Kuna ongezeko la vitendo vya ukeketaji kwa wanawake na wasichana nchini Sudan. Kuna ongezeko la vitendo vya ukeketaji kwa wanawake na wasichana nchini Sudan. 

Sudan:takribani wanawake 9 kati ya 10 wamefanyiwa ukeketaji

Kwa mujibu wa Ripoti ya 2018 ya Mbinu Rahisi ya Utafiti wa Maeneo nchini Sudan,kulikuwa na kupungua kwa maambukizi ya ukeketaji kutoka 89% mwaka 2010 hadi 83.9%.Chombo kinachofuatilia utafiti huo kilisema huduma za uhamasishaji na utetezi zaidi ya jamii 200 katika maeneo 20 yameachana na ukeketaji.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Nchini Sudan, takribani wanawake 9 kati ya 10 wamefanyiwa ukeketaji (FGM), licha ya sheria inayoufanya kuwa uhalifu tangu Julai 2020. Mbali na ukatili, unyanyasaji na unyonyaji, theluthi moja ya wasichana wenye umri wa miaka 0-14 nchini wamefanyiwa ukeketaji. Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), jambo hilo ambalo linakiuka haki msingi za mamilioni ya binadamu duniani kote, linatambuliwa kuwa ni uhalifu baada ya marekebisho ya kifungu cha 141 cha sheria ya makosa ya jinai. Na ni katika nchi hiyo ya Kiafrika kwamba maendeleo yanaanza kuonekana kwa zaidi ya jamii 1,300 Sudani yote kutangaza hadharani kuachana na mila ya ukeketaji.

Zaidi ya hayo, kwa mujibu wa Ripoti ya 2018 ya Mbinu Rahisi ya Utafiti wa Maeneo nchini Sudan, kulikuwa na kupungua kwa maambukizi ya ukeketaji kutoka 89% mwaka 2010 hadi 83.9% mwaka wa 2018. Chombo kinachofuatilia utafiti huo kilisema kuwa shukrani kwa msaada wa majadiliano ya jamii, huduma za uhamasishaji na utetezi zaidi ya jamii 200 katika maeneo 20 yaliyojitolea kuachana na ukeketaji. Shirika la Afya Ulimwenguni linakadiria kuwa zaidi ya wanawake milioni 200 wamekeketwa katika nchi ambazo mila hiyo imekithiri, na takriban wasichana milioni 3 wako katika hatari ya kukatwa kila mwaka, wengi wao kabla ya umri wa miaka 4- 15. Utaratibu huu umeenea hasa katika nchi zipatazo 30 barani Afrika na Mashariki ya Kati, lakini pia katika baadhi ya nchi za Asia na Amerika Kusini na miongoni mwa jamii kutoka maeneo haya.

Ili kufanya suala la ulinzi wa watoto kuwa gumu zaidi ni ukweli kwamba Sudan inaendelea kuwakaribisha wakimbizi kutoka nchi jirani za Ethiopia, Eritrea, Chad, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini, lakini katika miaka ya hivi karibuni pia kutoka Siria na Yemen. Mahitaji ya kibinadamu yanaendelea kukua, yakichochewa na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mzozo wa kiuchumi, uhaba wa chakula, mafuriko, magonjwa ya milipuko na ghasia baina ya jamii. Na pia ni ndani ya dharura hizo tata ambapo ulinzi wa watoto dhidi ya vurugu, unyonyaji, unyanyasaji na kutelekezwa unatiliwa shaka mara kwa mara.

17 April 2023, 15:09