Tafuta

2023.07.18Katika Mkutano wa wanadake nchini Rwanda "Women's Delivery shirika la Women Global Health lilitoa tuzo kwa wanake 12 mashujaa wa afya. 2023.07.18Katika Mkutano wa wanadake nchini Rwanda "Women's Delivery shirika la Women Global Health lilitoa tuzo kwa wanake 12 mashujaa wa afya.  

Afrika:Wanawake 12 mashujaa wa afya watunukiwa tuzo na Women Global Health!

Hafla ya kutunukiwa tuzo hiyo ilifanyika katika muktadha wa kongamano la “Women Deliver” lililofanyika kuanzia tarehe 17 hadi 20 Julai 2023 mjini Kigali,Rwanda,ambapo msisitizo uliwekwa katika kujitawala kwa chombo cha wanawake na juu ya haki za kimsingi za wanawake na wasichana wote.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Washindi wa tuzo ya kifahari ya “Mashujaa wa Afya” walitangazwa na Women Global Health, ambayo sasa iko katika toleo lake la sita kwa mwaka huu  2023 ikilenga wataalamu wa afya wa ajabu kutoka  barani Afrika. Mpango huo uliosisitizwa katika dokezo na Amref Health Africa-Italia, unalenga kutambua jukumu la msingi ambalo wanawake wnajikita nalo katika nyanja ya afya, jukumu ambalo mara nyingi halizingatiwi au kutambuliwa kidogo. Wakiwakilisha karibu asilimia 70% ya nguvu kazi katika sekta ya afya, wanawake hawa ni uti wa mgongo wa mifumo ya afya lakini bado wanakabiliwa na ukose wa usawa wa kijamii na malipo kidogo.

Kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserikali NGO linaelezea kuwa hii ni “Fursa ya kusherehekea ujasiri na kujitolea kwa wanawake hawa, ambapo mgombeaji wa Amref anajitokeza kwa kazi yake ya kipekee nchini Senegal. Hafla ya kutunukiwa tuzo hiyo ilifanyika katika muktadha wa kongamano la “Women Deliver” lililofanyika kuanzia tarehe 17 hadi 20 Julai 2023  mjini Kigali, Rwanda, ambapo msisitizo uliwekwa katika kujitawala kwa chombo cha wanawake na juu ya haki za kimsingi za wanawake na wasichana wote.  Kwa njia hiyo “Tumechagua kuwa wakunga, wafanyakazi wa afya, wataalamu wa afya, hivyo ni wajibu wetu kukaa hapa ili kusaidia jamii kuboresha afya zao,"”alisema mmoja wa washindi wa tuzo, hyo Joséphine Djiboune, mgombea wa wakunga wa Amref, ambaye alionesha dhamira isiyo na kifani katika kuboresha hali ya afya ya jamii za vijijini katika wilaya ya Médina, nchini Senegal.

Katika eneo hilo la vijijini, kwa mujibu wa taarifa , Djiboune alikuwa na lengo la wazi: la kuleta mabadiliko kwa wanawake wa kijiji, licha ya changamoto nyingi zinazosababishwa na uhaba wa huduma na uhaba wa miundombinu ya afya. Mama wa watoto watatu na mume wake wanaoishi mbali , mazza machazhe kutoka jiji la  Dakar, Djiboune walipata msukumo kutokana na uzoefu wake wa utotoni.  Kastika maelezo yake alisema kuwa “Ninawapenda sana watoto na watoto, kwa sababu nilikuwa nikipeleka  chakula dada yangu, ambaye pia ni mkunga, katika kituo cha afya cha eneo hilo. Kushuhudia furaha ya kujufungua watoto na kusaidia wanawake wenye uhitaji kumenifanya niwe na shauku ya taaluma hiyo.” Katika wilaya yake, anasimamia kituo cha afya, kutoa mafunzo kwa wakunga, kushirikiana na jamii, na kusimamia wafanyakazi wa usimamizi ili kuimarisha zaidi upatikanaji, ubora wa huduma, na haki za uzazi za wanawake. “Madaktari wanakabiliwa na changamoto kubwa huko Médina, na hakuna huduma za afya za kutosha kwa idadi ya karibu watu 200,000," alisema Djiboune.

"Wengi inawalazimu kusafiri safari ndefu kwa miguu au kwa pikipiki, mara nyingi kilomita 15, ili kuweza kufika tu kwenye kituo cha afya kilicho karibu. Mbali na kuwa eneo gumu kufikiwa, pamoja na watu maskini sana na ambao kwa kiasi kikubwa hawajui kusoma na kuandika ambao mara nyingi wanajikuta katika madeni makubwa kutokana na gharama za huduma za afya” alisisitiza. “Mashujaa 12 wa afya barani Afrika, pamoja na wanawake wote wanaofanya kazi bila kuchoka katika sekta ya afya, wanastahili kusherehekewa na kuungwa mkono katika kazi yao muhimu ili kuhakikisha maisha ya baadaye yenye afya na mafanikio zaidi kwa wote. Azimio na kujitolea kwao Shirika la Amrefu linahitimisha kwa kusema kuwa “ hututia moyo na kutusukuma kuelekea ulimwengu ambao uhuru wa mwili na haki za kujamiiana na uzazi zimehakikishwa kwa wanawake wote, popote walipo.”

Tuzo kwa wanawake 12 mashujaa wa kiafya iliyotolewa na Women Global Health (WGH)
21 July 2023, 16:52