UN:Takriban raia elfu 7wamekufa na elfu 11 kujeruhiwa Ukraine tangu kuanza vita
Na Angella Rwezaula; - Rwezaula.
Jeshi la Ukraine limejiandaa kujibu mashambulizi mapya yanayoweza kufanywa na wanajeshi wa ardhini wa Urussi kutoka Belarus kuelekea mji mkuu Kyiv. Kwa maana hiyo, nafasi za ulinzi kaskazini mwa nchi hiyo tayari zimeandaliwa na kuimarishwa. Rais wa Ukraine, Bwana Volodymyr Zelensky, katika ujumbe uliorekodiwa kwenye sherehe ya kutoa tuzo ya Golden Globe alithibitishwa kwamba hakutakuwa na Vita vya Kidunia vya Tatu, na kwamba, kwa msaada wa ulimwengu huru, Ukraine itasimamisha uchokozi wa Urussi kwenye ardhi yao. Na wakati Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) na NATO zikithibitisha uungaji mkono wa kijeshi kwa nchi hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani alisita kupeleka vifaru vya Leopard huko Kyiv.
Papa: Ukraine inakabiliwa na mateso ya kikatili,daima iko katika mioyo yetu
Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya katekesi yake, Jumatano tarehe 11 Januari 2023, kwa mara nyingine tena aliomba kuendelea kuombea nchi hiyo ambayo "inakabiliwa na mateso ya kikatili" a kwa hiyo watu hao wako moyoni mwake kila mwata. Umoja wa Mataifa (UN), wakati huo huo, umethibitisha kifo hicho hadi sasa cha watu 6,952 na kesi 11,144 za majeruhi ya raia nchini Ukraine kufuatia uvamizi kamili wa Urussi ulianza mnamo tarehe 24 Februari 2022. Hata hivyo, Umoja wa Mataifa ulisisitiza kwamba idadi halisi ya vifo inaweza kuwa kubwa zaidi, kwa sababu kuna ucheleweshaji wa kupokea taarifa kutoka kwa baadhi ya maeneo ambako mapigano yanaendelea na ripoti nyingi bado hazijathibitishwa. Kulingana na Wafanyakazi wakuu wa Vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine, Urussi badala yake ianakadiriwa kupoteza watu 112,960 katika safu yake tangu siku ya shambulio la Moscow dhidi ya Ukraine, tangu Februari 24 iliyopita.
Vita
Warussi walishambulia Kharkiv saa chache baada ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock. Wakati huo huo, kundi la wanajeshi Urussi Wagner limetangaza kuwa watu wake wameudhibiti mji wa Soledar, mji wa mashariki mwa Ukraine wenye migodi ya chumvi. Jiji lingezingirwa na idadi ya wafungwa hata hivyo ilikuwa imetangazwa. Japokuwa taarifa kutoka mji mkuu Kyiv lilikanusha unyakuzi wa Urussi wa Soledar.
Ukraine:baada ya Noeli suluhisho la mapigano ni makali
Ulaya na NATO inathibitisha kutoa msaada wa kijeshi kwa Ukraine. Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani, hata hivyo, inasitasita kutuma vifaru vya 'Chui'. Wakati Italia itaendelea “kufanya sehemu yake nchini Ukraine ambayo ni tayari kutuma silaha zaidi kwa lengo la kufikia amani ya haki ambayo inatambua uhuru wa Kyiv”. Hii imesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje Bwana Antonio Tajani, huku akisisitiza kwamba Roma inafanya kila iwezalo katika Bunge, ikiongeza michango ya kiuchumi kwa milioni 10, za kutuma zaidi ya tani 50 za nyenzo kwa ajili ya ujenzi wa mkondo wa umeme wa nchi ilioharibiwa kutokana na mashambulizi ya Moscow”.