Tafuta

2022.08.06 Fao Africa occidentale e del Sahel

Fao,Ocha,Unicef na Wfp:shaka juu ya chakula na utapiamlo Afrika/kati&magharibi

Utafiti mpya wa FAO,OCHA,UNICEF na WFP umebainisha kuwa uhaba wa chakula na utapiamlo katika Afrika Magharibi na Kati upo katika kiwango cha juu cha miaka kumi na mgogoro huo umeenea kwa nchi za pwani.Kwa ukanda wa Sahel,kwa mara ya kwanza watu 45,000 wanatarajiwa kukumbwa na viwango vya juu vya janga la njaa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Ifikapo mwezi Juni mwaka huu 2023 uhaba mkubwa wa chakula utakuwa wa juu zaidi katika muongo mmoja katika Afrika Magharibi na Kati, kulingana na utafiti mpya uliofanywa na mashirika ya FAO, OCHA, UNICEF na WFP. Mashirika hayo ya Kimataifa  yana wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa uhaba wa chakula katika nchi za pwani na viwango vya janga la njaa vinavyoathiri maeneo yaliyoathiriwa na migogoro kama nchini Burkina Faso na Mali, ambapo ukosefu wa usalama ni kikwazo kikubwa kwa usaidizi wa kibinadamu. Katika ukanda wa Sahel, kwa mara ya kwanza watu 45,000 wanatarajiwa kukumbwa na viwango vya janga la njaa (Awamu ya 5),  kwenye ukingo wa njaa  ikiwa ni pamoja na 42,000 nchini Burkina na 2,500 nchini Mali. Athari za pamoja za migogoro, majanga ya hali ya tabianchi, UVIKO-19 na bei ya juu ya vyakula zinaendelea kuzidisha njaa na utapiamlo katika eneo hilo.

Migogoro ya kivita na kisilaha inasababisha uhaba wa Chakula Afrika ya Kati na magharibi
Migogoro ya kivita na kisilaha inasababisha uhaba wa Chakula Afrika ya Kati na magharibi

Kulingana na uchanganuzi wa suala la usalama wa chakula kwa mwezi Machi 2023 wa Cadre Harmonisé, ni kubainisha kuwa idadi ya watu wasio na upatikanaji wa mara kwa mara wa chakula salama na chenye lishe bora inaweza kuongezeka hadi milioni 48 wakati wa msimu wa kiangazi (kuanzia Juni-Agosti 2023), kutokuwa na  ongezeko mara nne katika miaka mitano iliyopita. Matokeo hayo pia yanathibitisha mwelekeo wa muda mrefu kuelekea upanuzi wa uhaba wa chakula katika kanda. Kwa hiyo mzunguko wa usalama wa chakula na lishe katika Afrika Magharibi ni mbaya zaidi kwa mujibu wa  Chris Nikoi, Mkurugenzi wa WFP wa Kanda ya Afrika Magharibi. Kwa upande wake amesema “Kuna hitaji muhimu la uwekezaji mkubwa ili kuimarisha uwezo wa jamii na watu binafsi kustahimili mishtuko, kutoa kipaumbele kwa masuluhisho ya ndani na ya muda mrefu ya uzalishaji wa chakula, usindikaji na ufikiaji wa vikundi vilivyo hatarini”.

Hali ya lishe ambayo tayari ni mbaya kwa jamii katika eneo lote pia inazidi kuwa mbaya, huku watoto milioni 16.5 chini ya miaka mitano wanakabiliwa na utapiamlo wa hali ya juu mnamo 2023, wakiwemo watoto milioni 4.8 wanaougua ugonjwa huo katika hali mbaya sana. Hili ni ongezeko la 8% la utapiamlo uliokithiri duniani ikilinganishwa na wastani wa 2015-2022. Mbali na kutowezekana kwa kupata chakula cha aina mbalimbali, chenye lishe na afya (hasa kwa watoto na wanawake), migogoro na kuhama kwa idadi ya watu ni miongoni mwa sababu kuu katika hali mbaya zaidi, na kusababisha kupungua kwa upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii (afya, lishe, usafi; ulinzi wa kijamii) na kuathiri vibaya shughuli za utunzaji. Kati ya 2019 na 2023, matukio ya usalama yaliongezeka kwa 79% katika mkoa, na kusababisha watu wengi kuhama makazi yao na kufanya upatikanaji wa ardhi ya kilimo na lishe kuwa shida.

Kuongezeka kwa ukosefu wa usalama na migogoro kunamaanisha kuongezeka kwa hatari katika kanda, na kuifanya kuwa vigumu kusaidia jamii katika maeneo ya mbali, alisema Marie-Pierre Poirier, Mkurugenzi wa UNICEF Kanda ya Afrika Magharibi na Kati. Kwa kuongezea alisema kwamba wanasaidia serikali kuimarisha mifumo ya afya katika ngazi ya vituo na ngazi ya jamii ili kugundua na kutibu utapiamlo kwa mafanikio, kwa kuzingatia kuzuia. Licha ya kuboreshwa kwa viwango vya mvua mwaka wa 2022, upatikanaji na upatikanaji wa chakula bado ni tatizo kuu. Kanda inaendelea kutegemea uagizaji wa bidhaa kutoka nje, kushuka kwa thamani ya fedha pamoja na mfumuko wa bei wa juu huongeza gharama za uagizaji wa chakula katika kanda, wakati nchi zinakabiliwa na matatizo makubwa ya uchumi na changamoto. Zaidi ya hayo, kuna wasiwasi kwamba vizuizi vya kuhama kwa ubinadamu na viwango vya juu vya mifugo katika baadhi ya maeneo vinaweza kusababisha kuzorota zaidi kwa hali zinazohusiana na ufugaji na usalama.

Maendeo yenye ukame katika Afrika Magharibi na ukanda wa sahel
Maendeo yenye ukame katika Afrika Magharibi na ukanda wa sahel

Naye Robert Guei, Mratibu wa FAO wa Kanda Ndogo ya Afrika Magharibi  alisema kwamba kuendelea kuzorota kwa hali ya chakula na lishe katika Afŕika Maghaŕibi na Sahel ni jambo lisilokubalika; licha ya kuongezeka kwa uzalishaji wa nafaka, upatikanaji wa chakula kwa wananchi walio wengi bado ni mgumu kutokana na kuyumba kwa utendakazi wa soko kutokana na ukosefu wa usalama na bei kubwa ya vyakula. Mwelekeo huu utaendelea kuwa mbaya zaidi hali ya chakula na lishe, hivyo lazima tushughulikie vyanzo vya mgogoro huu kwa njia ya pamoja na mara moja. Kwa hiyo wanahitaji kuchukua hatua sasa kufufua uzalishaji wa kilimo na kufikia uhuru wa chakula katika eneo lao aliongeza kusisitiza Guei

Kwa hiyo FAO, OCHA, UNICEF na WFP walitoa wito mpya kwa washirika wa maendeleo na misaada ya kibinadamu -pamoja na sekta ya kibinafsi  kusaidia serikali za kitaifa katika kuimarisha usalama wa chakula na lishe katika eneo hilo. Hii ni pamoja na kujenga mifumo ya vyakula vinavyozingatia lishe, afya, maji, vyoo na usafi wa mazingira na programu za ulinzi wa kijamii zinazolenga makundi hatarishi kama vile wanawake na watoto wadogo. Ushirikiano unahitaji kuimarishwa ili kuzuia na kutibu utapiamlo uliokithiri miongoni mwa watoto na kukuza programu zinazolengwa za hali ya hewa zinazosaidia kupunguza hatari kubwa ya kanda ya majanga ya hali ya hewa na hatari ya kupungua kwa maliasili.

Afrika Magharibi na Kanda ya Sahel zinakumbwa na baa la njaa
Afrika Magharibi na Kanda ya Sahel zinakumbwa na baa la njaa

Mgogoro wa chakula na lishe una athari za kisekta nyingi katika hali ya maisha ya watu walioathirika katika kanda, katika maeneo ambayo tayari yanakabiliwa na migogoro ya kibinadamu na katika nchi za Afrika Magharibi na Kati. Hili linahitaji kupelekwa kwa pamoja kwa mbinu za kisekta mbalimbali kulingana na mahitaji yaliyoelezwa na wakazi, na kuwaweka watu wa Afŕika Maghaŕibi na Kati katikati,” aliongeza kusema Bwana Charles Bernimolin, Mkuu wa Ofisi ya OCHA ya Kanda ya Afŕika Maghaŕibi na Kati.

19 April 2023, 15:01