Tafuta

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani tarehe Saba, Mwezi Julai 2023 ni “Kiswahili kwa Amani na Ustawi.” Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani tarehe Saba, Mwezi Julai 2023 ni “Kiswahili kwa Amani na Ustawi.”  

Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani 2023: Amani na Ustawi

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani tarehe Saba, Mwezi Julai 2023 ni “Kiswahili kwa Amani na Ustawi.” Lengo kuu la maadhimisho haya ni kusaidia kunogesha matumizi ya lugha ya Kiswahili kama nguvu ya amani, ustawi na maendeleo endelevu ya binadamu sanjari na mchakato wa kuimarisha tamaduni mbalimbali. Siku hii ilianzishwa na UNESCO tarehe 23 Novemba 2021 na kuanza kuadhimishwa tarehe 7 Julai 2022. Leo tunayo Historia ya Kiswahili.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO katika mkutano wake wa 41 uliofanyika mjini Paris, Ufaransa, tarehe 23 Novemba 2021 uliamua kwamba, tarehe 7 Julai ya kila mwaka itakuwa ni Siku ya Kiswahili Duniani na Siku hii ikaanza kuadhimishwa kwa mara ya kwanza kunako mwaka 2022. Azimio hili lilipitishwa na wanachama wote wa UNESCO bila kupingwa. Waswahili kutoka sehemu mbalimbali za dunia, wakafurahia sana tamko hili, kwa Umoja wa Mataifa kuamua kutoa kipaumbele cha pekee kwa Lugha ya Kiswahili. Hii ni lugha ya kwanza ya mawasiliano kutoka Barani Afrika kutambuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa na kutengewa siku maalum ya kuadhimishwa Kimataifa. Kiswahili kinatambulikana kuwa ni lugha rasmi ya kazi na mawasiliano kwenye Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Bunge la Afrika.

Takwimu zinaonesha kwamba watu zaidi ya millioni 500 wanatumia kiswahili
Takwimu zinaonesha kwamba watu zaidi ya millioni 500 wanatumia kiswahili

Lakini, ikumbukwe kwamba, Kiswahili ni kati ya lugha zinazozungumzwa na watu wengi duniani na inakadiriwa kwamba, kwa sasa watumiaji wa lugha hii adhimu wamefikia milioni mia tano. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani kwa Mwaka 2023 ni “Kiswahili kwa Amani na Ustawi.” Lengo kuu la maadhimisho haya ni kusaidia kunogesha matumizi ya lugha ya Kiswahili kama nguvu ya amani, ustawi na maendeleo endelevu ya binadamu sanjari na mchakato wa kuimarisha tamaduni mbalimbali. Katika makala hii, tunapenda kukushirikisha historia ya Lugha ya Kiswahili kwa kuzama zaidi katika: Asili ya lugha ya Kiswahili; Kiswahili kabla, Wakati na Baada ya Ukoloni. Kiswahili kilienea kupitia: elimu, dini, tawala na kilimo. Makala haya yataangalia pia mwenendo wa Kiswahili baada ya uhuru na jinsi hali ilivyo kwa wakati huu.

Historia ya Kiswahili

 

07 July 2023, 14:56