Maandamano ya Israel. Maandamano ya Israel. 

Israel,Waziri Mkuu Netanyahu asitisha mageuzi ya haki yenye utata

Mafanikio huko Israel ili kukabiliana na wimbi la maandamano dhidi ya mageuzi ya haki mahakamani.Waziri Mkuu Netanyahu amesitisha sheria hiyo yenye utata hadi sherehe za Pasaka na kuwataka wapinzani kujadiliana kuhusu sheria hiyo kwa marekebisho yanayofaa.

Na  Angella Rwezaula, - Vatican.

Waziri Mkuu Benjamini Netanyahu ameyatoa matamshi hayo Jumatatu usiku 27 Machi mjini Yerusalem na kusema kwamba ameamua kusitisha mpango wa kuwasilisha na kuyasoma mapendekezo yake kwa mara ya pili na ya tatu katika kikao cha bunge, hivyo muswada huo hautapelekwa bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura hadi mwishoni mwa mwezi Aprili. Kwa mujibu wa Netanyahu, wako katikati ya mzozo ambao unatishia umoja wao, hivyo kila mtu anapaswa kuchukua hatua kwa kuwajibika. Waziri Netanyahu  hata hivyo alionya kuhusu vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo havipaswi kutokea. Kwa mujibu wake alisema: “Iwapo kuna uwezakano wa kuzuia vita vya wenyewe kwa wenyewe kupitia mazungumzo, mimi, kama waziri mkuu, nimeamua kufuata njia ya mazungumzo. Ninatoa fursa hii kuhakikisha tunafanya mazungumzo ya kweli na yanayofaa."

Maandamano nchini Israel
Maandamano nchini Israel

Mapema Jumatatu, 27 Machi, hata hivyo Waziri wa Usalama wa Ndani wa Israel, Itamar Ben-Gvir alisema kuwa yeye pamoja na Netanyahu wamekubaliana kuahirisha mageuzi hayo. Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, Ben-Gvir na Netanyahu walikutana kabla, kwa ajili ya kikao cha dharura ambacho inasemekana Ben-Gvir alitishia kujiuzulu iwapo Netanyahu asingezingatia mipango ya mageuzi.

Maandamano makubwa sana huko Israeli 27 -28 Machi 2023
Maandamano makubwa sana huko Israeli 27 -28 Machi 2023

Haya yote wakati yanafanyika na  maandamano yakiendelea uwanjani  wakiwemo mabalozi wa kigeni, wamezuiwa kabisa kutokana na mgomo huo mkuu. Lakini hatua ya Netanyahu sasa inaupelekea mjadala huo kwenye ngazi ya kisiasa, ukihusisha washirika wa kijamii na  wa upinzani juu ya mageuzi ambayo yangepunguza mamlaka ya Mahakama ya Juu, na kutoa mamlaka makubwa kwa sera ya uteuzi wa majaji. Rais wa Israel, Bwana  Isaac Herzog ameipongeza hatua ya kusitishwa kwa mpango wa mageuzi, akisema sasa ni muda wa kuanza mazungumzo ya dhati na yenye uwajibikaji ambayo yatapunguza mivutano iliyopo. Bwana Herzog ametoa wito kwa pande zote kuwajibika ipasavyo na kwamba wote wabakie wamoja na kuwa ni taifa moja la Wayahudi na lenye kufuata demokrasia.

Watu wa Israel wanataka Demokrasia
Watu wa Israel wanataka Demokrasia
29 March 2023, 12:40