Tafuta

Umoja wa Mataifa unawanaalikwa kuadhimisha siku ya Urafiki duniani kwa mujibu wa utamaduni na desturi za jumuiya zao. Umoja wa Mataifa unawanaalikwa kuadhimisha siku ya Urafiki duniani kwa mujibu wa utamaduni na desturi za jumuiya zao.  (Vatican Media)

Siku ya Urafiki Duniani:urafiki ni hisia nzuri ya thamani katika maisha ya wanadamu

Kila Julai 30 ni Siku ya Urafiki Duniani iliyotangazwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kunako 2011 ili kukuza urafiki kati ya watu na hivyo kuchangia mshikamano umoja na amani ya dunia kupitia uhusiano kati ya jumuiya mbalimbali na tamaduni.Rafiki anahitajika kwa kuzingatia kwamba urafiki ni moja ya mali ya thamani sana katika maisha yetu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 30 Julai 2023, Baba Mtakatifu amesema “Leo tunaadhimisha siku mbili za dunia zilizoandaliwa na Umoja wa Mataifa: Siku ya Urafiki na Siku dhidi ya biashara haramu ya binadamu. Ya kwanza inahamasisha urafiki kati ya watu na tamaduni". Ya pili Siku hiyo inapambana na uhalifu unaowafanya watu kuwa bidhaa.” Kwa hiyo katika muktadha wa ya kwanza,  Siku ya Kimataifa ya Urafiki hufanyika kila mwaka mnamo Julai 30. Ilitangazwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitia azimio A/RES/65/275[1] mnamo mwaka 2011, likikumbusha umuhimu na malengo ya Azimio na Mpango wa Utekelezaji wa Utamaduni wa Amani  na sasa ni zaidi ya miaka 20 ya  Kimataifa ya Ukuzaji wa Utamaduni wa Kutotumia Vurugu na Amani kwa Manufaa ya Watoto wa Ulimwengu. Siku hii huadhimisha urafiki kati ya watu, nchi, tamaduni na watu binafsi, kwa wazo kwamba inaweza kuhamasisha juhudi za amani na kutoa fursa ya kujenga madaraja kati ya jamii na mshikamano. Baraza Kuu hili linatambua umuhimu wa urafiki kama hisia nzuri na ya thamani katika maisha ya wanadamu duniani kote. Kusadikishwa umuhimu wa kuwashirikisha vijana na viongozi wa siku zijazo katika shughuli za jumuiya zinazolenga kujumuisha kuheshimu tamaduni mbalimbali, uelewa wa kimataifa, kuheshimu utofauti na utamaduni wa amani.

Kwa njia hiyo Wanachama wote wa Umoja wa Mataifa, serikali, mashirika ya kimataifa, mashirika ya kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali wanaalikwa kuadhimisha siku hii, kwa mujibu wa utamaduni na desturi za jumuiya zao za mikoa, kitaifa na kikanda. Mwimbaji mmoja wa Italia anaitwa Antonello Venditti aliimba wimbo mmoja unaitwa “Ci vorrebbe un amico”, yaani “anahitajika rafiki” na kwa hakika anasema ukweli, ikizingatiwa kwamba urafiki ni moja ya mali ya thamani sana katika maisha yetu. Marafiki ndio watu tunaowachagua kama familia: wako kando yetu katika nyakati nzuri na katika giza. Huenda ikawa ni kwa sababu hii leo hii tarehe 30 Julai tunaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Urafiki, inayojulikana kama Siku ya Urafiki Duniani. Kwa maana hiyo ni tarehe maalum, iliyoadhimishwa duniani kote, ambayo inakuza wema, umoja, na mshikamano kutukumbusha kuwaweka watu karibu nasi angalua kidogo.

Kuna nadharia nyingi za kisayansi, zilizothibitishwa na UN, ambazo zinashuhudia jinsi urafiki kati ya watu unavyodhihirisha matokeo ya  amani na utulivu, mshikamano na kuboresha usalama wa kimataifa. Shukrani kwake, kiukweli, watu wanaweza kushinda kutoaminiana na kwa hivyo tarehe kama hiyo  haikuweza kukosea, ambayo inapenda kuinua kwa upya  maadili ya uvumilivu na udugu ili ulimwengu uweze kuwa bora zaidi ambao umegawanywa na vita na kinzani kila upande. Hata hivyo, historia ya Siku ya Urafiki Duniani ni ya zamani zaidi. Ili kupata matokeo ya kwanza ya  sherehe hizi  tunapaswa kwenda nchini Marekani na kurudi kwenye miaka ya 1919. Ilikuwa ni desturi iliyounganishwa kati ya marafiki kubadilishana zawadi, maua na kadi na kujitolea kibinafsi. Mnamo 1958, hata hivyo, itakuwa nchini Paraguay ambayo itaingiza maadhimisho haya rasimi katika kalenda.

Katika muktadha huo ndipo mnamo tarehe ya Julai 30 ilipendekezwa na mwanzilishi ‘World Friendship Crusade’  yaani Vita vya Kidunia vya Urafiki, aitwaye Ramón Artemio Bracho, ambalo ni shirika la kimataifa ambalo madhumuni yake yalikuwa kukuza urafiki kama utamaduni wa amani, kama msemo wa hekima maarufu usemavyo: “Yeyote anayepata rafiki, hupata hazina”. Ukiwa naye hukua, mnagombana na mnapendana sana. Kumshangaza rafiki kwa dokezo au ujumbe mfupi  hakika ni njia nzuri ya kusherehekea siku hii. Kwa nini usijaribu moja kati ya hayo, kwa kumuonesha na kuenzi siku ya urafiki huo?

Na katika Biblia tunakutana na maneno mazuri na historia ya urafiki. Ni nani anaweza kusasahau kwa mfano wa Urafiki kati ya Yonathani na Daudi, ambao kwa hakika ulikuwa mfano bora wa mshikamano na ujasiri; Ruthu na Naomi, au maneno kama “Kinywa chake kimejaa maneno matamu, kwa ujumla anapendeza. Basi, hivyo ndivyo alivyo mpenzi wangu, naam, ndivyo alivyo rafiki yangu, enyi wanawake wa Yerusalemu( Rej. Wimbo ulio bora 5,16). Urafiki unaweza kutufanya tuwe na maisha yenye furaha na mafanikio. Marafiki wazuri huwa na uvutano mzuri kwa wenzao na kuwasaidia kuboresha sifa zao nzuri. Na ndiyo maana Yesu mwenyewe kwa urafiki na mitume wake  alisema: “Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu. Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni(Rej. Yh 15, 15-25). Urafiki wa Yes una familia ya Marta, Maria na lazaro hadi kumlilia. Haya ni machache tu kuhusiana na urafiki. Kimsingi ni kukumbuka angalau ahayo machache katika kuenzi siku hii muhimu ya urafiki kimataifa.

Siku ya Urafiki duniani Julai 30.
30 July 2023, 09:56