B20 nchini Indonesia nafasi ya dini katika kuzindua majadiliano kati ya Wakuu wa Mataifa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mkutano wa XVII wa B20, ambao ni jukwaa la wakuu wa nchi na serikali, mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu ulioundwa tangu mwaka 1999 baada ya mfululizo wa migogoro ya kifedha, umeanza tarehe 15 na 16 Novemba 2022 huko Bali, Indonesia, ili kupendelea kimataifa uchumi kwa kuzingatia uchumi mpya unaoendelea. Umoja wa nchi za Ulaya na nchi 19 zilizoendelea zaidi kiviwanda duniani zinashiriki, kama vile Saudi Arabia, Argentina, Australia, Brazil, Kanada, China, Korea Kusini, India, Indonesia, Ufaransa, Ujerumani, Japan, Italia, Mexico, Uingereza, Urussi, Marekani, Afrika Kusini na Uturuki. Miongoni mwa mada za mkutano huo, ni mzozo wa chakula, mvutano kuhusu nishati, vita vya Ukraine na matokeo yake duniani, ongezeko la mfumuko wa bei na hatari ya mdororo wa uchumi duniani kwa madhara kwa nchi maskini zaidi.
Migawanyiko kati ya Mashariki na Magharibu ya dunia inashika kasi
Katika hali ambayo migawanyiko kati ya Mashariki na Magharibi ya dunia inazidi kushika kasi, huku China na Urusis zikiwa upande mmoja na Marekani na Ulaya kwa upande mwingine nazo pia ziko kwenye B20 huko Bali, kwa mujibu wa Padre Marcin Schmidt, Padri mmisionari kutoka Poland na mtaalam wa mambo ya mgogoro kwamba "kuna matarajio makubwa ya mkutano unaowezekana kati ya wajumbe wa Urussi na Ukraine, na ule kati ya wajumbe wa Urussi na Amerika na kawaida, kuna maandalizi makubwa pia kuhusu usalama. Sehemu ya jiji la Bali kwa sasa inahisi kama ngome." Huko watakutana na wawakilishi wengi wa nchi nyingine nyingi na pia wa vyama na harakati kwa sababu kati ya mada hizo kuna si tu matarajio, juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa rais wa Kirussi au Kiukreni, lakini Indonesia akiwa ni rais wa sasa wa B20 kwa mwaka 2022, alifafanua wazi jinsi katikati ya mkutano huo kuna uwezo, baada ya Uviko -19, kurejesha uwezekano wa kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya wote kuanzia mabadiliko yanayotokea katika ulimwengu wa kisasa", alisisitiza Padre Schmidt.
Scholas Occurrentes huko Bali
Miongoni mwa harakati za kimataifa zilizopo huko Bali pia kuna Scholas Occurrentes ambao wanashiriki katika mikutano juu ya mada ya elimu. Vijana ni mojawapo ya vipaumbele vya B20, kwa ajili ya majadiliano kati ya vizazi na uwepo wao katika ulimwengu wa kidijitali. Kwa mfano, moja ya majopo ya B20 itahusu ulinzi wa haki za watoto katika ulimwengu wa kidijitali, kutokana na mtazamo wa kisheria na kwa sababu ufikiaji wa mtandao ni wa haki na haki kwa vijana wanaoishi katika nchi zilizo maskini zaidi.
Majadiliano ya kidini
Kwa mujibu wa padre Schmidt alithibitishwa kwamba anaamini kuwa majadiliano ya kidini kidini katika B20 ya Indonesia yanaweza kuwa na jukumu muhimu, pia kwa sababu wako katika nchi, Indonesia ambayo ni mwenyeji wa mkutano wa kilele cha mwaka huu, ambayo kwa ishara yake, katika kauli mbiu yake kuu, isemayo 'Tumeungana katika tofauti'. Majadiliano ya kidini yatakuwa mhusika mkuu katika mikutano mingi huko Bali kwa lengo la kudumisha na kuimarisha uwiano na ushirikiano kati ya viongozi dunia ya kidini hasa kwa ajili ya amani. Kwa mara ya kwanza, kiukweli, mkutano huo unatoa nafasi kwa dini na mchango wao katika maendeleo shirikishi ya mwanadamu na utamaduni wa amani." Ndio maana ilianzishwa ya 'Breligioni 20' ambayo inajumuisha, pamoja na mambo mengine, mkutano kati ya vijana wa dini mbalimbali ili kuzungumzia mchango ambao vizazi vipya na imani za kidini zenyewe zinaweza kutoa katika maendeleo shirikishi ya binadamu. Kwa kutambua umuhimu wa kujumuisha ushirikiano kati ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea ni muhimu sana na katika hali hii dini zinaweza kufanya mengi kwa majadiliano yao kusaidia kujenga utamaduni wa kukutana, utamaduni wa mazungumzo na ushirikiano,” alihitimisha.
Mada kuu
Umakini ambao sio tu kwa wakuu wa nchi lakini kuna mada ya mpito wa nishati, mada msingi kama amani na uchumu, katika urais wa Indonesia wa B20. Mpito ambao lazima uwe wa haki na wa kuunga mkono. Katika ajenda, hata kama si moja kwa moja, kuna mada nyingi ambazo ni sehemu ya Majisterio ya Papa. Hasa, "Uchumi wa Francesco". Katika moja ya matukio kando ya mkutano wa kilele wa B20 kuna majadiliano ya haja ya kuunda uchumi mpya, jumuishi, kwa mfano ulioainishwa huko Assisi. Na ni muhimu kwamba B20 ichunguze maono mapya ya kiuchumi kuanzia pendekezo la Papa. Kwa hakika, huko Bali, mijadala mbalimbali ya kundi la B20 yanajaribu kupendekeza falsafa, mfano wa Indonesia, ambayo inazungumzia maelewano katika uhusiano na wat, wenyewe binafasi, kuanzia katika maelewano na Mungu na asili.