Tafuta

Kila tarehe 7 Aprili ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Kumbu Kumbu ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda. Kila tarehe 7 Aprili ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Kumbu Kumbu ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda.   (AFP or licensors)

Siku ya 29 ya Kimataifa ya tafakari ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda

Tangu mauaji ya kinbari katika kizazi,hatupaswi kusahau yaliyotokea na kuhakikisha vizazi vijavyo vinakumbuka kila wakati.Tunaomboleza zaidi ya watoto,wanawake na wanaume milioni moja walioangamia katika siku mia moja.Amesema hayo Katibu Mkuu wa UN katika fursa ya Siku ya Kimataifa ya kumbu kumbu ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda yaliyotokea 1994.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kila tarehe 7 Aprili ya kila mwaka ni moja ya kumbu kumbu ya kurasa za kutisha zaidi za historia ya kisasa kwa  mauaji ya kimbari nchini Rwanda yaliyotokea mnamo 1994. Siku hii lazima iwe kama taadhari lakini pia na zaidi ya yote kama mwanzo wa kurejesha simulizi ya  kweli ya matukio ambayo leo hii, zaidi kwa mwaka  wa 29 baadaye, bado yanafichuliwa vibaya katika ulimwengu wa Magharibi ili kuepuka kukwema  majukumu ya kimataifa. Mauaji ya kimbari ya Rwanda kwa hakika si kisa pekee ambapo mataifa makubwa ya kikoloni yaliepuka kuwakilisha ukweli halisi wa ukweli, lakini kwa hakika ni yale ambayo majaribio potofu ya maoni ya umma wa Ulaya, lakini pia kutojali kabisa kwa sehemu kubwa ya yenyewe mbele ya hatma ya maelfu ya wanaume, wanawake na watoto yaliyofanywa kuwa dhahiri zaidi na ya kushangaza.

Kumbu kumbu ya mauaji kimbari nchini Rwanda
Kumbu kumbu ya mauaji kimbari nchini Rwanda

Kwa mwaka 2023 ni kumbukumbu ya miaka 29 tangu kufanyika mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda, moja ya sura mbaya zaidi katika historia ya mwanadamu. Zaidi ya watu milioni moja, Watutsi kwa wingi, lakini pia Wahutu na wengine waliopinga mauaji ya halaiki, waliuawa kwa utaratibu katika chini ya miezi mitatu. Katika Siku hii, lazima tuwaheshimu wale waliouawa na kutafakari mateso ya wale walionusurika kwa sababu “kizazi tangu mauaji ya halaiki, hatupaswi kusahau yaliyotokea  na kuhakikisha vizazi vijavyo vinakumbuka kila wakati”. tunaomboleza zaidi ya watoto, wanawake na wanaume milioni moja walioangamia katika siku mia moja.Amesema hayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Gutterres katika fursa ya siku hii.

Historia ya kutisha kwa siku 100 nchini Rwanda 1994
Historia ya kutisha kwa siku 100 nchini Rwanda 1994

Kwa mujibu wa ujumbe wake amebainisha kuwa: “Tunaheshimu kumbukumbu za waathirika, Watutsi walio wengi mno, lakini pia Wahutu na wengine waliopinga mauaji ya kimbari. Tunatoa pongezi kwa ujasiri wa walionusurika. Tunatambua safari ya watu wa Rwanda kuelekea uponyaji, urejesho, na upatanisho. Na tunakumbuka  kwa aibu kushindwa kwa jumuiya ya kimataifa.  Kizazi tangu mauaji ya kimbari, hatupaswi kusahau yaliyotokea na kuhakikisha vizazi vijavyo vinakumbuka kila wakati. Jinsi matamshi ya chuki yanavyobadilika kwa urahisi kuwa kiashiria kikuu cha hatari ya mauaji ya halaiki na kuwa uhalifu wa chuki”.

Rais wa Rwanda akiwasha taa katika mnara wa kumbu kumbu ya mauaji ya kimbari
Rais wa Rwanda akiwasha taa katika mnara wa kumbu kumbu ya mauaji ya kimbari

Kwa hiyo “Hatupaswi kuridhika katika uso wa ukatili. Kuzuia mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya ubinadamu, uhalifu wa kivita, na ukiukaji mwingine mkubwa wa sheria za kimataifa ni jukumu la pamoja. Ni jukumu la msingi la kila mwanachama wa Umoja wa Mataifa. Kwa pamoja, tusimame kidete dhidi ya ongezeko la kutovumiliana. Hebu tuwe makini  na daima kuwa tayari kuchukua hatua. Na kiukweli tuheshimu kumbukumbu ya Wanyarwanda wote walioangamia kwa kujenga mustakabali wa utu, usalama, haki na haki za binadamu kwa wote”, alihitimisha ujumbe wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa..

Ndondoo  za mauaji haya

Kisingizio ambacho kilikuwa chanzo cha mauaji ya kimbari ni mauaji ya Rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana alipokuwa akisafiri kwa ndege ya rais na Rais wa Burundi Cyprien Ntaryamira ambaye pia aliuawa katika shambulio hilo. Kwa hakika, mnamo tarehe 6 Aprili 1994, ndege hiyo ilidunguliwa na makombora mawili ya kutoka ardhini hadi angani wakati wa kutua na kuanguka katika bustani ya makao ya rais huko Kigali, mji mkuu wa nchi hiyo. Rais Habyarimana alichukuliwa na Wahutu wenye msimamo mkali kuwa mwenye msimamo wa wastani dhidi ya kabila la Watutsi na, ingawa ushahidi wa kutosha haujapatikana wa kuunganisha safu hii ya itikadi kali na shambulio hilo kwa uhakika usio na shaka, mkondo wa matukio uliofuata ulionekana kuthibitisha dhana kwamba hawa ndio watu wenye msimamo mkali walioua marais wa Afrika. Kiukweli, karibu wakati huo huo na shambulio hilo, vizuizi vya kwanza viliibuka katika mitaa ya mji mkuu ambapo raia walisimamishwa, kupekuliwa na, ikiwa ni wa kabila la Watutsi, walipigwa risasi na kufa papo hapo.

Rais Paul Kagame wa Rwanda akihutubia wawakilishi mara baada ya kuwasha taa katika mana wa kumbu kumbu
Rais Paul Kagame wa Rwanda akihutubia wawakilishi mara baada ya kuwasha taa katika mana wa kumbu kumbu

Wakati wa usiku kati ya tarehe 6 na 7 Aprili 1994, askari, wakiongozwa na Kanali Théoneste Bagosora, wakati huo mkuu wa Wizara ya Ulinzi ya Rwanda na kumfikiria mpangaji mkuu aliyepanga mauaji ya kimbari, waliingia kwenye nyumba za viongozi wa vyama vya upinzani na kuwachinja mmoja baada ya mwingine. Alfajiri ya tarehe 7  Aprili1994  wanajeshi waliingia nyumbani kwa Waziri Mkuu Agathe Uwilingyimana aliyekuwa wanamke wa kwanza alikamatwa, hatimaye wakamuua. Wanajeshi hao hao walizuia ufikiaji wa nyumba ya Waziri Mkuu kwa kofia za bluu za Ubelgiji zilizosimamia ulinzi wake na, baada ya kumuua Uwilingyimana, waliwachukua kumi kati yao wafungwa na kuwapeleka kwenye kambi ya kijeshi. Ukweli huu pekee ulitosha tu kugeuza usikivu wa maoni ya umma wa Ubelgiji kutokana na  kile kilichotokea katika siku zilizofuata.

Rais Kagame na mke wake wakiandaa kuwasha taa katika mnara wa kumbu kumbu ya mauaji ya kimbari
Rais Kagame na mke wake wakiandaa kuwasha taa katika mnara wa kumbu kumbu ya mauaji ya kimbari

Asubuhi ya tarehe 7 Aprili,  Radio ya Mille Collines, ambayo hapo awali ilizindua jumbe hatari za chuki dhidi ya kabila la Watutsi kwa hiyo walizindua wito wa “kuwatesa na kuwaua mende wa Kitutsi”. Kuanzia wakati huo na kuendelea, msako wa kweli ulianzishwa ambao, katika siku 100 tu, ulisababisha:kuangamizwa kwa zaidi ya watu 800,000, wengi wao wakiwa wanaume wa kabila la Watutsi na baadhi ya Wahutu wenye msimamo wa wastani; kuteswa na kubakwa kwa zaidi ya wanawake 250,000, wengi wao wakiwa na VVU kufuatia ukatili walioupata; kwa zaidi ya watoto yatima 400,000. Ili kutoa wazo bora la mauaji ambayo yaliikumbua Rwanda, wastani wa watu 335 waliuawa kila saa, 6 kila dakika. Yote hayo yalitokea katika kutojali kabisa kwa jumuiya ya kimataifa, ambayo tahadhari pekee wakati huo ililenga pekee kwenye kofia kumi za bluu zilizozuiliwa katika kambi ya jela ya kijeshi. Moja ya mauaji ya kutisha sana yalifanywa huko Gikongoro, yaliyokuwa makao makuu ya taasisi ya kiufundi ya Murambi, ambapo zaidi ya Watutsi 27,000 waliuawa kinyama kiasi kwamba wakati wa usiku kutoka kwenye makaburi ya kimbari ambayo maiti zilimwagwa damu  kulowanisha hata ardhi jirani. Ili kufanya wazo la ukatili wa huu wa kikabila kuwa wazi zaidi utashangaa kwamba silaha yao haikuwa ya  mabomu, wala bunduki za mashine, kwani maelfu yote ya watu waliuawa kwa mapanga au vijiti vyenye misumari.

Rais Kagame na mke wake wakisaidiana kuwasha taa katika afla ya kumbu kumbu ya mauaji ya kimbari.
Rais Kagame na mke wake wakisaidiana kuwasha taa katika afla ya kumbu kumbu ya mauaji ya kimbari.

Mauaji hayo yaliisha pale tu mnamo tarehe 17  Julai 1994 wakati Harakati ya Kisiasa kiitwacho Rwandan Patriotic Front (RPF), na kijeshi lililoanzishwa na Watutsi, lilipofanikiwa kuwashinda wanajeshi wa serikali. Mnamo tarehe 19 Julai, serikali ya umoja wa kitaifa ikiongozwa na FPR ilianzishwa ambayo ilijaribu kubaini wale waliohusika na mauaji ya kimbari lakini ambayo ilikuwa na athari ya kusababisha maelfu ya wakimbizi wa Rwanda wakati huu wa kabila la Wahutu, ambao wengi miongoni mwao ni wale waliohusika walijichanganya na kuokolewa na hukumu. Wakati huo huo, kipindupindu na kuhara damu vilienea miongoni mwa wakimbizi wa Rwanda waliokimbilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, na kusababisha vifo vya maelfu ya watu, na hivyo kushindwa kubainisha kwa uhakika idadi ya vifo vilivyosababishwa na mzozo huo. Ni machache tu ya athari mbaya sana, lakini hisoria hiyo ya siku 100 ilikuwa ya kutisha hasa.

07 April 2023, 15:40