Tafuta

Watu 19 wamefariki dunia na abiria 26 wameokolewa na wananchi wa kawaida. Watu 19 wamefariki dunia na abiria 26 wameokolewa na wananchi wa kawaida.  

Ajali ya Ndege Bukoba: Sr. Eunice Wangari! Shujaa Maja Munyama!

Watu 19 wamefariki dunia na abiria 26 wameokolewa na wananchi wa kawaida. Watanzania wamesema, kuna haja ya kuimarisha zaidi kitengo cha maafa na shughuli za uokoaji; kuwekeza zaidi katika rasilimali watu na vifaa vya uokoaji. Watanzania wanampongeza Marehemu Burhani Rubaga kwa jitihada zake za kutaka kuokoa maisha ya abiria wake, lakini bila mafanikio yaliyokusudiwa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Ndege ya Shirika la Ndege la Precision Air yenye namba za usajili 5HPWF iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Bukoba kupitia Mwanza Dominika tarehe 6 Novemba 2022 ilishindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba na hatima yake ni kutumbukia Ziwa Victoria mita chache kabla ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba. Watu 19 wamefariki dunia na abiria 26 wameokolewa na wananchi wa kawaida. Watanzania wamesema, kuna haja ya kuimarisha zaidi kitengo cha maafa na shughuli za uokoaji; kuwekeza zaidi katika rasilimali watu na vifaa vya uokoaji. Watanzania wanampongeza Marehemu Burhani Rubaga kwa jitihada zake za kutaka kuokoa maisha ya abiria wake, lakini bila mafanikio yaliyokusudiwa.

Watu 19 wamefariki dunia na wengine 26 wameokolewa na wananchi
Watu 19 wamefariki dunia na wengine 26 wameokolewa na wananchi

Wakati huo huo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Jumapili Novemba 6, 2022 amewasili Mkoani Kagera, na kushuhudia zoezi la uokoaji linaloendelea kufuatia ndege ya Precision Air kupata ajali ilipokuwa ikikaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba. Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika eneo la ajali Waziri Mkuu amewasilisha salam za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wakazi wa Bukoba na Tanzania kwa Ujumla. “Rais Samia ameniagiza kuja kufuatilia zoezi hili na kuhakikisha linakwenda salama, pia ameguswa sana na tukio hili, na amekuwa akifuatilia kwa karibu ili kuhakikisha zoezi la uokoaji linafanyika kwa mafanikio.” Mheshimiwa Majaliwa amewashukuru wakazi wa Mkoa huo pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kujitokeza na kushiriki kutoa msaada na kufanikiwa kuwaokoa abiria 26.

Waombolezaji wakati wa kuaga miili ya watanzania waliofariki dunia 6.11.2022
Waombolezaji wakati wa kuaga miili ya watanzania waliofariki dunia 6.11.2022

Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali inaendelea kufuatilia kwa ukaribu zoezi la uokoaji pamoja na kusimamia kuitoa ndege hiyo katika eneo la ajali, na kutanabaisha kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo. Waziri Mkuu pia ametembelea majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera na na kuwahakikishia kuwa watapewa huduma zinazostahili na kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kusimamia na kufuatilia kwa karibu huduma wanazopewa. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mheshimiwa Waziri Mkuu majeruhi hao wameishukuru Serikali kwa kuwajari kwa kupatiwa huduma kwa haraka tangu walipookolewa kutoka katika eneo la ajali. Mheshimiwa Majaliwa amesema mpaka sasa abiria 26 wameokolewa na kukiwa na miili 19 ambayo imetolewa katika eneo la ajali.

Majaliwa Jackson, Maja Munyama atakumbukwa sana na watanzania
Majaliwa Jackson, Maja Munyama atakumbukwa sana na watanzania

Kati ya wale waliopoteza maisha yumo pia Sr. Eunice Wangari wa Shirika la Mtakatifu Theresia wa Wakarmeli aliyekuwa anafanya utume wake Parokia ya Nyakato, Jimbo kuu la Mwanza. Taarifa kutoka kwa Askofu mkuu Renatus Leonard Nkwande wa Jimbo kuu la Mwanza, Tanzania, zinasema, kwamba, Kanisa linaendelea kufanya taratibu nyingine, zikikamilika waamini watapewa taarifa rasmi. Watanzania na watu wenye mapenzi mema kutoka sehemu mbalimbali za dunia, wanawapongeza wavuvi mkoani Kagera na wananchi katika ujumla kwa jitihada za kuokoa maisha ya abiria wa ndege iliyokuwa imezama, wengi wanamkumbuka mvuvi Majaliwa ambaye alivunja mlango wa ndege kwa kasia lake na abiria wakaanza kutoka, lakini aliuumia na kupoteza fahamu, kwa sasa anaendelea vyema. Habari zaidi zinasema kwamba, Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kwamba, kijana Majaliwa Jackson “Maja Munyama” Mvuvi aliyeshiriki kuokoa abiria kwenye ajali ya ndege Bukoba, akabidhiwe kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na atafutiwe nafasi kwenye Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ili aweze kupewa mafunzo ya ujasiri zaidi.  

Ajali ya Ndege
07 November 2022, 15:48