COP27-Ahadi zilizotolewa na nchi 193 bado hazijatekelezwa!
Na Angella Rwezaula-Vatican.
COP27 ni mkutano wa 27 wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya tabianchi ambao utafanyika huko Sharm El-Sheikh nchini Misri kuanzia tarehe 6 hadi 18 Novemba 2022. Katika Mkutano huo utahudhuriwa na viongozi zaidi ya 100 wakiwemo wakuu wa nchi na serikali kutoka ulimwenguni kote. Mkutano huo utazingatia miongozo ya kukabiliana kikamilifu na mabadiliko ya hali ya tabianchi. Kwa mujibu wa taarifa, za watayarishaji wanamebainisha kwamba wataanzia pale walipoishia mwaka mmoja uliopita hasa kuhusu chaguzi za kisiasa zinazopaswa kufanyiwa kazi na kushiriki michakato ya kufanya maamuzi. Itakuwa fursa ya kutathmini ahadi zilizotolewa katika COP26 huko Glasgow, au jinsi ya kuweka mkakati wa kupunguza ongezeko la joto duniani hadi kufikia ndani ya nyuzi juto 1.5 ° C. Kwa maana hiyo wamebainisha kwamba lengo hili si rahisi kufikiwa, kwa kuzingatia kwamba wastani wa joto duniani tayari umeongezeka kufikia nyuzi 1 ° na kwamba uzalishaji wa gesi chafuzi duniani haupungui katu.
Ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita, hali imekuwa mbaya zaidi na masuala ya dharura ambayo yameibuka na yanahatarisha kudhoofisha hatua za muda mfupi na za muda mrefu za kupambana na mabadiliko ya tabianchi zilizofanywa na nchi duniani kote katika mazingira ya makubaliano ya kimataifa ka mfano vita vya Ukraine, bado vinaendelezwa mdororo wa kiuchumi, mzozo wa nishati, ambao umeanza tena uwekezaji katika mafuta na kama gesi inayozalisha gesi chafuzi. Shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa (Unfccc) na urais wake huki Misri walikutana na kuandaa ajenda pana, na vikao vya suala moja na meza za pande zote. Mada zitakazotolewa kwa kila siku ni kuhusu fedha, kilimo, maji, hupunguzaji wa hewa chafu, bioanuwai, nishati.
Ripoti hiyo mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa, {UNFCCC} inaonesha kwamba ahadi za sasa zilizotolewa na nchi 193 zilizotia saini Mkataba wa Paris kuhusu hali ya hewa zitasababisha ongezeko la wastani wa joto la 2.5 ° C ifikapo 2100 ikilinganishwa na viwango vya kabla ya viwanda. Mkataba badala yake unatoa kwamba ongezeko la joto duniani huwekwa chini ya 2° na ikiwezekana ndani ya 1.5. Ahadi za sasa zitaongeza uzalishaji wa gesi chafuzi kwa 10.6% hadi 2030 (badala ya 13.7% kama ilivyotabiriwa hapo awali), na baadaye kuacha. Bado uzalishaji wa gesi chafuzi hauoneshi mwelekeo wa kushuka kwa kasi ambao sayansi inaona kuwa muhimu katika muongo huu. Ongezeko la ahadi za uondoaji wa ukaa katika nchi moja moja litakuwa mojawapo ya mada kuu za Mkutano wa Tabianchi {COP27}.
Hata hivyo Umoja wa mataifa umebainisha kwamba Misri ihakikishe usalama wa washiriki kiraia.
Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa walisema Misri lazima ihakikishe usalama na ushiriki kamili wa sehemu zote za mashirika ya kiraia. Wimbi la vikwazo vya serikali kwenye maandamano tayari vilizua hofu ya kulipizwa kisasi wanaharakat baada ya miaka ya ukandamizaji unaoendelea na wa muda mrefu dhidi ya mashirika ya kiraia na watetezi wa haki za binadamu. Kukamatwa na kuwekwa kizuizini, vikwazo vya usafiri dhidi ya watetezi wa haki za binadamu vimejenga hali ya hofu kwa mashirika ya kiraia ya Misri ”.