Sudan:makubaliano hayakudumu ni ghasia katika mapigano
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Silaha zinaendelea kuzungumzwa nchini Sudan, ambapo hali bado ni mbaya kutokana na mapigano makali mno ambayo yamekuwa yakiendelea tangu tarehe 15 Aprili 2023 kati ya jeshi la kawaida na wanajeshi wa Kikosi cha Msaada wa Haraka ambao wanapigania udhibiti wa nchi hiyo. Makubaliano ya tarehe 21Aprili ya kusitisha mapigano kwa siku tatu katika fursa ya sikukuu ya Waislamu ambayo inafunga mwezi wa Ramadhani hayakuweza kudumu. Mapigano, mabomu na ufyatuaji risasi hayasalimishi mtu, kwani hadi sasa inakadiriwa waathirika ni 413, ikiwa ni pamoja na raia wa Marekani na mfanyakazi wa shirika la kutoa misaada wa Umoja wa Mataifa.
Kuongezeka kwa ghasia kwa kasi sana kiasi kwamba imesukuma Marekani na Uingereza kufikia uamuzi wa kuandaa uhamishaji wa balozi zao zilizopo Khartoum. Serikali ya shirikisho ya Canada pia inakusudia kusimamisha shughuli mbele ya taasisi za kidiplomasia, ambazo hata hivyo zimetangaza mipango inayoendelea kwa uwezekano wa usambazaji wa wanaume na vifaa katika uwanja huo. Wakati huo huo, serikali ya Korea Kusini imeamuru kutumwa haraka kwa kikosi cha wanamaji cha kupambana na uharamia kwenye maji ya pwani ya Sudan, ili kuwalinda raia wenzao nchini humo. Japan pia inajiandaa kwa ajili ya kuwatoa watu wake, kwa ajili hiyo, imetangaza kwamba imetuma ndege ya C-130 nchini Djibout kufanya maandalizi ya kuondoa wanajeshi wake.
Hali katika nchi hiyo ya Kiafrika itakuwa katikati ya meza ya mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya iliyopangwa kufanyika Luxembourg Jumatatu tarehe 24 Aprili 2023. Mkuu wa diplomasia ya Ulaya, Bwana Joseph Borrell, anendeleza mawasiliano na serikali za nchi zilizo karibu na Sudan, zinazochukuliwa kuwa wahusika muhimu katika kufanikisha mapatano.