Tafuta

2022.11.29  Gofu la litawashwa taa kwa sababu ya kupinga adhabu ya kifo 2022.11.29 Gofu la litawashwa taa kwa sababu ya kupinga adhabu ya kifo 

Taa kuangaza magofu ya kale na giza la adhabu ya kifo

Tarehe 30 Novemba 2022,jijni Roma na miji mingine elfu mbili itawasha taa katika minara yao maarufu ili kwa pamoja kupinga mateso.Mwanajumuiya ya Mtakatifu Egidio,Marazziti amesema adhabu ya kifo ni ukatili mbaya unaosikindikiza historia ya binadamu,lakini inawezekana kubadilisha dira hiyo.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Italia imetoka mbali kwa miaka 236, lakini bado kuna mengi ya kufanywa, kwa sababu adhabu ya kifo, tangu ilipokomeshwa mnamo tarehe 30 Novemba 1786, kwa mara ya kwanza katika mkoa ambao ulikuwa unatawaliwa na mfalme wa Toscana. Leo hii adhabu hiyo bado imewekwa katika sheria kwa baadhi ya nchi, ambazo kwa hakika ni chache ukilinganisha na mchakato wa historia, ambapo lakini bado kuna hamasisho kuhusu tunu ya haki ya maisha, msingi wa kila haki yoyote ile. Adhabu ya kifo ni msindikizaji katili wa historia ya binadamu, japokuwa tangu mnamo mwaka 1975, wakati kulikuwa na nchi 16 tu ambazo zilikuwa zimesitisha adhabu hiyo, leo hii zinahesabika  zaidi ya nchi 144, na kwa sababu hiyo kuna kupiga hatua ya mbele katika kugeuza dira ya historia  ya kibinadamu.

Mpango wa kuwasha taa minara ya miji unaungwa mkono zaidi ya miji 2000

Hayo yameelezwa na Mario Marazziti  wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Jumuiya ambayo tangu mnamo mwaka 2000 imekuwa mstari wa mbele kwa kuandaa tukio la kuwasha taa katika Gofu la Kale,  mahali ambapo enzi zile za utawala wa kirumi ulikuwa ni uwanja wa kuua watu kupitia wanyama wakali na michezo migumu na mikali ya kifo;  kwa maana hiyo  mwanga wa taa hizo ni dhidi ya adhabu ya kifo. Ni mpango ambao kwa kadiri ya kipindi kinavyopita, umeweza kuungwa mkono zaidi ya miji 2000 ambayo itawasha taa ya minara yao mashuhuri ili kuweza kwa pamoja kupinga mateso.

Wao ni Miji kwa ajili ya Maisha

“Wao ni Miji kwa ajili ya Maisha”,  ndiyo harakati inayohusisha maelfu ya watu katika mabara yote na ambalo limefanikiwa kupitia dhamira ya pamoja ya wagonjwa na uhusiano na serikali mbalimbali, katika kupunguza idadi ya nchi zilizobaki. Kwa upande wa Marazziti amesisitiza kwamba bado kipande cha njia, ambacho kinatazama nchi karibu 10 au 12 hivi katika mataifa ambayo bado  yanatumia adhabu ya kifo. Nchini Marekani, kuna serikali tano kati ya serikali zake ambazo mwaka huu wameua watu wenye adhabu ya kifo.

Kusitishwa na kufutwa adhabu ya kifo

Ni miaka zaidi ya 20, kwa maana hiyo Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ikiwa inaalaani vikali  hukumu ya adhabu hiyo ya kihistoria ambayo imepita kutoka watu 3,700 kufikia vifo chini ya elfu tatu. Aliyesaidia mabadiliko haya ya kitabia ambayo yamepelekea kuona au baadhi ya kesi za kifo, bilashaka ni mabadiliko ya kusikiliza ulimwengu, kwa mujibu wake Marazziti. Hii kama ilivyokuwa mateso na utumwa, ambayo ilionekana kuwa haiwezi kuvumilika kwa dhamiri ya mwanadamu, hii hukumu ya kifo sio hisia sawa, japokuwa  kwa upande wa Marazziti, amesema inaonekana kuwa haiwezi kuzuilika, pia kufikiria juhudi zilizofanywa za kuunganisha wakati wa kupingana, ambao ulisababisha mgawanyiko kati ya wale ambao wanakubali hata kusitishwa na wale ambao badala yake walitetea kufutwa kwake.

Papa Francisko analaani adhabu ya kifo

Mabadiliko yalikuwa ni hatua kuelekea kusitisha, kwani katika karne ya XX kulikuwa na migawanyiko kuhusu muktadha huu, leo hii hisia ni za pamoja na ambazo haziwezekani kukatazwa. Suala la kupinga adhabu ya kifo ni juhudi ambayo ipo inatoa mchango mkubwa kwa Umoja wa Nchi za Ulaya (UE) na hata mataifa binafsi, kuanzia na Italia, lakini hata zaidi na Baba Mtakatifu. Papa aliweka wazi juu ya mtazamo wake  Vatican. Adhabu ya kifo haikubaliki, alisema huku akibainisha kwa namna ya kweli iliyoungwa mkono tayari  na mapapa wa kipindi cha baada ya vita  vya dunia hadi leo hii, kuanzia  na Papa Paulo VI, Yohane Paulo II na Papa mstaafu Benedikto XVI. Kwa maana hiyo Gofu la Kale, maarufu sana jijini Roma litawashwa taa tarehe 30 Novemba 2022, saa 12.30 masaa ya Ulaya,  na kutakuwa na afla ambapo watasoma  baadhi ya barua zilizoandikwa na wale waliohukumiwa adhabu ya kifo.

Kupinga adhabu ya Kifo

 

30 November 2022, 10:34