini. Zaidi ya hayo, hali ya dharura ya hali ya tabianchi ni unyanyasaji mpya dhidi ya watu wanaoishi katika umaskini, kwani jamii hizi zinakabiliwa na matukio ya mara kwa mara ya majanga ya asili na uharibifu wa mazingira, na kusababisha uharibifu wa nyumba zao, mazao na maisha yao.  Mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 35 ya Siku ya Dunia ya Kuondokana na Umaskini Uliokithiri na maadhimisho ya miaka 30 ya Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Umaskini. Siku hii inaheshimu mamilioni ya watu wanaoteseka kutokana na umaskini na ujasiri wao wa kila siku na inatambua mshikamano muhimu wa kimataifa na wajibu wa pamoja tunaoshikilia ili kuondoa umaskini na kupambana na aina zote za ubaguzi.

Inawezekana kutokomeza umaskini ikiwa ubinafsi utafutika duniani
Inawezekana kutokomeza umaskini ikiwa ubinafsi utafutika duniani

Katika ulimwengu ulio na kiwango kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi, njia za kiteknolojia na rasilimali za kifedha, kwamba mamilioni ya watu wanaishi katika umaskini uliokithiri ni hasira ya kiadili. Umaskini si suala la kiuchumi pekee, bali ni jambo la pande nyingi ambalo linajumuisha ukosefu wa mapato na uwezo wa kimsingi wa kuishi kwa utu. Watu wanaoishi katika umaskini wanakumbana na kunyimwa mambo mengi yanayohusiana na kuimarishana ambayo yanawazuia kutambua haki zao na kuendeleza umaskini wao, ikiwa ni pamoja na:hali hatari za kazi, makazi yasiyo salama, ukosefu wa chakula bora, ufikiaji usio sawa wa haki , ukosefu wa mamlaka ya kisiasa, upatikanaji mdogo wa huduma za afya

16 October 2022, 13:38