Tafuta

Barafu katika baadhi ya maeno dunia inahatari ya kutoweka ifikapo 2050 kwa mujibu wa utafiti uliobainisha na UNESCO Barafu katika baadhi ya maeno dunia inahatari ya kutoweka ifikapo 2050 kwa mujibu wa utafiti uliobainisha na UNESCO 

UNESCO,barafu katika maeneo ya Urithi wa ubinadamu itayeyuka ifikapo 2050

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya UNESCO imebainisha juu ya harati ya kuyeyuka kwa barafu katika maendo ya urithi wa kibinadamu ifikapo 2050.Lakini bado inawezekana kuokoa theluthi mbili nyingine,ikiwa ongezeko la joto ulimwenguni halitazidi nyuzi 1.5°C ikilinganishwa na kipindi cha kabla ya viwanda.

Na Angella Rwezaula-Vatican.

Takwimu mpya za Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni {UNESCO} ambayo inamulika kasi ya kuyeyuka kwa barafu katika maeneo ya Urithi wa Dunia, na barafu katika theluthi moja ya maeneo  zitatoweka ifikapo 2050. Lakini bado inawezekana kuokoa theluthi mbili nyingine, ikiwa ongezeko la joto ulimwenguni  halizidi nyuzi 1.5°C ikilinganishwa na kipindi cha kabla ya viwanda. Hii itakuwa ni changamoto kubwa ya kuelezea katika Mkutano Mkuu wa COP27 utakaofanyika nchini Misri. Maeneo 50 ya Urithi wa Dunia wa UNESCO ni nyumba ya barafu, ikiwakilisha karibu asilimia 10% ya eneo lote la Dunia lililo na barafu. Zinajumuisha zile za juu zaidi (karibu na Mlima wa  Everest), ambao ni mrefu zaidi huko Alaska) na ulimwenguni na barafu za mwisho zilizobaki barani Afrika, miongoni wakitoa muhtasari wa kuwakilishi hali ya jumla ya barafu ulimwenguni.

Mabadiliko ya Tabia nchi kuathiri uso wa dunia ifikapo 2050 kama hakuna hatua ya kupunguza joto
Mabadiliko ya Tabia nchi kuathiri uso wa dunia ifikapo 2050 kama hakuna hatua ya kupunguza joto

Kwa maana hiyo utafiti mpya wa UNESCO,  lakini kwa ushirikiano na IUCN, unaonesha  kuwa barafu hizi zimekuwa zikipungua kwa kasi tangu mwaka 2000 kutokana na uzalishaji wa hewe chafuzi {CO2} ambao ni joto la juu. Kwa sasa inapotea tani bilioni 58 za barafu kila mwaka, sawa na matumizi ya maji ya kila mwaka ya nchi ya Ufaransa na Uhispania na inawajibika kwa karibu asilimia 5% ya kuongezeka kwa usawa wa bahari ulimwenguni. Suluhisho moja tu la ufanisi: ni punguza haraka uzalishaji wa hwe chafuzi CO2. Kwa maana hiyo katika kuhitimisha Ripoti wanasema barafu katika theluthi moja ya maeneo 50 ya Urithi wa Dunia iko hatari ya kutoweka ifikapo mwaka 2050, bila kujali juhudi za kupunguza ongezeko la joto. Lakini bado inawezekana kuokoa barafu katika theluthi mbili iliyobaki ya tovuti ikiwa ongezeko la joto halizidi 1.5°C ikilinganishwa na kipindi cha kabla ya viwanda.

Kwa mujibu wa Audrey Azoulay, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO alisema “Ripoti hii ni wito wa kuchukua hatua. Kupungua kwa kasi tu kwa viwango vyetu vya uzalishaji wa hewa chafuzi CO2 ambako kunaweza kuokoa barafu na bioanuwai ya kipekee inayotegemewa. COP27 itakuwa na jukumu muhimu la kusaidia kupata suluhisho kwa suala hili. UNESCO imedhamiria kuunga mkono mataifa katika kutekeleza lengo hili”. Mbali na kupunguza kwa kiasi kikubwa cha uzalishaji wa kaboni, UNESCO inatetea kuundwa kwa hazina ya kimataifa ya ufuatiliaji na uhifadhi wa barafu. Mfuko kama huo ungesaidia utafiti wa kina, kukuza mitandao ya kubadilishana kati ya washikadau wote na kutekeleza tahadhari za mapema na hatua za kupunguza hatari za maafa.

Nusu ya wanadamu inategemea moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja juu ya barafu kama chanzo chao cha maji kwa matumizi ya nyumbani, kilimo na nishati. Miundo ya barafu pia ni nguzo za bioanuwai, inayolisha mifumo mingi ya ikolojia. Miamba ya barafu inapoyeyuka kwa kasi, mamilioni ya watu hukabiliwa na uhaba wa maji na hatari inayoongezeka ya majanga ya asili kama mafuriko, na mamilioni zaidi wanaweza kuhama makazi yao kwa sababu ya kuongezeka kwa kina cha bahari. Utafiti huu unaangazia hitaji la dharura la kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi na kuwekeza katika Masuluhisho ya Asili, ambayo yanaweza kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuruhusu watu kukabiliana vyema na athari zake,” alisema Dk. Bruno Oberle, Mkurugenzi Mkuu wa IUCN.

VYANZO VYA MAJI NA NISHATI VITUNZWE
03 November 2022, 14:47