Tetemeko la ardhi:zaidi watu elfu 21 wamekufa,huduma ya kwanza yawasili Siria!
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Takwimu za kusikitisha za janga la tetemeko la ardhi lililopiga kusini mwa Uturuki na kaskazini mwa Siria tarehe 6 Februari bado linaongezeka. Zaidi ya watu 21,000 wamethibitishwa kufariki kufikia sasa katika nchi hizo mbili. Kuna zaidi ya waathrika 17,000 nchini Uturuki na zaidi ya 3,000 nchini Siria. Kadiri maasa yanavyozidi uongezeka ndivyo wanazidi kuwapata majeruhi ambapo wanaeleza hadi sasa ni 75,000. Wakati huo huo, shughuli za uokoaji na utafutaji zinaendelea; huko Malatya mwanamke mjamzito alibaki chini ya vifusi kwa masaa 82, wakati katika mkoa wa Hatay, pia katika eneo la Uturuki, msichana wa miaka 10 alipatikana akiwa hai baada ya masaa 90, shukrani kwa kazi ya timu zilizowasili kutoka nchi 53 tofauti kwa jumla ya waokoaji wa kigeni 6,153.
Kwa hiyo Juhudi za utafutaji zinaendelea bila kupunguzwa, kwa kutomia vikosi maalumu, lakini nafasi za kupata manusura zinapungua. Idadi ya watu waliohamishwa na ulinzi wa raia wa Uturuki kutoka eneo lililoharibiwa na tetemeko la ardhi imezidi 35,000. Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameahidi kwamba “hakuna mtu atakayeachwa bila makao” na amehakikisha ujenzi mpya wa haraka ndani ya mwaka mmoja na lira 10,000 za Kituruki - sawa na karibu euro 500, kwa kila mtu aliyeathiriwa na tetemeko la ardhi. Kwa jumla, mataifa 95 yametoa msaada kwa Uturuki katika siku hizi ngumu.
Pia nchini Siria, msafara wa kwanza wa misaada kwa maeneo ya waasi ulifika, kupitia ukanda wa kibinadamu wa Bab al-Hawa, ambao kwa sasa ndio pekee: malori sita yalipeleka mablanketi, magodoro, mahema, nyenzo za misaada na taa za jua. Uturuki imeahidi kufungua vivuko viwili zaidi vya mpaka kwa ajili ya misaada zaidi ya kibinadamu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana António Guterres amesema yuko tayari kwa wazo la kupeleka misaada kwa watu walioathiriwa na tetemeko la ardhi nchini Siria kupitia vivuko vingine, pamoja na lile la Bab al-Hawa, akiongeza kuwa mashirika mengi ya kibinadamu yasiyo ya Umoja wa Mataifa tayari yanawasilisha kupitia njia zingine. Msaada umefika kutoka Urussi na Iran na mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni Tedros Adhanom Ghebreyesus pia atakwemda huko, ambaye katika ukurasa wake wa Twitter alitoa taarifa juu ya msaada wa WHO katika maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi la hivi karibuni, kulingana na kazi ya muda mrefu nchini kote. Ili kuunga mkono juhudi za misaada na uokoaji, Benki ya Dunia ilitangaza msaada wa dola bilioni 1.78 kwa Uturuki.