Tafuta

Watoto wanapata shida katika nchi zenye migogoro kama Yemen, Siria,  kwa ujumla Nchi za Mashariki ya Kati. Watoto wanapata shida katika nchi zenye migogoro kama Yemen, Siria, kwa ujumla Nchi za Mashariki ya Kati. 

UNICEF imezindua ombi la kuongeza zaidi ya dola bilioni 2.6 kwa 2023

Watoto wa eneo la Mashariki ya kati ni wahitaji zaidi duniani.Eneo hilo ni mwenyeji wa baadhi ya migogoro iliyodumu kwa muda mrefu zaidi duniani:Nchini Siria,baada ya takriban miaka 12 ya vita,watoto milioni 6.5 wanategemea usaidizi.Nchini Yemen,wanakabiliwa na mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu duniani kwa karibu watoto wote nchini humo wanategemea usaidizi.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Kama sehemu ya wito wa kimataifa, UNICEF inaomba ufadhili wa dharura wa dola bilioni 2.6 zaidi ili kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa zaidi ya watoto milioni 52.7 wanaohitaji katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kwa mwaka 2023. Huku karibu nusu ya nchi katika eneo hilo zikikabiliwa na shida, migogoro au kukabiliwa na athari za migogoro na vita, watoto wanasalia kuwa walioathirika zaidi na wanaohitaji msaada zaidi, alisema  hayo Adele Khodr, Mkurugenzi wa UNICEF wa Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. Kwa mujibu wake: “Mwaka baada ya mwaka, hali inazidi kuwa mbaya zaidi na familia nyingi zinakuwa maskini kutokana na athari za migogoro mingi”.

Migogoro Yemen, Siria, Lebanon na Sudan

Baadhi ya migogoro inayodumu zaidi ulimwenguni hufanyika katika eneo hilo. Kama matokeo ya karibu miaka 12 ya vita nchini Siria, watoto milioni 6.5 wanategemea msaada. Yemen ndio mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu duniani, ambapo karibu watoto wote nchini humo wanategemea msaada. Mgogoro unaozidi kuwa mbaya nchini Lebanon na ukosefu wa utulivu nchini Sudan ulimaanisha kuwa mamilioni ya watoto zaidi wanaishi katika hali mbaya. Kwa maana hiyo:  “Iwapo zitapatikana, fedha hizo za dharura zitawezesha UNICEF kufikia watoto walioathiriwa na migogoro na migogoro ya kibinadamu kwa wakati na kwa njia inayofaa. Na UNICEF inawashukuru wafadhili wote ambao wamesaidia katika kuwezesha kukabiliana na mahitaji ya watoto katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. Fedha kwa wakati, zinazotabirika na zinazobadilika ni muhimu kuchangia ustawi na afya ya watoto katika kanda,” alihitimisha kueleza Bi Khodr.

Kuhamasisha rasilimali muhimu katika kuingilia kati maeneo yaliyoathirika

Kwa miaka mingi, UNICEF imechukua mbinu ya kimkakati ya kukabiliana na migogoro na migogoro katika kanda, ikilenga sio tu kutoa msaada wa haraka wa kibinadamu, lakini pia katika kuimarisha mifumo, kuunda programu zinazozingatia hatari na mipango na maandalizi ya dharura. UNICEF ilitambua umuhimu wa kujumuisha jumuiya za mitaa na uwajibikaji kwa watu walioathirika, kufanya kazi na washirika wa kikanda kuwawezesha wasichana na wavulana na kukuza ushiriki wao katika mipango ya kibinadamu. Juhudi pia zimelenga katika kuendeleza ubia na kuhamasisha rasilimali muhimu ili kuhakikisha maendeleo ya muda mrefu na athari. Mnamo 2022, UNICEF iliendelea kujibu mahitaji ya watoto na familia zao katika kanda.

Unicefu inaomba ufadhili kwa ajili ya kusaidia watoto walioko katika maeneo ya vurugu na vita
14 December 2022, 14:04