Makamu Rais wa Marekani ziarani nchini Ghana,Tanzania na Zambia!
Na Angella Rwezaula,- Vatican.
Makamu Rais wa Marekani Bi Kamala Harris alianza ziara yake ya Barani Afrika kwa Juma moja kuanzia tarehe 26 Machi na atahitimisha mnamo tarehe 2 Aprili 2023 ambapo anatembelea nchi tatu kuanzia na Ghana, Tanzania na hatimaye Nchini Zambia. Akiwa nchini Gana mnamo Jumanne tarehe 28 Machi Bi Kamala alifanya ziara yake katika jengo lililokuwa lango la kuwapitisha watumwa waliosafirishwa kutoka Afrika kwenda bara Amerika na visiwa vya Karibeani, lililo katika mji wa mwambao wa Cape Coast nchini Ghana.
Jengo hilo limewekwa katika orodha mirathi za dunia. Bi Kamala Harris akiwa hapo aliweka shada la maua kwa ajili ya heshima ya watu waliopoteza maisha yao katika biashara mbaya ya watumwa na wakati wa kutoa neno alisema kuwa historia hiyo inapaswa kufundishwa nchini Marekani.
Hata hivyo kabla hapo alitoa hata wito wa uwekezaji zaidi katika sekta ya uvumbuzi barani Afrika huku akielezea matumaini yake makubwa kwa mustakabali wa bara hilo. Tarehe 29 Machi 2023, Bi Kamala anatua Nchini Tanzania na kituo cha mwisho cha ziara yake barani Afrika kitakuwa nchini Zambia.