Siku ya Kimataifa dhidi ya ubaguzi:Kampeni#UPprezzami ya harakati ya vijana ya Save the Children
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Imechapishwa video mpya ya vijana kwa ajili ya kusema hapana kuwa na hukumu na kunyanyapaa. Ubaguzi unakataa hadhi ya mtu binafsi, na hivyo kumpunguza kuwa wa kikundi kinachotambulika: hata kabla ya kutambuliwa kama mtu binafsi wenye sifa za kibinafsi, wasichana, wavulana na vijana wananyanyapaliwa kama washiriki wa kikundi, kinachofafanuliwa kwa misingi ya kitabaka potofu kama vile umri, utaifa , makundi yenye asili ya kabila moja, ulemavu, mwelekeo wa jinsia na mengine. Vivyo hivyo, mtindo wa mwonekano wa nje unahusu kila kitu ambacho kimeainishwa kwa mtazamo wa kwanza, kama vile rangi ya ngozi, jinsia, sifa za mwili, mavazi na katika hali nyingi husababisha kumhukumu mtu kwa njia ya juu juu na isiyo sahihi.
Huu ndio ujumbe ambao Jumuiya ya Vijana ya Save the Children inataka kuzindua katika maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Ubaguzi Duniani, kupitia kampeni ya "UP-prezzami" dhidi ya dhana potofu, iliyotungwa na kuzinduliwa na wasichana na wavulana zaidi ya 500 kati ya umri wa miaka 14 na 25, iliyojitolea kuhamasisha haki za watoto na vijana. Harakati hiyo wakifuatiwa na wataalamu wa masuala ya mawasiliano walitaka kuweka nuru mada inayowagusa kwa karibu na ambayo wanaamini inazungumzwa kidogo sana. Ili kufanya hivyo, walichagua video ambayo unaonesha umri wao ambao umewekwa na picha ambayo, hata hivyo kama kufungwa kunapendekeza, mara nyingi kuna hatari ya kupotosha. Na swali ambalo wanataka kuuliza wenzao ni: Je! una uhakika kwamba chaguo bora ni kutegemea kuonekana?”
Save the Children inasisitiza umuhimu wa mipango ya aina hii, ambayo huanzia na vijana, kwa sababu wao ndio wa kwanza kupata hali hizi ambazo mara nyingi zinaweza kuwa na athari kubwa. Kuhusika kwa rika ni muhimu kuwatenga wale wanaofanya vitendo vya kibaguzi, sio kupunguza dalili yoyote ya kufungwa kwa tofauti na kueneza utamaduni wa kuheshimu haki za kila mtu, shuleni na katika maeneo mengine ya mikutano. Shule hasa inaweza na lazima iwe na jukumu muhimu katika kukuza utamaduni wa kukubalika, kuelimisha kwa heshima kwa utofauti na hisia, kukuza matumizi ya lugha chanya na isiyo ya kibaguzi, kupendelea fursa za kukutana, maarifa na urutubishaji mtambuka kwa utofauti. Harakati ya Vijana wa Save the Children, ambalo linajumuisha vikundi vya vingine vya SottoSopra na timu ya wahariri ya Change the Future, inawakilisha nafasi ya kudumu ya ushiriki.